MENEJA AFUNGUKA ULOMI KUVUNJIWA MKATABA
.
SIKU chache baada ya mshambuliaji David Ulomi [emoji1241] kuvunjiwa mkataba na klabu ya Al Hilal Omdurman ya nchini Sudan [emoji1232] meneja wa mchezaji huyo, Michael Mwebe ameweka wazi kilichosababisha nyota huyo kuachana na timu hiyo.
.
Ulomi alijiunga na Al Hilal, Oktoba mwaka jana kwa mkataba wa miaka miwili na alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
.
Mwebe amesema ni kweli Ulomi aliyewahi kukipiga Ruvu Shooting na Dodoma Jiji kabla ya kwenda Sudan, amevunjiwa mkataba, ikisababishwa na timu hiyo kutolewa katika mashindano ya kimataifa.
.
Mwebe amesema sheria za Sudan zinaruhusu wachezaji wanne wa kigeni lakini kwenye mchezo mmoja lazima wawe watatu tu na alipokuwa akipangwa Ulomi kulikuwa na sintofahamu nyingi kwa sababu ya umri wake.
.
“Ukweli ni kwamba Ulomi ni mdogo ilipotokea anatakiwa mchezaji mmoja apunguzwe kwa wale wageni haraka haraka ilikuwa kwake, kocha anampenda sana na ndio maana alikuwa anampa mechi za kucheza hata zile za kimataifa,” amesema.