Makapuku Forum

Makapuku Forum

BREAKING NEWS...!!!

Rasmi Kocha wa Simba SC JUMA MGUNDA amekuwa APPROVED na CAF hivyo leo ataiongoza timu yake pale Lilongwe akiwa mkuu wa benchi la ufundi.

Upande mwingine Kocha wa Yanga SC NASREDDINE MOHAMED NABI AMEZUIA na CAF kukaa kwenye benchi la timu hiyo kwa kukosa vigezo.

Hivyo kesho benchini atakuwepo Kocha KAZE CEDRIC na Prof Nabi atakuwa jukwaani kama iliyokuwa kwa Didier Gomes Da Rosa.

BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)
Screenshot_20220910-082422_OGInsta%2B.jpg
 
Poker habari yako mkuu wangu hivi sisi mashangazi wa makapuku nini tumekukosea tukuombe hata msamaha kuna sehemu tuliona umetusema sana vibaya kupiga kwetu story ni shida kwako je hata habari tunazopost we huzioni kweli usiwe unatuchukia bila sababu mkuu usiwe na roho hiyo ya kuchukia watu tu mkuu sio vizuri kama kuna sehemu tuliwahi kukukosea sisi mashangazi wa makapuku tunaomba utusamehe.

Usimchukie hata siku moja mtu usiyemjua watu wenyewe tunaishi jf kwa I'd fake chuki ni kirusi kibaya sana mkuu kemea hiyo roho kama we ni mristo ikuondoke.
 
Scandal24

FOOTBALL ECONOMY || Geita Hovyo kwa Branding
.
Siku moja pata nafasi uwasikilize watu wanaoizunguka Geita Gold Fc, wanavyoongelea uwekezaji wa katika mpira unaweza ukadhani wao ni Manchester City au Newcastle United. Halafu ukija kuwaona ni KAUZU FC au VIGUNDO ya Temeke Mabingwa wa #Ndondocup2021.
.
Muda tunavyoongea wapo Sudani na vyombo vya Huko vinasema Timu kubwa kutoka ukanda wa Madini nchini Tanzania ipo hapa kupambana na mwakilishi wetu. Lakini kiukweli ni timu ya Hovyo, isothamini biashara na washirika wake ma wala wao wenyewe hawajielewi wanafanya nini kwenye kitu kinaitwa BRANDING.
.
Hadi naingia mitamboni, wao ndio timu ya ligi kuu ilovaa hezi zenye #KitSupplier wote wakubwa duniani. Kwanza wao wana mkataba na #Masita lakini wamevaa jezi zenye #UhlSports, #NewBallance #Adidas na #Puma. Bila woga kwenye mechi moja wanavaa Jezi zenye Kit Supplier wawili tofauti. Bila woga George Mpole kashika Mpira wa Masita jezi ya Puma na bango masita. Wanaishi Dunia yao.
.
Sasa huwa najiuliza, kwa nini wanaogopa kuwapa vijana kazi katika vilabu vyao..? Vijana wenye exposure na uwezo wa Kufanya mambo..! Lakini hawataki kutoa mashavu na matokeo yake ni aibu kwa Taifa zima, huko wanajiuliza maswali mengi sana lakini sisi hatujali. Hao Masita wanatamani kuondoka Nchi hii maana mizengwe ya MATUSI YA KIBIASHARA haikomi. Maana wanachokifanya Geita ni kuwadharau Masita licha ya Mapungufu ya kuchelewesha Vifaa kwa MASITA.
.
Che Guevara
.
NB
Weka Maneno
.
Screenshot_20220910-083727_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220910-083745_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220910-083805_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220910-083822_OGInsta%2B.jpg
 
Scandal24

FOOTBALL ECONOMY || Taaluma.
.
Kwa mujibu wa kaka yetu mchambuzi Jemedari Said Kazumari ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa soka Tanzania amethibitisha kuwa Juma Mgunda atakuwepo katika Benchi la Simba kutokana na Leseni yake kuwa Active kwa Mujibu wa CAF na TFF. Pia Mgunda Kapewa KOFIA baada ya mimi kutoka mishipa ya Shingo.
.
Kwa Mujibu wa Vyanzo Mbalimbali kocha mkuu wa Yanga Mohamed Nasreddine Nabi hatokuwepo kwenye Benchi la Yanga kwa mujibu wa Kanuni za CAF kwenye michezo yao. Hii inatokana na kocha huyo kuwa hana Leseni ya Diploma A ya Shirikisho hilo la Mpira barani Afrika.
.
NOTE
Ukiangalia mwenendo wa TTT, idara yake ya Habari na Mkuu wake wa kitengo ni watu wenye uwezo mdogo mnoo eidha kufanya kazi inavyotakiwa au kufanya kazi. Wanahitaji kusaidiwa.
.
Che Guevara
.
NB:
Kibao Kimegeula....!
Screenshot_20220910-084435_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220910-084453_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom