
RAFIKI* *RAFIKI*
- Urafiki ni sehemu ya maisha, hata gaidi ana marafiki.
- Urafiki ni hitaji la moyo wa mtu, sote tunahitaji marafiki katika maisha yetu.
- Japo urafiki ni sehemu ya maisha, kila mtu ana wajibu wa kuchagua aina ya marafiki.
- Si kila mtu anaweza kuwa rafiki yako.
- Urafiki hufaa mkiwa na nia moja.
- Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu - Mithali 17:17
- Msingi wa urafiki ni upendo.
- Pasipo upendo, urafiki ni unafiki.
- Urafiki ni kushirikiana, kusaidiana, kuboreshana, kuinuana, kutiana moyo, kuambatana, kufurahi pamoja n ahata kulia pamoja.
- Linalomuhusu rafiki yako linakuhusu.
- Kuna marafiki ambao waweza kuwa karibu nawe zaidi hata ya nduguzo, wathamini hao marafiki, hasa kama wanakupeleka pazuri.
- Mchunguze sana rafiki yako kabla hujampa nafasi moyoni mwako, kwani rafiki anaweza kuwa sababu ya kuangamia kwako.
- Jifanyie marafiki wanaoweza kukunoa, na unaoweza kuwanoa.
- Jiulize, huo urafiki wenu umekuongezeaa nini?
- Huo urafiki wenu umekusaidia vipi katika hatma yako?
- Zaidi ya yote, urafiki ni kuwa na ushirika.
- Urafiki ni kupeana muda wenu.
AKUFAAYE KWA DHIKI NDIYE RAFIKI