Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,166
Yanga SC vs Namungo [NBC Premier League]
Na @swalehmawele
[emoji344] Mechi ngumu, ladha chungu kwa Yanga na mtihani mgumu kwa Namungo, quality ya vikosi, matokeo yao katika mechi za hivi karibuni na shauku ya kuutaka mchezo baina ya pande zote mbili, Yanga anataka kuendelea kuweka gape la alama na Namungo akiendelea kuzipigania nafasi tatu za juu ili kuweka heshima na historia.
[emoji344] Mara ya mwisho kukutana kwa timu hizi mbili mechi ilimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1, kabla ya hapo mechi nyengine nne walizokutana kwenye ligi nazo pia zimetamatika kwa sare, tofauti ni kwamba nne kati ya tano walizokutana jumla magoli yalifungwa kwa timu zote mbili.
[emoji344] Yapo maswali ambayo walinzi wa Namungo watatakiwa kuyajibu mbele ya washambuliaji wa Yanga ambao wamefunga magoli kumi katika mechi tano za mwisho, yapo maswali ambayo wachezaji wa Yanga watatakiwa kuyajibu mbele ya Namungo ambayo haijapoteza mechi yeyote kati ya tano walizocheza ugenini hivi karibuni.
[emoji344] Msingi wa kwanza wa Namungo mara nyingi huwa ni kupishana na Yanga, wanaamini katika quality ambayo wanayo, ni timu inayofurahia kucheza, ni timu inayofurahia kushambulia hasa kupitia pembeni ( wide ), hatari kwa Yanga itakuwa wapi? katika kuishinda pressing ya Namungo kama watamudu kuifanya katika zone ya Yanga.
[emoji344] Yanga watautaka mchezo, wapo kwenye uwanja wa nyumbani, watahitaji ku dominate na kushambulia muda wote, watakuwa kwenye ubora gani katika kuzuia nafasi hasa katika wide zao mbili, ubora wao mkubwa pengine ukawa katika kutengeneza overloads na kuizuia Namungo kuanzia kwenye eneo lao kwa kuziba njia za pasi kwenda kwa mawinga ( cut the passing lane ).
[emoji344] Mtihani wa Namungo upo katika kucheza dhidi ya quality ya Yanga, timu ambayo imezifungua timu nyingi katika ligi kuu, hata katika nyakati ambazo walikuwa na wakati mgumu bado individual ziliwabeba, mtihani wa Yanga ni kucheza kwenye quality yao ili kushinda mbele ya timu iliyowasumbua mara nyingi kwenye ligi, ni mechi nzuri ya kuitazama.