Muziki: Tabasamu la Sifa
Ni siku nzuri tena, na ndo inaishiria na niseme kweli. Sitojisikia vema kama sijakusalimia wewe kapuku mheshimika. Ujue nini, Jukwaa hili ni sehemu nzuri kwa sababu tu wewe uko hapa na si vinginevyo. Asante kwa uwepo wako na ama baada ya salamu nikukaribishe kwenye kipengele hiki cha muziki. Unajua huwa ninachagua muziki ninaoupenda kwanza ndo unakuja unaochagua wewe.
Leo itakuwa ni tofauti, kwanini, usiulize kwanini maana kwanini ni mwanzo wa ugomvi. sababu ya mimi kuandika leo ni kupongeza alichofanya anko wangu, ni kitendo cha kiungwana sana maana aliposikia Dr Luiz Shika kakosa mdhamini yeye kampigia simu inspector wa central, kesho tutakuwa na dr Luiz shika hapa jukwaani. Itapendeza sana. Ila nimejaribu kuangalia ukarimu wa anko wangu na kugundua makubwa sana, kumbe anajitahidi kuficha msala uliomkuta ugenini baada ya kupigana akitaka kurudishiwa hela zake kwa huduma mbovu za masaji alizopatiwa, yeye kazoea body to body massage huko kapewa tofauti alidhani yuko Sinza
Muziki sasa, karibu
ABJ , hapa utafurahia maana wewe utakuwa sehemu ya watu wema wote tuliomo humu hata mjomba wangu. Halafu kingine, nina mpenzi anayejulikana humu, ila hilo lisikukatishe tamaa endapo utaniona nakuja kukujulia hali. (maneno haya sio yangu ni ya mjomba)