Makapuku Forum

Makapuku Forum

Shunie ina maana wewe hupendi kupashughulisha hapo kati mzee mwenzangu?

Mimi niwe mkweli, pamoja na kuzeeka kwangu lakini kati muhimu sana hata pawe panaguswa guswa mipapaso tu Kuna Raha yake, tena ukute ngozi nyororo laini mikono imeumbika kama ya chibonge mwepesi cheusi mangala mtoto mlito a.k.a shangazi Shunie Shunie awwwwwww Mimi ni nani hata nisipagawishwe akii!!???
Hahahhahha mzee huna akili wewe
 
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 57 mkazi wa Kata ya Puge Wilaya ya Nzega mkoani Tabora ameuawa na Mumewe kwa kushirikiana na Mwanae na kisha kuning'inizwa kwenye kamba ili aonekane amejinyonga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Safia Jongo amesema tukio hilo limetokea August 03, 2021 katika Kijiji cha Isalalo ambapo Baba na Mtoto wake walimuua Mwanamke huyo na kutengeneza tukio la kujinyonga.

RPC amesema sababu iliyopelekea mauaji hayo ni Wanafamilia hao kuchoka kumuuguza Mama huyo na kukosekana kwa pesa ya matibabu, Watuhumiwa wanashikiliwa na baada ya mahojiano wamekiri kuhusika na tukio hilo.
Screenshot_20210805-145413_GBInsta.jpg
 
Kesi ya Mbowe inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba leo lakini hata hivyo Mbowe hajafikishwa Mahakamani bali kesi yake inaendeshwa kwa njia ya mtandao.

Mbowe ameshitakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu July 26, 2021 kwa mashtaka mawili ikiwemo la tuhuma za Ugaidi.
Screenshot_20210805-145848_GBInsta.jpg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kuendelea kusikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kutokana na hitilafu ya mtandao.

Kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ilipangwa kuendeshwa kwa njia ya mtandao "Video Conference" lakini imeshindikana kutokana na tatizo la kimtandao.

Wakili wa Mbowe, Peter Kibatala amesema kutokana na sababu hizo, Mbowe atafikishwa Mahakamani kesho August 6, 2021 badala ya kesi hiyo kuendeshwa kwa njia ya mtandao.

Mbowe alifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza July 26, 2021 kwa mashtaka mawili ikiwemo la tuhuma za Ugaidi.
Screenshot_20210805-150141_GBInsta.jpg
 
Kutoka Mahakama ya Kisutu leo hizi ni picha za matukio mbalimbali yakiwemo yale ya baadhi ya Wafuasi wa CHADEMA waliofika Mahakama hapa kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, kukamatwa na Askari Polisi baada ya kuinua mabango na kupiga kelele kwamba “Mbowe sio Gaidi”.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kuendelea kusikiliza kesi hiyo ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kutokana na hitilafu ya mtandao.

Kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ilipangwa kuendeshwa kwa njia ya mtandao "Video Conference" lakini imeshindikana kutokana na tatizo la kimtandao, Wakili wa Mbowe, Peter Kibatala amesema kutokana na sababu hizo, Mbowe atafikishwa Mahakamani kesho August 6, 2021 badala ya kesi hiyo kuendeshwa kwa njia ya mtandao.

Mbowe alifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza July 26, 2021 kwa mashtaka mawili ikiwemo la tuhuma za Ugaidi.
Screenshot_20210805-150325_GBInsta.jpg
Screenshot_20210805-150351_GBInsta.jpg
Screenshot_20210805-150408_GBInsta.jpg
Screenshot_20210805-150441_GBInsta.jpg
Screenshot_20210805-150459_GBInsta.jpg
Screenshot_20210805-150522_GBInsta.jpg
Screenshot_20210805-150538_GBInsta.jpg
 
Hahah
Shunie ina maana wewe hupendi kupashughulisha hapo kati mzee mwenzangu?

Mimi niwe mkweli, pamoja na kuzeeka kwangu lakini kati muhimu sana hata pawe panaguswa guswa mipapaso tu Kuna Raha yake, tena ukute ngozi nyororo laini mikono imeumbika kama ya chibonge mwepesi cheusi mangala mtoto mlito a.k.a shangazi Shunie Shunie awwwwwww Mimi ni nani hata nisipagawishwe akii!!???
Hahahaha
 
GREALISH NI SUALA LA MUDA TU ETIHAD
.
Staa Jack Grealish yupo kwenye hatua za mwisho kabisa za kukamilisha uhamisho wake wa rekodi kwenye Ligi Kuu England kwa kujiunga na Manchester City kwa ada ya Pauni milioni 100 (Sh 323 Bilioni)
.
Na kila kitu kinaonekana kuwa kwenye hali nzuri ambapo kwa taarifa za mtaalamu Fabrizio, Grealish atafanyiwa vipimo vya Afya hii leo Alhamisi.
.
Grealish anaenda kuvunja rekodi ya Paul Pogba ya kuwa mchezaji ghali zaidi kwenye Ligi Kuu England, wakati aliponaswa kwa Pauni milioni 89 na Manchester United kutoka Juventus mwaka 2016.
.View attachment 1880467
duh! yaaani thamani ya huyu bwana ni luis jose miquissone 160
 
Klabu ya PSG tayari imeanza mazungumzo na Wawakilishi wa Lionel Messi kuhusu uwezekano wa kujiunga na miamba hiyo ya Paris

Inasemekana mpaka sasa PSG ndio wanaongoza mbio za kunasa saini ya Messi
Screenshot_20210806-112214_GBInsta.jpg
 
Lionel Messi aliwasili Camp Nou jana ili asaini kandarasi mpya mpaka June 2026 lakini kutokana na kanuni za LA LIGA (SPAIN LA LIGA REGULATIONS) dili hilo limefeli

Ni hivi Ligi kuu na Ligi daraja la kwanza walisaini sheria tangu 2013 za kuhakikisha klabu zote zinakuwa na kiwango cha matumizi kwa mishahara ya Wachezaji na Makocha

Kutokana na suala hilo, Barcelona wamevuka kiwango kinachotakiwa na inasemekana sio Messi pekee bali Wachezaji wengi wa klabu hiyo wanashindwa kuwaingiza kwenye mfumo mpaka baadhi wapungue

Kutokana na hilo, PSG tayari wameanza mazungumzo ya kumnasa Lionel Messi ikiwa ni baada ya Messi kugoma mara ya kwanza
Screenshot_20210806-112403_GBInsta.jpg
 
Barcelona rasmi wamejiunga na Real Madrid kupinga mkataba kati ya LA LIGA na CVC, ikiwa ndio sababu ya Lionel Messi kutoweza kusainiwa

Mkataba huo wa miaka 50 walioingia LA LIGA utafanya klabu hizo mbili kupoteza zaidi ya Euro 800 Million kwa miaka 50 ijayo

La Liga walipitisha mpango huo ili kuzipa fedha kiasi klabu lakini hakitoshi kukidhi mahitaji, huko lengo Mama ilikuwa kuuwa wazo la EUROPEAN SUPER LEAGUE

Perez alikuwa Rais pekee Hispania kupinga mpango huo na alishaelezea athari zake na changamoto ila hakueleweka, ila sasa Mashabiki wa soka na mpaka Barcelona wameelewa kwanini Perez alipinga
Screenshot_20210806-112551_GBInsta.jpg
 
Staa wa Simba, Clatous Chama ‘Tripple C’ amesema msimu ujao wa ligi utakuwa na ushindani kutokana na jinsi wachezaji wapya wanaosajiliwa huku akitoa nafasi kubwa kwa matajiri wa Jiji la Dar Azam FC, kufanya vizuri kutokana na usajili wanaoendelea ndani ya timu hiyo.
.
“Natumaini Usajili unaofanyika na Azam ni dhahiri utaleta ushindani mkubwa msimu ujao kwenye Ligi, lakini pia itakuwa poa kuona Azam ikishinda kwa ajili ya mataji na vyote unajua tusiwe tu na Ligi ya Simba na Yanga, mara hii nadhani Azam FC wamesajili vizuri.”
.
Azam Fc hadi sasa imenasa saini ya wachezaji saba ambao ni golikipa, Ahmed Ali Suleiman ‘Salula’ kutoka Zanzibar, beki wa kushoto, Edward Manyama, kiungo mkabaji, Paul Katema (Zambia), viungo washambuliaji, Charles Zulu (Zambia), Kenneth Muguna (Kenya), washambuliaji Rodgers Kola (Zambia) na Idris Mbombo (DRC).
Screenshot_20210806-112844_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom