Makapuku Forum

Makapuku Forum

shululu asante sana kwa magazeti, asante mpenzi wangu husna muba kwa Historia, asante anko Lyon Lee kwa UF na asante BH BlessedHope kwa sala ya asubuhi. Zaidi asante wewe Kapuku kwa kuwa hapa.
Jumatano Njema and let us have a great rest of the day, ninafurahi kuwa hapa kwa sababu najua kuna watu wema humu, wenye ufahamu na maarifa wanayopenda na kufurahia kushare na zaidi, ujue nini, wanafurahia kutabasamu.
Tutaonana baadaye kidogo, itapendeza zaidi.
 
...asante umeshusa presha yangu, si unajua nina moyo ambao nimeupa kazi nyingine kabisa tofauti na kusukuma damu, kazi ya kukupenda wewe.
Ungependa jioni nikuletee chipsi zenye mayonnaise au mix tape ya Juma Baro

Mpendwa,kwasababu nakupenda basi chochote utachokileta nitakifurahia tu

Ila usikitaje maana nataka muda ule ule ndio nijue kuwa nimeletewa nn
Hapo VP?!
 
shululu asante sana kwa magazeti, asante mpenzi wangu husna muba kwa Historia, asante anko Lyon Lee kwa UF na asante BH BlessedHope kwa sala ya asubuhi. Zaidi asante wewe Kapuku kwa kuwa hapa.
Jumatano Njema and let us have a great rest of the day, ninafurahi kuwa hapa kwa sababu najua kuna watu wema humu, wenye ufahamu na maarifa wanayopenda na kufurahia kushare na zaidi, ujue nini, wanafurahia kutabasamu.
Tutaonana baadaye kidogo, itapendeza zaidi.
hata tukionana jioni haitodhuru
 
ANZA SIKU NA BWANA
KWA NENO NA MAOMBI
*YOHANA 10:14&15*
14 Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;
15 kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.
Mpendwa hebu tafakari juu ya;
1.Mchungaji mwema YESU.
■ Angalia wema wa
Yesu katika maisha
yako.
■ Alivyo kiongozi katika mambo yako mengi tena magumu yanayopita fahamu zàko na huna majibu lakini YESU hukupa majibu na kukuongoza kwenye njia sahihi na maamuzi sahihi.
■Ulipojikwaa na kuanguka, alikushika mkono na akakuinua akakutia moyo na akafunga jeraha zako. Akakwambia *ENDELEA MBELEE...* mwanangu kwa upendo mkuu mno.
2.Walio wangu nawajua.
● Je wewe unajulikana
kwa Yesu?
3. Nao walio wangu
wananijua.
●Je wewe unamjua
Yesu?
4.Nautoa uhai wangu
kwa ajili ya kondoo.
●Je wewe umetoa
maisha yako kwa
*YESU* ?
*TAFAKARI**
Nafasi bado ipo mkaribiashe Yesu ili awe *MCHUNGAJI* wako.
Barikiwa sana mtu wa Mungu uwe na *Jumatano* njema.
 
shululu asante sana kwa magazeti, asante mpenzi wangu husna muba kwa Historia, asante anko Lyon Lee kwa UF na asante BH BlessedHope kwa sala ya asubuhi. Zaidi asante wewe Kapuku kwa kuwa hapa.
Jumatano Njema and let us have a great rest of the day, ninafurahi kuwa hapa kwa sababu najua kuna watu wema humu, wenye ufahamu na maarifa wanayopenda na kufurahia kushare na zaidi, ujue nini, wanafurahia kutabasamu.
Tutaonana baadaye kidogo, itapendeza zaidi.
Ubarikiwe Obe asante
 
Siku zinaenda mbio sana, na kadiri zinavyosonga unagundua muda haukutoshi ndio maana biblia imetuhimiza tuukomboe wakati.

Tunapoteza muda mwingi sana kwenye mambo yanayotukwamisha, tunatumia muda mwingi kwenye mahusiano, na mambo yanayotuchelewesha sana.

Tunatumia nguvu akili na uwezo wetu hapo na kusahau muda wetu umepimwa na kusudi lililotuleta duniani hatujafikia hata robo, najaribu kuhesabu wangapi leo wana maumivu, mawazo, machungu, kilio, kisa tu wameachwa ama kuumizwa na waliowaamini?

Usimpe moyo wako mwanadamu maana material zinazouunda huo moyo anazijua Mungu tu, jijenge kwa Mungu usijijenge kwa mtu, muamini Mungu usimuamini mtu, wekeza kwa Mungu sio kwa mtu, jitoe kwa Mungu si kwa mtu. Ukishafanya hayo Mungu atakuheshimu ndipo ataleta mtu sahihi atakayekuja kukusaidia kuimarisha uliyoyajenga, atakuja kukusaidia na kuinuka nawe kwa Mungu.

Ni kweli tumefanya makosa ya uchaguzi, tumekosea wala hatuwezi kugeuka kurekebisha, na wakati mwingine tunahitaji maamuzi magumu maana muda unatuonyesha umbali tuluofika na tunaona gharama tulizotumia kuupoteza, NAKUTIA MOYO MAADAM UNAISHI HUJACHELEWA KAMWE WAWEZA JIPANGA UPYA NA KUINUKA TOKA KWENYE MAUMIVU, MAWAZO, HASIRA, NA UCHUNGU NA KUANZIA HAPO UKAUPANGA MUDA VIZURI SI TU KWA MAHUSIANO BALI HATA KWA MAMBO MENGINE. MUNGU AKUPE AMANI AMBAYO ULIOWAAMINI WAMEINYANG'ANYA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom