Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220321-035300_Instagram.jpg
 
Mwenyekiti wa TLP-Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya PAROLE nchini Dk. Augustino Lyatonga Mrema ametangaza kuwa anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni katika Parokia ya Uwomboni Kijijini kwake Kiraracha Mkoani Kilimanjaro.

Mrema anafunga ndoa hiyo mara baada ya kumpoteza Mke wake Rose Mrema aliyefariki dunia mwaka jana.

Mrema amesema "Nimepata Binti mwenye umri mdogo mweupe ambaye ni chaguo langu na tutafunga pingu za maisha mara baada ya kufuata taratibu zote za kikanisa pamoja na ulipaji wa mahari"

Amesema kilichomsukuma kuoa ni kumpata Msaidizi wa kumsaidia katika maisha yake kwani yeye ni Mzee na anahitaji Mtu wa karibu wa kumwangalia na kumsaidia kwa ukaribu ambapo ameishukuru Familia yake kwa kumkubalia kuoa.
Screenshot_20220321-035651_Instagram.jpg
 
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema Urusi imeshindwa kupata udhibiti wa anga la Ukraine hadi sasa ikiwa ni karibu wiki ya nne toka ianze mashambulizi ambapo kushindwa huko kupata udhibiti ni moja ya sababu za vita yake kukosa mafanikio ambayo iliyatarajia ndani ya muda mfupi.

Taarifa za leo za kijasusi kutoka Wizara ya ulinzi ya Uingereza zimesema Urusi imeshindwa kupata udhibiti wa anga na kwa kiasi kikubwa na kuifanya ibaki kutegemea kufanya mashambulizi yake ya anga kutokea kwenye anga la Urusi.

Imefahamika kwamba lengo la Urusi kwenye Nchi ya Ukraine lilikua ni kuifikia Ikulu ya Nchi hiyo ndani ya siku mbili tu za mwanzo lakini hadi sasa hilo halijawezekana kutokana na uimara wa Jeshi la Ukraine na jinsi walivyoweza kuwadhibiti Wanajeshi wa Urusi ambapo pia kupata udhibiti wa anga la Ukraine ilikua ni moja ya malengo muhimu ya kufanikisha kwenye siku za mwanzo.
Screenshot_20220321-035839_Instagram.jpg
 
Orodha ya Nchi zenye furaha duniani kwa mwaka 2022 imetoka huku Finland ikishika namba 1 kwa mwaka wa tano mfululizo huku nafasi ya pili ikishikwa na Denmark na namba 3 ikishikwa na Iceland lakini ukiachia Nchi hizo zilizoongoza utafiti uliofanywa hadi kwenye Nchi za Russia na Ukraine ambazo zipo kwenye mapigano kwa wiki nne sasa.

Orodha hii imeitaja Russia kama Nchi namba 80 huku Ukraine ikishika namba 98 ambapo Nchi ya mwisho kabisa kwenye orodha hii ikiwa ni Afghanistan ambayo imeshika namba 146 namba ambayo pia iliishika mwaka jana.
Screenshot_20220321-040027_Instagram.jpg
 
Rapper Ye maarufu Kanye West (44) ameondolewa kwenye orodha ya Wasanii waliokua wamepangwa kutumbuiza kwenye utoaji wa Tuzo za Grammy Las Vegas wiki mbili zijazo, Msemaji wa Ye amesema walipokea simu kutoka kwenye Academy kuwajulisha kuwa Ye ameondolewa ambapo sababu inayodhaniwa kuwa ni kuhusu tabia zake za mtandaoni.

Mitandao ya Marekani imeripoti kwamba hata hivyo Timu ya Kanye haikushangazwa na uamuzi huo kutokana na Msanii huyo mwenye msimamo mkali na vituko kugonga vichwa vya habari kwa matukio yake ya hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii ambayo yalisababisha hadi Instagram kuifungia kwa muda accoun yake ikidai amekiuka sera za Mtandao huo kuhusu matamshi ya chuki, uonevu na unyanyasaji.

Kanye ana shutuma za kutumia Instagram yake kuwapiga picha Watu kadhaa maarufu akiwemo Mke wake waliyeachana Kim Kardashian na mpenzi wake mpya Pete Davidson na pia alitumia Instagram yake kumkashifu Trevor Noah kwa kuzungumzia matukio ya Ye kwenye The Daily Show.
Screenshot_20220321-040128_Instagram.jpg
 
Orodha ya Nchi 20 duniani zilizotajwa kuwa zenye furaha zaidi kwa mwaka 2022 ambapo Finland ameshika namba 1 kwa mwaka wa tano mfululizo.

20. Ufaransa
19. Belgium
18. Czech Republic
17. United Kingdom
16. United States
15. Canada
14. Germany
13. Ireland
12. Australia
11. Austria
10. New Zealand
9. Israel
8. Norway
7. Sweden
6. Luxembourg
5. Uholanzi
4. Switzerland
3. Iceland
2. Denmark
1. Finland
Screenshot_20220321-040306_Instagram.jpg
 
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kifo cha Spika wa Bunge la Uganda, Jacob Oulanyah leo Jumapili "Alikuwa Kada mzuri nimechelewa kutoa taarifa ili Watoto wake wajulishwe kwanza"

Kilichosababisha kifo cha Oulanyah hakijabainishwa lakini alikuwa amelazwa Hospitali nchini Marekani kwa zaidi ya mwezi mmoja na ilizua mjadala kwa Waganda ambao walidai iligharimu pesa nyingi sana za walipa kodi kumtibu.

