Imeandikwa na @swalehmawele
[emoji344] Sijui kama wenzangu mmeliona hili, ilianza kwa Zolan Maki, ikaja kwa Seleman Matola na sasa Juma Mgunda, unajua nini kuhusu Clatous Chama na Pape Ousmane Sakho? nitakwambia kitu halafu ukichunguze siku ambayo hawa wawili watakapokuwa wakicheza.
[emoji344] Chama amepunguziwa mzigo ndani ya Simba, ndio!, Chama wa sasa anaishambulia zaidi zonal 14 ( lile eneo karibu na D ), hafanyi mikimbio mingi, hachezeshi sana timu kutokea chini, hilo jukumu lipo mabegani kwa Pape Ousmane Sakho, fatilia vizuri hili jambo.
[emoji344] Zitazame zile dribbling za Sakho kutokea chini, angalia namna anavyoitafuta space, ataingia ndani ( inverted ), atakimbia na mpira, atapiga pasi na kufanya vitu vingi kama playmaker, ni rahisi kusema kuwa playmaker wa sasa wa Simba ni Pape Ousmane Sakho.
[emoji344] Yes! ni playmaker anaetokea pembeni, anakuwa free pia, wakati ambao Pape anakuwa na mpira utamuona Chama anaishambulia zonal 14, hapa ni kumpunguzia majukumu Chama ambae alikuwa na role ya kutengeneza nafasi na kuchezesha timu, Chama wa sasa yupo kwa ajili ya kulisha zaidi.