Ndani ya hii Range Rover ambayo usukani wake upo upande wa kushoto mwa gari anaonekana Rais wa Rwanda Paul Kagame akimuendesha Rais wa Tanzania Samia Suluhu kumpeleka Uwanja wa Ndege wakati Rais Samia akirudi Tanzania baada ya ziara ya siku mbili Nchini humo.
Sio kwamba Dereva hakuwepo au aliumwa bali ni Rais Kagame kuendeleza ukarimu wake na heshima kubwa aliyompa Rais Samia baada ya ziara hiyo ambayo pamoja na mengine imepigilia msumari wa udugu na ushirikiano wa Nchi hizi mbili.
Kuhusu walichozungumza, Rais Samia alisema ———> “"Mazungumzo yalijikita kwenye kuimarisha, kukuza ushirikiano wa kiuchumi, pia siasa ya ukanda huu wa Afrika Mashariki, kubwa tulilokubaliana ni kukuza zaidi ushirikiano kwani Tanzania na Rwanda tupo kwenye biashara na uwekezaji na uhusiano mzuri tulionao bado kuna fursa nyingi tunazoweza kuzitumia ili kukuza biashara na uwekezaji kwa faida ya pande zote mbili"
"Pia tulizungumzia ushirikiano kwenye mambo ya TEHAMA kama mnavyojua Tanzania tuna mkongo ambao tumeusambaza katika Nchi jirani na Rwanda wanatumia na leo tumesaini hapa makubaliano kwamba tunaendelea kuweka uhusiano mzuri mkubwa kwenye matumizi ya TEHAMA na niwapongeze Rwanda mpo mbele yetu na sisi tuko tayari kuja kujifunza kwenu"
"Tulizungumzia pia COVID 19 na tumeweka mikakati ya kushirikiana kupitia kituo chetu cha Rusumo mpakani, tumekubaliana kuendeleza ushirikiano uliopo ambao ni wa kidugu na kihistoria" ——— Rais Samia Suluhu.
View attachment 1879545