Oulanyah alichukua kiti cha Spika wa Bunge la Uganda mnamo Mei 2021 na kabla ya hapo alikuwa Naibu Spika kuanzia 2011.
Screenshot_20220321-040419_Instagram.jpg
 
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema imewaua makumi ya Mamluki (Maaskari waliokodiwa ambao hawako kwenye Jeshi la Ukraine) katika shambulio la kombora dhidi ya kituo cha mafunzo magharibi mwa Ukraine.

Msemaji wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Igor Konashenkov,amesema zaidi ya Wanajeshi 100 wa Ukraine na Mamluki wa kigeni wameuawa baada ya kombara la hali ya juu kulipua kambi karibu na Ovruch mjini Zhytomyr Oblast.

"Makombora yetu yamelipua kambi ya vikosi maalumu vya Jeshi la Ukraine ambako Mamluki wa kigeni waliowasili Ukraine wanaishi"
Screenshot_20220321-040614_Instagram.jpg
 
Baraza la Jiji la Mariupol nchini Ukraine limesema vikosi vya Urusi vimeshambulia kwa mabomu Shule ambayo Watu 400 walikuwa wamehifadhiwa "Jengo limeharibiwa na Watu wakiwemo Wazee, Watoto na Wanawake wako chini ya vifusi, bado hakuna taarifa kuhusu majeruhi"
Screenshot_20220321-040748_Instagram.jpg
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mwantum Mgonja ametoa maagizo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo na Wataalamu wake kuchukua hatua mara moja ya kuyafunga maduka yote ya dawa yaliyokaguliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) na kukosa vigezo huku akiwataka wamiliki wote kufuata sheria za Nchi.

Mwantum Mgonja ameyasema hayo wakati wa kikao cha Kamati ya Chakula na Dawa (CFDC) ya Halmashauri hiyo ya Mkuranga na Wawakilishi wa TMDA.

Katika kikao hicho alipokea ripoti ya ukaguzi uliofanywa na TMDA kwenye maduka ya dawa za binadamu na mifugo, ukaguzi uliofanyika Machi 14-18 mwaka huu na kukuta mapungufu mbalimbali ikiwemo kukutwa na dawa zilizokwisha muda wake, huku mengine kutokuwa na watoa dawa waliopata mafunzo.

"Nakuagiza Mganga Mkuu kuhakikisha ndani ya Halmashauri hii ya Mkuranga, maduka yote ambayo hayana vibali na hayataki kufuata taratibu yafungiwe haraka sana kuanzia sasa napotoa taarifa hii lakini kingine nimezuia maduka ya dawa ambayo yanauza yakiwa hayana Wataalamu, tunawaita 'Famasia', Mtu anafungua duka lake la dawa lakini anaenda kuuza dawa kienyeji, yale maisha ni maisha hatarishi, tunahatarisha wananchi wa Wilaya hii ya Mkuranga lakini pia tunahatarisha maisha yetu sisi binafsi ambao ni wakazi wa hapa Mkuranga"
Screenshot_20220321-040858_Instagram.jpg
 
Kikundi maalumu cha ulengaji shabaha nchini Ukraine kimeendelea na zoezi la kuwafundisha Raia matumizi sahihi ya silaha.

Hatua hii inakuja baada ya Rais wa Ukraine kuwapa ruhusa ya kupewa silaha Raia wote walio tayari kuungana na Wanajeshi kuitetea Nchi yao dhidi ya uvamizi wa kijeshi wa Urusi.
Screenshot_20220321-041416_Instagram.jpg
 
Korea Kaskazini imefanya jaribio jingine la makombora manne leo Jumapili, Wanajeshi wa Korea Kusini wamesema makombora hayo yamerushwa kutoka kwenye roketi tatu tofauti na kuelekezwa Baharini, Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilirusha kombora jingine ambalo hata hivyo lilifeli.
Screenshot_20220321-041525_Instagram.jpg
 
Kirusi kingine kipya cha corona kimeibuka katika nchi za China, Japan na Korea.

China kwa sasa inapambana na visa vya Uviko-19 zaidi ya mara mbili katika milipuko inayokua kwa kasi, katika mkakati wa nchi hiyo kutokomeza ugonjwa huo.

Machi 15 nchi hiyo imeripoti zaidi ya wagonjwa wapya 5,000 waliothibitishwa kupata Uviko-19, zaidi ya mara mbili ya idadi iliyoripotiwa Jumatatu Machi 14 na hesabu kubwa zaidi ya kila siku tangu janga hilo lianze zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Kutokana na hali hiyo, Waziri wa Afya nchini Ummy Mwalimu amewataka wananchi waendelea kujitokeza kupata chanjo kwa kuwa haina madhara kama baadhi ya watu wanavyosema.

Pia amesema aina mpya ya kirusi kipya kilichoibuka nchini China, Japan pamoja na Korea ni tahadhari hivyo amewataka wananchi kuendelea kuwa makini huku akisisitiza wajitokeze kupata chanjo.

"Kwa sasa kitu ambacho kinaweza kutusaidia kujikinga na Uviko-19 ni chanjo kwa kuwa ni salama sana, nawaomba wote ambao hamjapata mkapate chanjo ili tuweze kujikinga," Amesema Waziri Ummy.
Screenshot_20220321-041757_Instagram.jpg
 
Mkazi wa kitongoji Kijiji cha Sibwesa wilayani Tanganyika, Mande Emanuel (30) amejinyonga baada ya kumjeruhi mumewe, Dotto Enos (35) kwa kumkata mapanga.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Machi 20, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia uliosababishwa na shughuli za kilimo.
Screenshot_20220321-041912_Instagram.jpg
 
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amevisimamisha vyama vya kisiasa nchini humo vinavyounga mkono Russia, akisema “shughuli za wanasiasa zinazolenga mifarakano na ushirikiano hazitafaulu”.
Screenshot_20220321-042023_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom