Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210804-083117_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20210804-083136_Opera%20Mini.jpg
 
MANARA PRESS CONFERENCE| SERENA, DSM

"Wakati naingia Simba sikuwa nalipwa bali niliombwa nijitolee tu, nami nilifanya kazi ya kujitolea, Viongozi wanajua hatukuwa na pesa nikawa napigia mpaka Rafiki zangu wanisaidie kwa ajili ya Simba, kutupa maji na hata sehemu za malazi yenye hadhi ya Simba" Haji Manara
Screenshot_20210804-125956_GBInsta.jpg
 
MANARA PRESS CONFERENCE| SERENA, DSM

"Kaka yangu Juma Nkamia analalamika sikuwa napokea simu yake, napokeaje simu wakati yeye ni Mgombea na kipindi kilikuwa cha uchaguzi, mimi ni muajiriwa wa Simba, iliwezekana vipi kuvunja utaratibu?"

"Kaka yangu Nkamia anisamehe tu, nilikuwa kwenye utaratibu wa kazi, mimi ni muumini wa utaratibu"

Haji Manara, anazungumza
Screenshot_20210804-130244_GBInsta.jpg
 
MANARA PRESS CONFERENCE| SERENA, DSM

"Nilienda Lesotho kwa gharama zangu binafsi, hawajawahi kuniandika kwenye safari ila nilikuwa natumia gharama zangu, kuniandika mimi wanasema ni matumizi yasiyo na lazima, kila kitu nilifanya kwa posho yangu mpaka mafuta tu ya kufanya media tour sikuwa napewa"

Manara, anazungumza hapa Serena

Screenshot_20210804-130405_GBInsta.jpg
 
MANARA PRESS CONFERENCE| SERENA, DSM

"Wakati Senzo anakuja kwa mara ya kwanza, alinifuata na kuniambia amepewa kazi ya kunifukuza Mimi kazi, lakini Senzo alihoji kwanini nimfukuze bila sababu?"

"Kifupi walimleta ili atekeleze matakwa ya wakubwa ila Senzo alisimama imara sana, alipinga kufanya kitu bila kukichunguza ndicho kilichomuondoa Simba"
Screenshot_20210804-130513_GBInsta.jpg
 
MANARA PRESS CONFERENCE| SERENA, DSM

"Kila anaeondoka Simba tu basi sababu ni kuhujumu, wameondoka zaidi ya watu 12 kwa kosa moja, mara Mbaga, mara Senzo na sasa Haji kaondoka, haya yote yapo chini ya Barbra ndie muhusika wa yote" Haji Manara

Screenshot_20210804-125833_GBInsta.jpg
 
MANARA PRESS CONFERENCE| SERENA, DSM

"Barbra huyu anasema Kashembe anahujumu Simba? Kashembe huyu aliehusika kwenye transformation? Kifupi watu wote muhimu walioapambana transformation ipite leo hii wanaonekana hawana maana, Barbra huyo" Haji Manara

Screenshot_20210804-125956_GBInsta.jpg
 
Aliyekuwa Afisa Habari wa Simbasc Tanzania, Haji Manara leo kwenye mkutano wake na Waandishi wa habari.

"Sijawahi kugombana na mwandishi yeyote kwa sababu ya masuala yangu binafsi, yote hii ilikuwa ni kwasababu ya Simba Sc, ni katika kutetea kiongozi au mchezaji pamoja na brand ya Simba, mimi sio mkamilifu katika kufanya kazi lazima kuna kukosea"

"Nawashukuru sana Yanga Sc wenyewe wanajiita Dar Es Salaam Young Africans hasa katika kipindi hiki cha usajili, yawezekana utani ulizidi ila lengo langu lilikuwa ni kudumisha utani wa jadi, pale nilipokosea wanisamehe na najua niliwakosea"

"Wanasema hakuna mtu mkubwa kuliko Simba Sc, hapana hiyo ni haramu, kwani kuna mahali niliwahi kusema Haji ni Mkubwa? nimefanya makubwa sana katika kuhamasisha timu, mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni"

"Mkiniona mikoani mjue najitegemea, Msemaji anayepiga promo kubwa na anaisemea timu, nauli anajitegemea, kula anajitegemea, hoteli anajitegemea hadi safari za nje anajitegemea, kila wakisafiri naambiwa jina lako halipo" ameeleza Haji Manara
Screenshot_20210804-130154_GBInsta.jpg
 
Aliyekuwa Afisa Habari wa Simbasc tanzania amesema kuwa Moo dewji alimpigia simu na kumwambia kuwa anataka kumtoa Simba kwa sababu amemzidi umaarufu.

"Mo Dewji anasema hapati faida, lakini mkiangalia jezi ya Simba ina matangazo mpaka ya Mo Foundation. Jezi imechafuka matangazo ya Mo kama timu za Sudan halafu mtu anasema hapati Faida ?." Haji Manara

Screenshot_20210804-130244_GBInsta.jpg
 
“Kwenye hili la kudukuliwa simu yangu naomba serikali inilinde, ni nani amempa mamlaka Mohammed Dewji ya kudukua simu yangu, ubaya sio mimi tuu niliyedukuliwa niliona majina ya wanasimba wengi wanaodukuliwa.

“Waliniita ofisini nikaenda wakaniambia jana ulionekana umeenda kigamboni Kwa Ghalibu kutuhujumu, walinionyesha simu inayoonyesha kuwa nilikuwa Kigamboni lakini nilipoangalia tarehe ilinionyesha ilikuwa tarehe 7 muone jinsi hawa watu walivyokuwa wananichukia,” haji Manara

Screenshot_20210804-125833_GBInsta.jpg
 
Ndani ya hii Range Rover ambayo usukani wake upo upande wa kushoto mwa gari anaonekana Rais wa Rwanda Paul Kagame akimuendesha Rais wa Tanzania Samia Suluhu kumpeleka Uwanja wa Ndege wakati Rais Samia akirudi Tanzania baada ya ziara ya siku mbili Nchini humo.

Sio kwamba Dereva hakuwepo au aliumwa bali ni Rais Kagame kuendeleza ukarimu wake na heshima kubwa aliyompa Rais Samia baada ya ziara hiyo ambayo pamoja na mengine imepigilia msumari wa udugu na ushirikiano wa Nchi hizi mbili.

Kuhusu walichozungumza, Rais Samia alisema ———> “"Mazungumzo yalijikita kwenye kuimarisha, kukuza ushirikiano wa kiuchumi, pia siasa ya ukanda huu wa Afrika Mashariki, kubwa tulilokubaliana ni kukuza zaidi ushirikiano kwani Tanzania na Rwanda tupo kwenye biashara na uwekezaji na uhusiano mzuri tulionao bado kuna fursa nyingi tunazoweza kuzitumia ili kukuza biashara na uwekezaji kwa faida ya pande zote mbili"

"Pia tulizungumzia ushirikiano kwenye mambo ya TEHAMA kama mnavyojua Tanzania tuna mkongo ambao tumeusambaza katika Nchi jirani na Rwanda wanatumia na leo tumesaini hapa makubaliano kwamba tunaendelea kuweka uhusiano mzuri mkubwa kwenye matumizi ya TEHAMA na niwapongeze Rwanda mpo mbele yetu na sisi tuko tayari kuja kujifunza kwenu"

"Tulizungumzia pia COVID 19 na tumeweka mikakati ya kushirikiana kupitia kituo chetu cha Rusumo mpakani, tumekubaliana kuendeleza ushirikiano uliopo ambao ni wa kidugu na kihistoria" ——— Rais Samia Suluhu.
Screenshot_20210804-134606_GBInsta.jpg
 
Klabu ya Al Ahly imefikia makubaliano na Simba SC juu uhamisho wa winga Luis Jose Miquissone.

Uhamisho Miquissone 26 raia wa Msumbiji utaigharimu Miamba hiyo ya Afrika ada ya uhamisho ya US$900,000 sawa na Shillingi bilioni 2.1 na atasaini mkataba wa miaka minne.
Screenshot_20210804-140913_GBInsta.jpg
 
Haji anasema mkataba ambao Hans Pope aliuzungumzia wa milioni nne ulikuja baada ya Mo Dewji kuomba Haji ampelekee mkataba wake wa kibiashara na kampuni ya Azam na hapo akiwa tayari ameitumikia klabu kwa miaka sita bila kuwa na mkataba.

Kwenye mkataba huo wa Azam ambao aliupeleka ulikuwa na kipengere kinachotaka kiasi cha shilingi milioni mia tatu hamsini kulipwa ili mkataba uvunjwe, Haji anasema sharti hilo ndilo lililopelekea Simba Sc kumuandalia mkataba ambao haukufikia kiasi cha shilingi milioni nne ukiwa na sharti la kutomtaka kufanya biashara na kampuni nyingine yoyote sipokuwa Mohamed Eterprises.
Screenshot_20210804-125956_GBInsta.jpg
 
"Pale ambapo niliteleza kama binadamu 'am sorry' sijakamilika, Sijawahi kuwa mkamilifu".- Haji Manara

Haji anasema katika kipindi cha miaka sita amezungumza na wanahabari mara nyingi zaidi hivyo kama binadamu wapo aliokwaza kwa namna moja ama nyingine kwenye utendaji.
Screenshot_20210804-142326_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom