Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220910-084856_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20220910-084912_Opera%20Mini.jpg
 
TUCHEL AKUNJA PAUNI 13 MILIONI CHELSEA
.
Thomas Tuchel ameripotiwa kuweka kibindoni mkwanja mrefu, Pauni 13 milioni (Sh 35 Bilioni) kama fidia ya kufutwa kazi Chelsea.
.
Tuchel, 49, alitupiwa virago huko Stamford Bridge na bosi mpya bilionea Todd Boehly baada ya timu hiyo kuanza msimu huu vibaya. Bilionea Boehly ni kama amefuata tu nyayo za mmiliki wa zamani wa The Blues, Roman Abramovich ambaye alikuwa akiwafungulia mageti ya kutokea makocha wake.
.
Ripoti zinafichua kwamba Tuchel kwa kuondolewa kazi jambo hilo litamfanya alipwe Pauni 13 milioni, huku benchi lake la ufundi wakilipwa Pauni 2 milioni.

…………..
Screenshot_20220910-090416_OGInsta%2B.jpg
 
REKODI YA BIG BULLETS KIMATAIFA
.
Nyasa Big Bullets Msimu uliopita iling’olewa hatua ya awali na Amazulu ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya awali kushinda ugenini bao 1-0 kabla ya kulala 3-1 nyumbani.
.
Msimu wa 2019-2020 ilitolewa na FC Platimun ya Zimbabwe na msimu wa 2018-2019 ilitolewa kwa penalti 4-3 na Gor Mahia ya Kenya baada ya sare ya 1-1 mechi zote.
Screenshot_20220910-090520_OGInsta%2B.jpg
 
AKPAN KUIKOSA BIG BULLETS
.
Kiungo Mnigeria Victor Akpan ameachwa jijini Dar es Salaam huku wenzake 24 wakitua salama mjini Lilongwe tayari kupigania timu kwenye mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa kesho Jumamosi.
.
Bado haijajulikana sababu ya Akpan kuachwa Dar.

……………………
Screenshot_20220910-090651_OGInsta%2B.jpg
 
TANZANIA itasimama kwa dakika 90 kushuhudia wawakilishi watatu katika Ligi ya Mabingwa Afrika, SIMBA, YANGA na KMKM leo wakitupa karata zao za kwanza katika raundi ya kwanza ya mashindano hayo jioni hii na usiku.
.
Lengo ni moja tu ushindi wa idadi kubwa ya mabao ili kukamilisha hesabu mapema
Screenshot_20220910-090754_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom