Makapuku Forum

Makapuku Forum

RAFIKI* *RAFIKI*

- Urafiki ni sehemu ya maisha, hata gaidi ana marafiki.
- Urafiki ni hitaji la moyo wa mtu, sote tunahitaji marafiki katika maisha yetu.
- Japo urafiki ni sehemu ya maisha, kila mtu ana wajibu wa kuchagua aina ya marafiki.
- Si kila mtu anaweza kuwa rafiki yako.
- Urafiki hufaa mkiwa na nia moja.
- Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu - Mithali 17:17
- Msingi wa urafiki ni upendo.
- Pasipo upendo, urafiki ni unafiki.
- Urafiki ni kushirikiana, kusaidiana, kuboreshana, kuinuana, kutiana moyo, kuambatana, kufurahi pamoja n ahata kulia pamoja.
- Linalomuhusu rafiki yako linakuhusu.
- Kuna marafiki ambao waweza kuwa karibu nawe zaidi hata ya nduguzo, wathamini hao marafiki, hasa kama wanakupeleka pazuri.
- Mchunguze sana rafiki yako kabla hujampa nafasi moyoni mwako, kwani rafiki anaweza kuwa sababu ya kuangamia kwako.
- Jifanyie marafiki wanaoweza kukunoa, na unaoweza kuwanoa.
- Jiulize, huo urafiki wenu umekuongezeaa nini?
- Huo urafiki wenu umekusaidia vipi katika hatma yako?
- Zaidi ya yote, urafiki ni kuwa na ushirika.
- Urafiki ni kupeana muda wenu.

AKUFAAYE KWA DHIKI NDIYE RAFIKI
 
RAFIKI* *RAFIKI*

- Urafiki ni sehemu ya maisha, hata gaidi ana marafiki.
- Urafiki ni hitaji la moyo wa mtu, sote tunahitaji marafiki katika maisha yetu.
- Japo urafiki ni sehemu ya maisha, kila mtu ana wajibu wa kuchagua aina ya marafiki.
- Si kila mtu anaweza kuwa rafiki yako.
- Urafiki hufaa mkiwa na nia moja.
- Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu - Mithali 17:17
- Msingi wa urafiki ni upendo.
- Pasipo upendo, urafiki ni unafiki.
- Urafiki ni kushirikiana, kusaidiana, kuboreshana, kuinuana, kutiana moyo, kuambatana, kufurahi pamoja n ahata kulia pamoja.
- Linalomuhusu rafiki yako linakuhusu.
- Kuna marafiki ambao waweza kuwa karibu nawe zaidi hata ya nduguzo, wathamini hao marafiki, hasa kama wanakupeleka pazuri.
- Mchunguze sana rafiki yako kabla hujampa nafasi moyoni mwako, kwani rafiki anaweza kuwa sababu ya kuangamia kwako.
- Jifanyie marafiki wanaoweza kukunoa, na unaoweza kuwanoa.
- Jiulize, huo urafiki wenu umekuongezeaa nini?
- Huo urafiki wenu umekusaidia vipi katika hatma yako?
- Zaidi ya yote, urafiki ni kuwa na ushirika.
- Urafiki ni kupeana muda wenu.

AKUFAAYE KWA DHIKI NDIYE RAFIKI
Mama shikamoo

Asante sana
 
Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

"lakini zai, kwani hao watu wanaokuja wengi wao wakoje"
"ni Waislamu tupu"
"sasa huoni upo tofauti nae,.. Wewe ni muislamu lakini huta itikadi hio, hivyo tafuta wale ambao ni taipu yako"
"sawa lakini hata hao nilio nao, pia nikimwambia swala la kuoana wanabaki kunichezea tu, ila zaituni analetewa posa tena kwa heshima ya hali ya juu"
"Nikwambie kitu shost..... Badilika dada"
"kivipi we ney"
"sikiliza, ukishajua kuwa gari yako ni ya petroli, basi anza kuwa rafiki na muuza petroli"
"una maana gani lakini"
"kuwa kama mdogo wako"
"aahhhhhh mi nashindwa kutwa kushinda msikitini yaani siwezi... Ila ili wanione kama yeye lazima nifanye kitu"
Aliongea zainabu huku akipiga chini kwa hasira
"ufanye kitu gani"
Aliuliza neema ambae ni rafiki yake na zainabu,....
"mpaka sasa hivi mdogo wangu zaituni ndio anapendwa kuliko hata mimi, yaani lazima nimfanyizie"
Hata neema aliogopa sana huku akiwa kafumba mdomo, kana kwamba zainabu alikuwa katili wa kutisha
"zai, unataka umuue ndugu yako"
"simuuwi wala nini... Ila chamoto atakiona"
"mungu wangu zai sio vizuri lakini.. Kumbuka ni pacha wako huyo"
"pacha anaenifanya nikose raha mjini, nani kasema??.... Nakwambia nakupa siku tatu tu.. Na iwe siri yako wewe na mimi tu.. Utakula vingi kama utakuwa msiri"
Aliongea zainabu na kumfanya neema kuwa na wasiwasi juu ya maneno hayo, ila neema hakuonekana kuridhika na kitu anachotaka kukifanya zainabu...

ENDELEA..........



Zainabu na zaituni ni mapacha waliozaliwa tumbo moja, baba mmoja mama mmoja, ila tabia zao zilikuwa tofauti tofauti sana ukilinganisha na mapacha wengine ambao asilimia kubwa hua hawaachani katika upande wa tabia, lakini kwa zainabu na zaituni wamekuwa wakiishi kwa kuchukiana,

Tabia njema ndio iliomfanya zaituni kuwa kipofu hadi hii leo,...
"pacha anaenifanya nikose raha mjini, nani kasema??.... Nakwambia nakupa siku tatu tu.. Na iwe siri yako wewe na mimi tu.. Utakula vingi kama utakuwa msiri"
"lakini zainabu, kumbuka akipata ndugu yako nawe umepata, wacha aolewe tu"
"skia neema,.. Tuyaache hayo, hebu nionyeshe dula linalouza tindikali ni lipi"
Neema kuskia hivyo alishtuka huku akiziba mdomo kuashiria kuwa jambo hilo sio zuri kabisa kumfanyia mwenzio hivyo
"zai unataka kufanya nini"
"nataka asione, afu nione hao viherehere kama watakuja tena"
Aliongea zainabu huku akiamka kutika kwenye kiti alichokalia,
"lakini zai sio vizuri hivyo"
"we nawe kama hutaki uniambie, mi staki mtu mnafki bwana"
"kiukweli sijui duka lolote linalouza hicho kitu na hata kama ningelikuwa nalijua nisingekuonyesha hata chembe"
Neema aliongea huku akiondoka zake huku zai akimuita
"ney sasa unakwenda wapi"
"sitaki kushiriki unachotaka"
Kitendo hicho kilimfanya neema akae pembeni kabisa,...
Zainabu alifanya jambo hilo peke yake pasina kushirikiana na mtu yeyote yule,...

Baada ya siku kadhaa kupita, siku moja zaituni akiwa anatoka madrasa kupata elimu ya dini yake, ikiwa ni mida ya saa 12 hivi jioni sana na kagiza ka saa moja kalikuwa kakianza hivi,...
Wakati huo zainabu akiwa kajificha katika kona moja hivi, maskini ya mungu zaituni akiwa hajui hili wala lile, anajikuta anamwagiwa tindikali ya usoni,.. Uzuri wa tindikali hio haikuwa ya kuchubua ngozi bali ilikuwa ni spesho kwa macho tu, mana kuna ya kuchubua ngozi na macho pia, lakini kuna ya macho peke yake,... Zaituni alihisi kamwagiwa maji machafu mana harufu hio ilikuwa ikiendana na maji ya ukoko hivi,..
"sasa tuone hao vimbalala vyako kama vutakupenda tena"
Aliisikia hio sauti lakini hakumuona mtu tena,.. Na uzuri ni kwamba sauti hio anaijui ni ya dada yake ambae ni kulwa na yeye ni doto, hivyo ni dada yake,.. Sasa baada ya dakika 5 zaituni kufumbua macho alijikuta haoni kabisa, yaani hapo hapo alipo ni hapo hapo... Mpaka wasamaria wema walipotokea na kumchukuwa kisha kumpeleka hospitalini,
 
Badaktari bigwa wa macho walifanya kila liwezekanalo zaituni aweze kupona, walishindwa na kusema macho hayo yameharibika sana hivyo kwa hapa Tanzania bado hawana uwezo wa kulitibu tatizo hilo, kwani waliambiwa kuwa tatizo hilo labda waende nje ya nchi... Sasa nje ya nchi na hali ya familia hio itaweza wapi,..

Wakati huo huku kwa zainabu akiwa na rafiki yake neema, alikuwa akichekelea sana kutokana na swala hilo
"tayari siku nyingi mtu haoni"
"lakini zai hivyo sio vizuri wewe"
"sasa nataka nianze kuwa kama yeye,.. Natamani kuolewa sana neema"
"kuwa kama yeye... Yaani uwe swala tano"
"ndio"
"huezi... Yaani huezi nakuapia huezi"
"nitajaribu nikishindwa basi.. Lakini staki kuona vijidume wanakuja kwa ajili ya zaituni"
Zainabu alikuwa akijiskia raha sana kwa kitendo alichokifanya kwa ndugu yake,
Sasa kuanzia siku hio hakuna aliokuja nyumbani kwa ajili ya zaituni yaani ile sifa ya kuletwa kwa posa ikawa haipo tena,.. Zaituni alipotoka hospitli akiwa kapewa miwani maalum na kifimbo kwa ajili ya kumseidia matembzi,... Atafanya kazi gani familia yao yenyewe ina hali duni sana,.. Aliona bora we omba kama watu wengine,... Lakini licha ya zainabu kumfanyia ndugu yake hivyo ili apate kuolewa yeye na sifa nyingi za kifamilia zimdondokee yeye.. Huezi amini mpaka leo hii hajaolewa wala kuchumbiwa tena ndio kwanzaa anatanga na njia, yaani kwa sasa kawa malaya wa kutupwa,...

SASA TURUDI KWENYE SIMULIZI YETU, MANA HIO ILIKUWA NI STORY KABLA YA UPOFU WA ZAITUNI

Sheby akiwa bado kasimama na dada huyo huku akilia sana kwa kutajiwa kuwa amekutana na mtu anafanana nae sana, ambae amemkuta supamaketi,...
"mbona unalia dada, kwani yule na wewe mpoje"
"ni stori ndefu sana kaka yangu"
Aliongea dada huyo ambaye bado hajajitambulisha kwa kijana sheby..
"pole sana dada yangu"
Lakini muda huo huo kuna mama alitokea eneo hilo..
"hujambo baba"
Alisalimia mama huyo huku kama anataka kuondoka na yule dada,
"sijambo shikamoo mama"
"marahaba..... Zai mwanangu kumekuchwa twende nyumbani"
Maskini kumbe yule aliokuja kumchukuwa alikuwa ni mama yake mzazi, tena hata mama yake alikuwa akilia kwa uchungu kutokana na hali aliofanyiwa mtoto wake,.. Na ndio aliokuwa akimpenda kuliko wote
"mama, kwani ni saa ngapi sasa hivi"
Aliuliza zaituni huku machozi yakimtoka, huezi amini hata sheby hakuweza kuvumilia, alitokwa na machozi mana ilikuwa inauma sana,..
"mwanangu ni saa kumi na mbili hii giza linaanza"
Zai hata muda unavyokwenda hajui, yapata miaka mitatu au minne toka afanyiwe unyama huo na dada yake,.
"sawa mama twende"
"leo umepata shing ngapi"
Mama huyo alimuuliza mtoto wake mana hakuna mtu anajua pesa kama kipofu, yaani ukimpa noti yeyote akiifikicha tu lazima ajue hii ni shilingi ngapi, mana bila kuwa hivyo hatojua pesa anayopewa na wasamaria wema... Hivyo ni mjuaji wa pesa kuliko kitu chochote kile
"leo nimepata elfu tano tu mama"
Aliongea zaituni huku mama akifurahi kwa kiasi alichokipata mtoto wake...
Sheby aliwaza kuwa yaani yeye katoka kulipia vitu vya laki tatu na arobaini, kumbe huku kuna watu wanasherehekea kupatikana kwa elfu 5 tu,... Chidi hajaamni macho yake,... Sasa mama akawa anamchukuwa mtoto wake ili kwenda nyumbani, mana anamleta asubuhi aombeeee afu jioni anakuja kumchukuwa,..
"Samahani mama angu"
Aliongea sheby huku akiwasimamisha, mama na mtoto wake
"bila Samahani mwanagu"
Alijibu mama huyo huku akigeuka..
"mama ni nani huyo unaemuita mwanangu"
Aliuliza zaituni kuwa ni nani aliomuita mwanae...
"ni yule kijana uliokuwa nae saa ile"
"haaaa kwani alikuwa bado hajaondoka"
"ndio"
Sheby aliwafuata wawili hao huku akitoa waleti na kutoa noti tano za shilingi elfu kumi kumi... Yaani jumla ni shilingi elfu 50,...
"itawaseidia hiii"
Sasa zaituni kuskia neno itawaseidia hii alimuuliza mama yake kiwa kijana huyo katoa shilingi ngapi
"mama... Katoa shing ngapi huyo kaka"
Sasa mama kabla hajasema, sheby akamnyamazisha na kumwambia katika skio kuwa
"mwambie nimetoa elfu tano tu"
Mama alishangaa kwanini kijana katoa elfu hamsini, lakini anataka amwambie zai kuwa imetolewa elfu tano tu
"mama niambie katoa shilingi ngapi"
"katoa elfu tano mwanagu"
"ooohhh mwenyezi mungu akujaalie wewe kaka... Nakuombea ufanikiwe kaka angu"
"ahsante dada"
"baba tunashukuru mwanangu"
"usijali mama"
Sasa zai kasikia pafyumu nzuri ya sheby...
"mama huyo kaka ndio mwenye huo mnukio"
Sheby akawahi kumwambia mama yake kuwa amwambie sio yeye kuna mtu kapita tu...
"hapana mwanangu kuna mtu kapita tu"
Sasa mama anazidi kujiuliza mbona huyu kaka hataki ajulikane kwa zaituni.... Mama alikuwa hapati jibu kwa kijana huyo...
"mama sasa hivi tuna elfu kumi si ndio eee"
Zaituni aliongea hivyo huku akitabasamu vizuri sana...
Yaani shilingi elfu tano tu katoa shukrani yote hio, sasa kama kajua ni elfu hamsini ingelikuwaje... Basi mama huyo na mtoto wake walikuwa wakiondoka lakini mama alikuwa kama ana maswali mengi sana kwa kijana sheby, mana kila anachotaka kujua mtoto wake, sheby hataki ajue sasa sijui alikuwa na maana gani..

Ikiwa ni mida ya saa 12 na dakika 45 sheby na mdogo wake wakiwa ndani ya gari kuelekea nyumbani,.... Akili ya sheby ilikuwa ipo kwa Zaituni tu, yaani Zaituni aliumbika yaani ni bonge la toto sio la kispoti spoti,...

Dakika chache yeye na mdogo wake walifika nyumbani,
"sheby mbona umechelewa hivyo lakini"
Aliongea mama yake sheby huku baba yake akiwa yupo hapo sebuleni,
"aahh mama, gari ilikuwa inasumbua kidogo, lakini hakuna shida mama"
"hofu juu yako lazima niwe nayo mwanangu"
 
"sawa basi nisamehe"
Lakini ghafla simu ya baba yake inaita,...
"eeehh halo mr magesh habari yako"
Ni baba yake na sheby wakiwa wanaongea biashara na mfanyabiashara mwenzake aliopo india, na sheby anamjua mtu huyo
"nzuri tu mr rashidi hali yako huko Tanzania"
"aahhh huku swalama tu magesh"
"sasa... Nina mzigo unatakiwa uende kongo,.. Ila utatakiwa uje india ili uueskoti mpaka huko"
"aahhhh sawa kabisa,... Nitafanya hivyo"
Sasa sheby kusikia ishu za india alijiskia raha sana mana anakuoenda sana huko,...
"aaahhh sasa ngoja niweke mambo sawa, kisha nitakupa mwongozo"
"sawa mr magesh"
Sasa simu ilipokatwa tu sheby kadakia juu kwa juu,...
"shikamoo mzee"
"marahaba vp"
"safi tu... Naskia kuna ishu ya kwenda india"
"ndio, ila hio huiwezi we zako za kenya uganda, huko niachie mimi"
Aliongea mzee huyo huku akiendelea kuangalia tv, lakini ghafla mama sheby anaingilia kati
"lakini baba sheby, kwani mtoto akijua na huko kuna shida gani"
"yes mamiii hebu mwambie baba... Kama vipi nitume nikauchukuwe huo mzigo"
"wewe sheby huezi.. Ni mizigo ya thamani sana huko huezi wewee utahari kazi.. Nitakwenda mwenyewe"
"babaaa, nipe nafasi hio moja tu basi yaani hio tu"
"kwanza ulishawahi kwenda india wewe"
"si tulishaendaga wote"
"nasemea peke yako"
"aahhhh peke yangu sijawahi kwenda"
"sasa je"
Sheby alikuwa anaitaka sana hio safari ya india na sijui ana ishu gani na huko
"baba.... Niamini mi mtoto wako nitume niende huko..nitafanya vizuri"
"mama sheby... Huyu mtoto mbona hanielewi... Hebu mwambie basi mwanao"
"lakini Baba sheby naomba nikuulize swali moja tu... Baada ya wewe nani atamiliki hizi mali"
"si hili jinga"
"heeeeeeee kawa jinga tena"
"ndio.... Leo nimeangalia kwenye akaunti ya kampuni, imepungua milioni 15, kazipeleka wapi? Leo nije nimuachie kazi kubwa kiasi hicho.. Hapana Siwezi"

Je? Unajua sheby anataka kwenda india ili iweje... Na Je? Ni kweli kachukuwa milioni 15???.. Vipi kuhusu zaituni???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom