Kweli kabisa mkuu.Ikitokea New comer ameanzisha uzi utasikia....peleka fb,...chuo kimefunguliwa?....jf imevamiwa na Division 5....Vi.laza wa Gram wameibukia JF.Lakini kama ni mkongwe ameanzisha uzi hata kama ni pumba, wazee wenzake watajitutumua kwenye comments ili uzi uonekane una maana.
Hayo ni tisa, kumi KE anzishe uzi.Yaani ata kama ni tusi, mizee mizima itajipendekeza na michango uchwara...utaona wakipost....hiyo avatar ni ya kwako?....njoo PM tumalizane....Upo maeneo gani?..n.k.
Lengo langu siyo kuleta matabaka kati ya ME na KE, ama kati ya wakongwe na wageni, la hasha!...Kama ikitokea mtu amepost kitu na anahitaji ushauri/maoni asaidiwe bila kujali kuwa ni KE ua ME, mkongwe ama mgeni....tushirikiane kwa pamoja ili jamii yenye uelewa ianzie hapa JF.
Jambo lingine dharau sii kitu kizuri, kama upo jf toka kuanzishwa kwake haimanishi kuwa wewe ni wa maana kuliko ambaye profile yake inasomeka...joined yesterday...Kila mtu kwa nafasi yake anaweza kutoa au kupokea mawazo ya kujenga kutoka kwa watu mbali mbali.
MWISHO: WADUMU MAKAPUKU....FIKRA ZA MAKAPUKU ZIISHI DAIMA....MILELE LIDUMU JINA LA MAKAPUKU.