Makapuku Forum

Makapuku Forum

Simba Mangu(Caracal), huyu ndiye mwenye kasi kuliko paka pori wengine wadogo wa Afrika na mwili wake ni mkubwa kidogo ukilinganisha na paka wengine wadogo wa porini.

Wao hula chochote watakachokipata ili mradi ni nyama, kuanzia ndege, nyani wadogo, panya, nguchiro na hata pimbi.

Jike huonesha utayari wa kujamiiana ili kupata Watoto kwa kusambaza mkojo wake, kisha Madume watagombana kuipata nafasi ya kujamiiana na Jike.

Majike hukaa na mimba kwa miezi mpaka 2.5.Kisha hutunza Watoto bila Dume na huwanyonyesha kwa miezi 4-6 ingawa wana uwezo wa kula nyama wakiwa na mwezi na kawaida Watoto huondoka wakifikisha miezi tisa au kumi na Madume huenda mbali zaidi kuliko Majike.
Screenshot_20210803-183623_GBInsta.jpg
Screenshot_20210803-183643_GBInsta.jpg
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovick Utouh, amesema anaunga mkono hoja ya Mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa na Hussein Bashe, kuhusu wabunge kukatwa kodi.
:
Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga, alisema miongoni mwa misingi mikubwa ya kodi ni usawa kwa kuwa kodi yoyote haitakiwi kuwa na matabaka ya watu.
:
“Tunalipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi sasa hawa wabunge si wana kipato, wanapokea mshahara kwanini wasilipe kodi, mantiki ya hiyo haipo,” alihoji Utouh.
:
Julai 23, Mbunge wa Ukonga, Slaa, akihutubia wananchi katika jimbo hilo, alisema imefika hatua wabunge waanze kulipa kodi kupitia mishahara yao ili wapate uwezo wa kuwaambia wananchi na wao walipe kodi.
Screenshot_20210803-184328_GBInsta.jpg
 
Bunge lisilaumiwe kuhusu tozo - Lusinde
-
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (MNEC) na Mbunge wa Mvumi mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde amefunguka kuhusu makato ya miamala katika simu za mikononi ambapo amedai Bunge wao walipitisha sheria na kiwango kilipagwa na Waziri wa Fedha na Mipango,(Dk. Mwigulu Nchemba) hivyo Bunge lisilaumiwe.

Amesema mjadala kwa sasa uwe tozo ni kubwa hivyo waziri apunguze sio lilaumiwe bunge kwa kupitisha sheria hiyo kwani hata mwanzo makato yalikuwepo na watu walikuwa wanalipa.

Pia amedai Wabunge wanakatwa kodi ambazo zinaenda kwenye shughuli za maendeleo hivyo jamii ipuuze maneno kwamba wao hawakatwi kodi.

Hatua hiyo, imekuja mara baada ya hivi karibuni Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa akiwa katika mkutano wa hadhara uliowashirikisha Wananchi wa Mzinga Ukonga Jijini Dar es Salaam kudai wabunge waanze kulipa kodi kupitia mishahara yao ili wapate uwezo wa kuwaambia Wananchi na wao walipe kodi.

Pia hivi karibuni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovick Utouh alisema wabunge hao wanatakiwa kukatwa kodi katika mishahara yao.

Akizungumza leo Agosti 3, na Waandishi wa Habari, Lusinde amesema bunge wametunga sheria na wala sio kiwango kwani hilo ni jukumu la Waziri wa Fedha na Mipango.

“Sisi tumetunga sheria sio kiwango, mbona hata mwanzo makato yalikuwa kwenye simu, kiwango anapanga Waziri na wanatengeneza kanuni ninauhakika makato yatapungua ndugu zangu tujifundishe kulipa kodi nani wa kutupa hela za bure?Mjadala uwe hapo tozo ni kubwa hivyo Waziri apunguze sio lilaumiwe Bunge,” amesema Lusinde.

Kuhusiana na mishahara yao kukatwa kodi, Lusinde amesema wao wanakatwa kodi ambazo zinaenda kwenye shughuli za kimaendeleo hivyo jamii iondokane na maneno kwamba wao hawakatwi kodi.
Screenshot_20210803-184458_GBInsta.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda wakitembelea katika kiwanda cha Inyange Plant Entrance mjini Kigali kinachozalisha Juisi, Maziwa na Maji ya kunywa leo tarehe 03 Agosti, 2021
Screenshot_20210803-184634_GBInsta.jpg
 
I Mwalimu wa shule ya msingi Radienya, Wilfred Nyaroko Oliech, mkazi wa Mtaa wa Obwere wilayani Rorya mkoani Mara, amefikishwa mahakamani kwa makosa mawili ikiwemo kubaka na kusambaza maambukizi ya Virui vya Ukimwi kwa binti mwenye umri wa miaka 15 jina limehifadhiwa.
Screenshot_20210803-184733_GBInsta.jpg
 
MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Brigadia Jenerali Marco Gaguti leo amezindua chanjo ya UVIKO-19 huku akiwata wananchi wa Mtwara kuendelea kuzingatia taratitibu zote za kujikinga na ugonjwa huo wa korona kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya.

Gaguti amemshukuru Raisi Samia Suluhu kwa hatua ya kuruhusu Tanzania kuwa miongoni mwa nchi ambazo zimepata chanjo ya UVIKO-19 na leo tarehe Agosti 3, 2021 imezinduliwa kwa Mkoa wa Mtwara, mkoa ambao uko pia jirani na nchi ya Msumbiji.

Amesema kwa awamu ya kwanza, Mkoa wa Mtwara umepata chanjo dozi elfu 20 ambapo amesema chanjo hizo zitaanza kutolewa kwa wahudumu wa afya, watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka 50 na watu wenye changamoto ya maradhi kuanzia miaka 18 na kuendelea.
Screenshot_20210803-185022_GBInsta.jpg
Screenshot_20210803-185041_GBInsta.jpg
 
UKISHAPATA CHANJO YA COVID19 USITUMIE KILEVI CHOCHOTE KWA SAA 72
-
Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti kutoka NIMR, Dkt. Paul Kazyoba anasema kilevi cha aina yoyote hakitakiwi baada ya kuchanjwa kwani kitaingilia Mfumo wa Uzalishaji wa Kinga za Mwili ambao unafanywa na Chanjo
-
Chanjo inapochomwa katika Mwili wa Binadamu, ikiingia huenda kusisimua Seli za Kinga (Antibodies) kuzalishwa na zikishajaa Mwilini huwa Askari wa kupambana na kirusi kitakachoingia
-
Ili kuufanya Mwili uzalishe Seli kinga nyingi inatakiwa usiingiliwe na kitu chochote cha tofauti kwenye Damu kwa saa 72 (Siku 3). Kilevi cha aina yoyote kitavuruga mfumo na kuifanya chanjo isifanye kazi yake vizuri
Screenshot_20210803-185655_GBInsta.jpg
 
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi-Taifa, James Francis Mbatia hii leo August 03, 2021 amechomwa chanjo ya Covid-19, katika Hospital ya Agha Khan Jijini Dar es Salaam.

Mbatia ameongozana na Mke wake Catharina James Mbatia, Katibu Mkuu wa NCCR Taifa, Martha Chiomba pamoja na Naibu katibu Mkuu - Bara wa Chama hicho Anthony Calist Komu.
Screenshot_20210803-190021_GBInsta.jpg
 
Hizi ni picha za Wakuu wengine wa Mikoa miwili ya Arusha, John Mongela na Morogoro, Martin Shigela ambao wameongoza pia Wananchi kwenye Mikoa yao leo katika zoezi la kupata chanjo ya Covid 19.
Screenshot_20210803-190151_GBInsta.jpg
Screenshot_20210803-190209_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom