Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amesema kiasi cha akiba ya nishati ya mafuta kilichopo sasa na yale yaliyopo kwenye Meli yakishushwa yatatosha kutufikisha mpaka July 15 mwaka huu hivyo hakuna sababu yoyote ya Wananchi kuwa na hofu.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam alipokutana Na wadau wa mafuta na wakala wa uagizaji mafuta pamoja kwa lengo la kutoa mrejesho wa kamati ya uchunguzi wa wizi wa mafuta na kupokea taarifa ya hali ya mafuta nchini.

RC Makalla amesema kiasi cha mafuta yaliyopo Sasa ukijumlisha na yale yatakayoshushwa na Meli yatafanya nchi kuwa na akiba ya Lita Milioni 512.7 za Dizeli, Petrol Lita Milioni 365.5, mafuta ya ndege Lita Milioni 40 na mafuta ya taa Lita Milioni 5.9 ambapo kwa pamoja yanaweza kutumika mpaka July 15 mwaka huu.

Kutokana na Mkoa wa Dar es salaam kuwa lango kuu la biashara ya mafuta, RC Makalla amesema Serikali itaendelea kulinda na kudhibiti miundombinu ya mafuta ili kutokomeza tatizo la wizi na uchepushaji mafuta na usalama wa Wananchi ambapo amesema kwa Sasa Bomba la Mafuta lipo salama.
Screenshot_20220422-140727_OGInsta%2B.jpg
 
Ikulu ya Urusi imesema kwamba Urusi bado inasubiri majibu kutoka kwa Ukraine kuhusiana na pendekezo la maandishi la hivi karibuni juu ya mazungumzo ya amani baina ya pande hizo mbili.

Ikulu hiyo imehoji ni kwa nini Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy hana taarifa na waraka huo, baada ya Zelenskyy kudai kwamba hajaona wala kusikia kuhusu mapendekezo hayo ya Urusi, mapendekezo hayo ni pamoja na kuitaka Ukraine isijiunge na NATO na iitambue Crimea kama eneo lililo chini ya Urusi.

Msemaji wa Ikulu ya Urusi Dmitry Peskov amenukuliwa akiyarejea matamshi yake kwa mara nyingine kwamba mapendekezo yao ya karibuni yaliwasilishwa kwa wapinzani wao, kupitia kwa ujumbe wa wasuluhishi kutoka Ukraine.
Screenshot_20220422-141001_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amefanya kikao na Wadau wa Sekta ya Maji wa Handeni na kuelekeza hatua za haraka kuchukuliwa ikiwemo kusimamishwa kazi kwa Watumishi wanne wa Wizara ya Maji kutokana na kusuasua kwa kazi ya ujenzi wa bwawa la Kwankambala.

Kikao hicho kilichofanyika Dodoma na kuhudhuriwa na Viongozi wa Wilaya ya Handeni ni moja ya hatua zilizochukuliwa baada ya ziara ya kikazi ya Aweso Wilayani hapo 12 April, 2022 ambapo ilibainika kwamba Injinia anayejenga bwawa hilo amelipwa Shilingi milioni 602,859,075.66 sawa na 33% ya gharama ya mkataba na kazi iliyofanyika ni asilimia 20 tu.

Vilevile iligundulika kwamba kampuni iliyopewa kandarasi ya kazi hiyo iitwayo Civil Loth Enterprises Ltd iliondoa vifaa vya kazi katika eneo la ujenzi, ingawa ilikuwa imeongezewa muda wa utekelezaji wa ujenzi na kutokana na hali hiyo, kikao kilichoongozwa na Aweso kimeelekeza yafuatayo kufanyika kwa mapitio ya Mkataba wa nyongeza wa Mkandarasi

Hatua nyingine ni kuwasimamisha kazi Watumishi wafuatao ili kupisha uchunguzi, Hamisi Matungulu (Msimamizi wa Mradi – RUWASA Makao Makuu), Jimmy Mwanyakunga (Mhasibu Mkuu – RUWASA Makao Makuu), Amos Mtweve (Meneja Udhibiti Ubora wa Miradi na Mwenyekiti wa Bodi ya Manunuzi RUWASA Makao Makuu), Zam Mlimira (Mkurugenzi wa Manunuzi na Ugavi – RUWASA Makao Makuu).
Screenshot_20220422-141151_OGInsta%2B.jpg
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia kwa Mkurugenzi wake wa huduma na elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo imetoa ufafanuzi baada ya TRA kukutana na Timu ya Wataalam wa Kampuni ya META inayomiliki mitandao ya Facebook, Instagram na WhatsApp ambapo kwa pamoja wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu namna ya kutoza kodi katika huduma hizo nchini.

"Mkutano kati ya TRA na kampuni ya META ulikuwa ni mkutano wa awali wao kuweza kuelewa mazingira ya sheria za kodi za Tanzania na pia kuweza kutupitisha katika jinsi wanavyofanya biashara yao na wanavyotozwa kodi katika Nchi nyingine"

"Lengo ni kufikia mahali huko mbeleni ili kampuni hiyo ichangie kodi kwa pesa inayopata kutokana na biashara inayofanyika hapa nchini kupitia mitandao, Wananchi hawatakiwi kuwa na hofu yoyote kwasababu hii inahusu biashara inayofanyika na kampuni hiyo katika Nchi mbalimbali"

"Na hili sio jambo geni lipo dunia nzima, tumesikia Kenya tayari hilo lipo, Benin, Cameroon na Nchi za Ulaya ambako kampuni hizo kubwa za mitandao duniani zinachangia kodi kwa kufuata sheria za nchi husika na taratibu za kimataifa" Kayombo
Screenshot_20220422-141250_OGInsta%2B.jpg
 
Jacqueline Ntuyabaliwe ambaye ni mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, marehemu Reginald Mengi, ameshinda pingamizi alilowekewa na wasimamizi wa mirathi katika rufaa ya mirathi.

Ameshinda pingamizi hilo baada ya Mahakama kukataa hoja zote saba za pingamizi la wasimamizi wa mirathi.

Hii ni mara ya pili kwa mjane huyo kushinda pingamizi kutoka kwa wasimamizi wa mirathi hiyo wanaopinga kusikilizwa maombi yake ya mapitio
Screenshot_20220422-141425_OGInsta%2B.jpg
 
Mbunge wa Kilindi (CCM), Omary Kigua ameitaka Serikali kutoa vibali vya ajira kwa wateule wa Rais wanaowaondoa watumishi waliowakuta katika taasisi wanazopangiwa kuongoza.

Kigua ameyasema hayo leo Ijumaa Aprili 22, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mwaka 2022/2023.

Kigua amesema kuna baadhi ya watu wanaoteuliwa na Rais huwaondoa watumishi hadi 30 kwenye taasisi na kuomba vibali vya kuleta watumishi wengine.
Screenshot_20220422-141540_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom