Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,978
Serikali imewataka viongozi wa dini nchini kuwaelimisha waumini wake umuhimu wa kuhesabiwa katka sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Aidha, imewataka viongozi wa dini kuendelea kusaidia katika suala zima la malezi ya kiroho ili kujenga jamii yenye kumcha mungu, uadilifu na ubinadamu.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa Kutabaruku Kanisa la Bikira Maria wa Fatima Geita mwishoni mwa wiki, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi ambazo bila ya kuwa na takwimu sahihi haitaweza kupanga mipango thabiti ya matumizi endelevu ya rasilimali hizo.
‘’Viongozi wa Dini mnao waumini wengi tumieni fursa hiyo kuwaelimisha waumini wenu umuhimu wa kuhesabiwa’’ ilieleza hotuba ya Waziri Mkuu.
Alisema, zoezi la sensa ya watu na makazi ni muhimu kwa kuwa linaipatia nchi takwimu za msingi zinazotumika kutunga sera, kupanga mipango na program za maendeleo pamoja na kufuatilia utekelezaji wake.