Badaktari bigwa wa macho walifanya kila liwezekanalo zaituni aweze kupona, walishindwa na kusema macho hayo yameharibika sana hivyo kwa hapa Tanzania bado hawana uwezo wa kulitibu tatizo hilo, kwani waliambiwa kuwa tatizo hilo labda waende nje ya nchi... Sasa nje ya nchi na hali ya familia hio itaweza wapi,..
Wakati huo huku kwa zainabu akiwa na rafiki yake neema, alikuwa akichekelea sana kutokana na swala hilo
"tayari siku nyingi mtu haoni"
"lakini zai hivyo sio vizuri wewe"
"sasa nataka nianze kuwa kama yeye,.. Natamani kuolewa sana neema"
"kuwa kama yeye... Yaani uwe swala tano"
"ndio"
"huezi... Yaani huezi nakuapia huezi"
"nitajaribu nikishindwa basi.. Lakini staki kuona vijidume wanakuja kwa ajili ya zaituni"
Zainabu alikuwa akijiskia raha sana kwa kitendo alichokifanya kwa ndugu yake,
Sasa kuanzia siku hio hakuna aliokuja nyumbani kwa ajili ya zaituni yaani ile sifa ya kuletwa kwa posa ikawa haipo tena,.. Zaituni alipotoka hospitli akiwa kapewa miwani maalum na kifimbo kwa ajili ya kumseidia matembzi,... Atafanya kazi gani familia yao yenyewe ina hali duni sana,.. Aliona bora we omba kama watu wengine,... Lakini licha ya zainabu kumfanyia ndugu yake hivyo ili apate kuolewa yeye na sifa nyingi za kifamilia zimdondokee yeye.. Huezi amini mpaka leo hii hajaolewa wala kuchumbiwa tena ndio kwanzaa anatanga na njia, yaani kwa sasa kawa malaya wa kutupwa,...
SASA TURUDI KWENYE SIMULIZI YETU, MANA HIO ILIKUWA NI STORY KABLA YA UPOFU WA ZAITUNI
Sheby akiwa bado kasimama na dada huyo huku akilia sana kwa kutajiwa kuwa amekutana na mtu anafanana nae sana, ambae amemkuta supamaketi,...
"mbona unalia dada, kwani yule na wewe mpoje"
"ni stori ndefu sana kaka yangu"
Aliongea dada huyo ambaye bado hajajitambulisha kwa kijana sheby..
"pole sana dada yangu"
Lakini muda huo huo kuna mama alitokea eneo hilo..
"hujambo baba"
Alisalimia mama huyo huku kama anataka kuondoka na yule dada,
"sijambo shikamoo mama"
"marahaba..... Zai mwanangu kumekuchwa twende nyumbani"
Maskini kumbe yule aliokuja kumchukuwa alikuwa ni mama yake mzazi, tena hata mama yake alikuwa akilia kwa uchungu kutokana na hali aliofanyiwa mtoto wake,.. Na ndio aliokuwa akimpenda kuliko wote
"mama, kwani ni saa ngapi sasa hivi"
Aliuliza zaituni huku machozi yakimtoka, huezi amini hata sheby hakuweza kuvumilia, alitokwa na machozi mana ilikuwa inauma sana,..
"mwanangu ni saa kumi na mbili hii giza linaanza"
Zai hata muda unavyokwenda hajui, yapata miaka mitatu au minne toka afanyiwe unyama huo na dada yake,.
"sawa mama twende"
"leo umepata shing ngapi"
Mama huyo alimuuliza mtoto wake mana hakuna mtu anajua pesa kama kipofu, yaani ukimpa noti yeyote akiifikicha tu lazima ajue hii ni shilingi ngapi, mana bila kuwa hivyo hatojua pesa anayopewa na wasamaria wema... Hivyo ni mjuaji wa pesa kuliko kitu chochote kile
"leo nimepata elfu tano tu mama"
Aliongea zaituni huku mama akifurahi kwa kiasi alichokipata mtoto wake...
Sheby aliwaza kuwa yaani yeye katoka kulipia vitu vya laki tatu na arobaini, kumbe huku kuna watu wanasherehekea kupatikana kwa elfu 5 tu,... Chidi hajaamni macho yake,... Sasa mama akawa anamchukuwa mtoto wake ili kwenda nyumbani, mana anamleta asubuhi aombeeee afu jioni anakuja kumchukuwa,..
"Samahani mama angu"
Aliongea sheby huku akiwasimamisha, mama na mtoto wake
"bila Samahani mwanagu"
Alijibu mama huyo huku akigeuka..
"mama ni nani huyo unaemuita mwanangu"
Aliuliza zaituni kuwa ni nani aliomuita mwanae...
"ni yule kijana uliokuwa nae saa ile"
"haaaa kwani alikuwa bado hajaondoka"
"ndio"
Sheby aliwafuata wawili hao huku akitoa waleti na kutoa noti tano za shilingi elfu kumi kumi... Yaani jumla ni shilingi elfu 50,...
"itawaseidia hiii"
Sasa zaituni kuskia neno itawaseidia hii alimuuliza mama yake kiwa kijana huyo katoa shilingi ngapi
"mama... Katoa shing ngapi huyo kaka"
Sasa mama kabla hajasema, sheby akamnyamazisha na kumwambia katika skio kuwa
"mwambie nimetoa elfu tano tu"
Mama alishangaa kwanini kijana katoa elfu hamsini, lakini anataka amwambie zai kuwa imetolewa elfu tano tu
"mama niambie katoa shilingi ngapi"
"katoa elfu tano mwanagu"
"ooohhh mwenyezi mungu akujaalie wewe kaka... Nakuombea ufanikiwe kaka angu"
"ahsante dada"
"baba tunashukuru mwanangu"
"usijali mama"
Sasa zai kasikia pafyumu nzuri ya sheby...
"mama huyo kaka ndio mwenye huo mnukio"
Sheby akawahi kumwambia mama yake kuwa amwambie sio yeye kuna mtu kapita tu...
"hapana mwanangu kuna mtu kapita tu"
Sasa mama anazidi kujiuliza mbona huyu kaka hataki ajulikane kwa zaituni.... Mama alikuwa hapati jibu kwa kijana huyo...
"mama sasa hivi tuna elfu kumi si ndio eee"
Zaituni aliongea hivyo huku akitabasamu vizuri sana...
Yaani shilingi elfu tano tu katoa shukrani yote hio, sasa kama kajua ni elfu hamsini ingelikuwaje... Basi mama huyo na mtoto wake walikuwa wakiondoka lakini mama alikuwa kama ana maswali mengi sana kwa kijana sheby, mana kila anachotaka kujua mtoto wake, sheby hataki ajue sasa sijui alikuwa na maana gani..
Ikiwa ni mida ya saa 12 na dakika 45 sheby na mdogo wake wakiwa ndani ya gari kuelekea nyumbani,.... Akili ya sheby ilikuwa ipo kwa Zaituni tu, yaani Zaituni aliumbika yaani ni bonge la toto sio la kispoti spoti,...
Dakika chache yeye na mdogo wake walifika nyumbani,
"sheby mbona umechelewa hivyo lakini"
Aliongea mama yake sheby huku baba yake akiwa yupo hapo sebuleni,
"aahh mama, gari ilikuwa inasumbua kidogo, lakini hakuna shida mama"
"hofu juu yako lazima niwe nayo mwanangu"