Makapuku Forum

Makapuku Forum

DEO KANDA UPDATES

- Nyota wa Mtibwa raia wa Kongo, Deo Kanda hatimae amepata leseni ya kuanza kuitumikia Mtibwa Sugar baada ya sakata la muda mrefu dhidi ya TP Mazembe

-Baada ya Mtibwa kuinasa saini ya Kanda, waliwekewa ngumu na miamba hiyo ya Lubumbashi ambao walidai wana mkataba na Kanda huku mchezaji mwenyewe akikakana

- Mgogoro huu ulifika mpaka FIFA na sakata limechukua zaidi ya miezi mitatu mpaka kupata ufumbuzi ambapo Mazembe wameshindwa kesi kutokana na kukosa vielelezo sahihi

- Kwa maana hiyo Kanda sasa ni ruksa kucheza mechi za Mtibwa, lakini pia tayari wamemalizana na Kitayose juu ya kulipa gharama ambazo nao walitoa kipindi wanaisaka saini yake

Screenshot_20220613-041235_OGInsta%2B.jpg
 
AISHI MANULA TRANSFER UPDATE

Nimezungumza na watu wa Simba lakini pia Wakala wa Aishi Manula kuhusu mkataba mpya wa Golikipa huyo

Simba wameshampa ofa yao ila pia kuna ofa mbili nchini Afrika Kusini, kilichopo sasa ni kuzipima ofa kisha atachagua wapi asaini

Taarifa zilizopo ni kuwa uwezekano mkubwa akasalia mitaa ya Uhuru na Msimbazi

Ila mpaka sasa bado hajasaini popote, NIMETHIBITISHA

Screenshot_20220613-041410_OGInsta%2B.jpg
 
STEPHEN AZIZ KI UPDATES

-Baada ya kutumia muda wa siku mbili kufuatilia sakata la Aziz Ki, kupitia chanzo changu nimepata yafuatayo

- Simba walipeleka ofa ya Dola 140,000 za Kimarekani kwa mwaka na mshahara wa dola 10,000 kwa mwezi lakini waligomea walitaka 150,000 kwa mwaka

-Yanga walipeleka ofa ya dola 80,000 kwa miaka miwili na mshahara wa dola 8,000 kwa mwezi

-Chanzo changu kimenipa taarifa hiyo na kuniambia anachofahamu mpaka sasa Mchezaji huyo hajasaini timu yoyote nchini Tanzania

Msimamo wa chanzo changu ndio msimamo wangu pia
Screenshot_20220613-041530_OGInsta%2B.jpg
 
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa chanzo changu cha karibu

Mchakato wa kuongeza mikataba kwa wachezaji ambao imeisha na bado wanahitajika kikosini imeenda vyema sana, baadhi wamesaini na wengine wamepewa muda wa kufanya maamuzi (Simba hawana tatizo nao)

Kuhusu sajili mpya timu bado inakimbizana na Kocha mpya ili kama itawezekana awe sehemu ya mapendekezo ya wachezaji wapya ambao timu ya Maskauti imefikisha majina mezani

Ni week na email kwa email, vikao kwa vikao na kitu cha uhakika ni kuwa wachezaji wanaowahitaji wote tayari majina yapo mezani, ikiwa pia mazungumzo yameanza kwa baadhi

Screenshot_20220613-041713_OGInsta%2B.jpg
 
Mfano fainali ya FA kati ya Yanga na Coastal Union itachezwa July 02, hivyo TFF watakuwa washatuma ombi la kuacha nafasi moja wazi ikitokea Coastal Union kachukua ubingwa wa FA basi atapata nafasi yake kimataifa

Dirisha la usajili la kimataifa bado sana kufungwa, litafungwa rasmi JULY 31 na CAF watakusanya majina yote ya wachezaji baada ya hapo

Screenshot_20220613-042223_OGInsta%2B.jpg
 
Wakati wa usajili ni wakati wa vita hakuna dhambi yoyote duniani endapo utashindwa kumsajili mchezaji either kwasasabbu umeshindwa bei yake au maelewano na terms..Leo Liverpool wamewagomea Bayern siyo kwasababu hawataki Mane auzwe lakini kwasababu ya price tu na sajili nyingi duniani zinashindikana kwasababu hizi na hakuna tatizo...hata Simba wameshindwa Kwa Adebayor.

Kwetu hapa inaonekana ni jambo la ajabu,Jana nimeshangaa Simba wanakanusha kama wamepeleka ofa may be walikanusha barua ile lakini ofa walipeleka,Yanga wao wakalazimisha Hadi picha na watu ambao ni viongozi wakapost picha hizo ,lakini hakuna picha ya mkataba na Mchezaji,tujifunze kudeal na sajili hizi in professional way,je ikitokea Leo timu zote zikashindwa kumsajili Aziz ki je mtaeleza nini mashabiki wenu ambao wameanza kupanga kikosi cha msimu ujao??

TUISHI KWENYE UHALISIA TUACHANE NA MBWEMBWE ZA MITANDAONI
Screenshot_20220613-042718_OGInsta%2B.jpg
 
TEN HAG AVUTA MPISHI OT
.
Wakati Man City na Liverpool wako busy Kusajili wachezaji huko kwa Mashetani Wekundu, Manchester United kocha wao mpya, Erik ten Hag amewaambia mabosi wa timu hiyo kwamba anataka mpishi mpya wa kantini iliyopo kwenye uwanja wa mazoezi ili wachezaji wawe wanapata chakula cha pamoja mazoezini.
.
Ombi Hilo la Ten Hag tayari limefanyiwa kazi vyema na mabosi wa Man United kwani tayari imeshaachia tangazo la kazi kwa mtu anayetakiwa.
Screenshot_20220613-043340_OGInsta%2B.jpg
 
POGBA AGEUKIA PSG
.
Kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba ambaekwa sasa yupo huru baada ya kuachana na wababe hao, ameripotiwa kubadili gia njiani na sasa anahusishwa kuwa kwenye hatua nzuri ya mazungumzo na mabosi wa PSG ili kujiunga na timu hiyo dirisha hili.
.
Awali Juventus ndiyo ilionekana kuwa na nafasi kubwa ya kuipata huduma ya staa huyu
Screenshot_20220613-043442_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom