Makapuku Forum

Makapuku Forum

m sio mwandikaji mzuri btw natamani ujue kilichotokea after pale nlinunua karanga nkawa na uza na ndo ukawa mwanzo wa kukutana na watu mbali mbali nkapata wazo la kwenda veta kupitia nlijibana bana nkapata kama 160k nkaja veta na hayo mambo mengne nkamuachia mungu sahv nasubr matokeo mwezi wa 6 inshaalah naenda kumaliza mwaka wa 3 pamoja na kua sina ada naamin kama iliwezekana kujisomesha miaka miwili kwa vibarua vya kulima na kupalilia na saiv ntaweza pia japo kwa sasa hv nna changamoto ya mkono btw naamini everything will be ok yote kwa yote nashkuru pengne 6k uliona ni ndogo btw kwangu ilifumbua macho mungu akujaalie maisha marefu
Jamani nimekumbuka sasa Mungu azidi kukubariki sana sana na ikitokea umekwama usisite kunitafuta mkuu tupo pamoja nakumbuka kuna watu walikuwa wanakuita tapeli nimekumbuka vizuri sana
 
Meli nne kubwa za kivita za Urusi zimeonekana zikisafiri karibu na visiwa vya Japan vya Honshu na Hokkaido zikielekea Ulaya ambapo inahisiwa kuwa huenda zinaenda kuongeza nguvu ya kijeshi nchini Ukraine.

Picha zilizotolewa na Wizara ya ulinzi ya Japan zimeonesha kinachoaminika kuwa malori ya kijeshi ndani ya meli hizo ambapo Msemaji wa Wizara ya ulinzi ya Japan amesema kuna uwezekano meli hizo zinakwenda nchini Ukraine.

Wachambuzi wa masuala ya kivita wanasema hadi sasa oparesheni ya kijeshi ya Urusi haijaenda kama ilivyopangwa na tayari vifaa vingi vya kijeshi vikiharibiwa kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyotarajiwa, lilikua ni lengo la Russia kuifikia Ikulu ya Ukraine ndani ya siku mbili tu za vita lakini hilo halijawezekana hadi sasa vita ikiwa na zaidi ya wiki mbili.
Screenshot_20220317-150358_Instagram.jpg
 
m sio mwandikaji mzuri btw natamani ujue kilichotokea after pale nlinunua karanga nkawa na uza na ndo ukawa mwanzo wa kukutana na watu mbali mbali nkapata wazo la kwenda veta kupitia nlijibana bana nkapata kama 160k nkaja veta na hayo mambo mengne nkamuachia mungu sahv nasubr matokeo mwezi wa 6 inshaalah naenda kumaliza mwaka wa 3 pamoja na kua sina ada naamin kama iliwezekana kujisomesha miaka miwili kwa vibarua vya kulima na kupalilia na saiv ntaweza pia japo kwa sasa hv nna changamoto ya mkono btw naamini everything will be ok yote kwa yote nashkuru pengne 6k uliona ni ndogo btw kwangu ilifumbua macho mungu akujaalie maisha marefu
Mkono ulifanyaje tena pole sana sana Mungu azidi kukuponya urudi kama zamani
 
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kupitia hotuba yake usiku wa kuamkia leo amesema hasara waliopata Wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine ni kubwa kuliko katika vita vya Syria, Chechnya na Afghanistan.

"Wanajeshi wa Urusi wamepata hasara kubwa Ukraine, tukio ambalo halikufanyika nchini Syria wala Chechnya, vilevile Wanajeshi wa Soviet hawakupata hasara kama hiyo nchini Afghanistan"

Idara ya kijasusi ya Marekani inakadiria kuwa zaidi ya Wanajeshi 7,000 wa Urusi wamekufa wakati wa uvamizi wa Ukraine ambao una zaidi ya wiki mbili sasa.
Screenshot_20220317-150838_Instagram.jpg
 
"Nawashukuru Wageni wote mliokubali wito wetu karibuni sana, leo March 17 umetimia mwaka mmoja tangu alipotutoka Mpendwa wetu Dr.Magufuli, sisi Wanafamilia tumeiandaa siku ya leo maalum kwa ajili ya misa takatifu ya kumuombea na kuenzi maisha yake"

"Ni imani yangu katika Dini zote tumefundishwa kushukuru kwa kila jambo naomba muungane nami katika kumshukuru Mungu, tunamshukuru Mungu kwa Neema zake kwani ilimpendeza kujifunza mema mengi kutoa kwa Hayati Magufuli hakika tutayaishi na kuyaenzi daima"

"Sisi Wanafamilia inatuwia vigumu kumtaja kila mmoja aliyekuwa nasi tangu msiba wa Hayati Magufuli, tunakushukuru Rais Samia kwa kuwa nasi kwa ukaribu sanasana wakati wote tulipoondokewa na Baba yetu"

"Rais Samia naomba nikiri kukupigia simu lakini kwa bahati mbaya sikufanikiwa ila baadaye ukanipigia nikakupa mwaliko huu ambao uliupokea kwa moyo mkunjufu na ukaahidi kuja ingawa haikuwa kimaandishi nashukuru mno, asante sana kwa kuja licha ya kuwa una majukumu mengi ya Kitaifa na Kimataifa umeniheshimu sana Mama tunakuombea Mungu akupe nguvu ya kuendelea kuongoza Taifa vema na Mungu azidi kukulinda akupe maisha marefu” ——— asema Mama Janeth Magufuli leo Chato Geita.
Screenshot_20220317-151037_Instagram.jpg
 
"Mzee Magufuli alipinga rushwa na kusisitiza uchapakazi, Magufuli alitamani kuiona Tanzania iliyojikomboa kiuchumi nikasema nitaiongoza Tanzania katika mwelekeo huo, nitayaendeleza yote aliyotuachia Magufuli"

"Baadhi ya miradi aliyotuachia imekamilika, hivi karibu tutazindua Daraja la Tanzanite pale DSM ambalo ilikuwa ni ndoto ya Hayati Magufuli kuona Daraja lile linakamilika"

"Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Chato kimefikia 95% na Stendi ya Chato imefikia 90% nataka niwaahidi Wana Chato miradi hii ikikamilika nitakuja mwenyewe kuifungua kama ambavyo Hayati magufuli angekuja kufungua kama angekuwepo" ——— asema Rais Samia akiwa Chato leo kwenye mwaka mmoja wa kifo cha Hayati Dr. Magufuli.
Screenshot_20220317-151418_Instagram.jpg
 
Ni Waingereza watupu, au
Wahispnia robo fainali Uefa

Ratiba ya mechi za robo fainali za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya inapangwa kesho (Ijumaa) asubuhi wakati timu nane zitakapofahamu zinapitia njia gani kufika Paris kucheza fainali iliyohamishwa kutoka jiji la Petersburg baada ya Russia kuivamia Ukraine.

Hakuna kanuni inayozuia timu moja kucheza na nyingine na hivyo kuna uwezekano wa kuwa na mechi ya robo fainali inayokutanisha timu tupu za England; Chelsea, Liverpool na Manchester City.

Hali kama hiyo inaweza pia kutokea kwa timu za Hispania ambako Villarreal, Real Madrid na Atletico Madrid zimefika robo fainali.

Timu nyingine ni Bayern Munich ya Ujerumani na Benfica ya Ureno. Villarreal, Atletico Madrid na Manchester City hazijawahi kutwaa ubingwa huo.

Bayern Munich na Liverpool zitakuwa zikiwania kuifikia AC Milan katika nafasi ya pili ya kutwaa ubingwa mara nyingi baada ya timu hiyo ya Italia kutwaa mara saba, wakati wababe Real Madrid wanaweza kudurufisha kiwango cha wapinzani wao kwa kutwaa kombe hilo mara 14.

Unadhani timu gani zitakutana robo fainali kabla ya ratiba kupangwa kesho?
Screenshot_20220317-151819_Instagram.jpg
 
Mkono ulifanyaje tena pole sana sana Mungu azidi kukuponya urudi kama zamani
kuna sehemu nlipata kibarua cha kubeba zege bahati mbaya nliteleza kwenye ngazi mkono ukateguka inshaalah ntakua sawa japo ndo mambo yamesimama kdg c unajua ofisi ni miili yetu wenyew ila ntakua sawa inshaalah kuna dawa za kienyej natumia
 
kuna sehemu nlipata kibarua cha kubeba zege bahati mbaya nliteleza kwenye ngazi mkono ukateguka inshaalah ntakua sawa japo ndo mambo yamesimama kdg c unajua ofisi ni miili yetu wenyew ila ntakua sawa inshaalah kuna dawa za kienyej natumia
Pole sana Mungu azidi kukuponya tupo pamoja usijali ukikwama nitafute tu
 
Mshambuliaji wa Azam, Prince Dube hapo jana alifanikiwa pia kupata bao lake la kwanza kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu huu baada ya timu yake kuilaza Namungo mabao 2-1.
Screenshot_20220317-152013_Instagram.jpg
 
UONGOZI wa klabu ya Yanga umefichua sababu za kuwasajili wachezaji kwa mikataba mifupi ni kutokana na mifumo ya soka hapa nchini ilivyo.

Mwenyekiti kamati ya usajili ya Yanga, Hersi Said alisema moja ya sababu kubwa ni aina ya skauti inayofanyika kuwapata wachezaji hao na asilimia kubwa wanasajiliwa bila kuwafahamu kiundani tangu akiwa chipukizi zaidi ya kuwaona wiki kadhaa tu.

“Ni ngumu sana kumfanyia skauti mchezaji hapa nchini kuanzia alipoanza mpaka ukubwani kutokana na aina ya mifumo ya upatikanaji wao ilivyokuwa, sasa kama shida iko hapo unawezaje kumsajili mchezaji kwa mkataba wa muda mrefu halafu akiharibu gharama tu za kuvunja nae mkataba sio mchezo, itakulazimu kumtumia hivyo hivyo hata kama kiwango kimeshuka,” alisema Hersi.
Screenshot_20220317-152331_Instagram.jpg
 
SIMBA YATOA WAWILI KIKOSI BORA CHA WIKI CAF
.
Hiki Hapa Kikosi Bora cha wiki Kombe la Shirikisho Afrika:
.
1. Zakaria Saidi (JS Soura)
2. Karim El Eraki (Al Masry)
3. Mohammed Hussein (Simba SC)
4. Kevin Mondeko (TP Mazembe)
5. Joash Onyango (Simba)
6. Ghazi Ayadi (JS Soura)
7. Hassan Ali (Al Masry)
8. Felix Oukine (Coton Sport)
9. Karim Konate (Asec Mimosas)
10. Mohammed El Fakih (Al Ahli Tripoli)
11. Kabelo Dlamin (Orlando Pirates)

Screenshot_20220317-152718_Instagram.jpg
 
Wakala: Saido ana ofa kibao nje
.
Wakala wa winga wa Yanga, Said Ntibazonkiza amesema sio klabu ya Renaissance Sportive Berkane ya nchini Morocco ambayo imeonyesha nia ya kutaka huduma ya mteja wake, lakini ana ofa nyingine nyingi.
.
"Bado sijakaa na Yanga kuzungumza nao kama tunaendelea nao au la, ila tayari tuna ofa nyingi kutoka nje ya nchi, hivyo baada ya kumalizana na Yanga nitajua wapi mteja wangu anaelekea.”
Screenshot_20220317-152939_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom