Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Viporo

U khali gani Kapuku mheshimika, leo ni Jumamosi na kesho ni Jumapili, nakukumbusha tu maana wengine haya mambo ya kuzijua siku si muhimu. Binafsi nimekuwa na wakati mzuri leo hasa baada ya mazoezi na kisha kufuatilia mambo ya soka. Sitaki kukuuliza wewe ulifanya nini, maana wikend ina mengi, kuanzia kutumika kimwili hadi kubet, na asikwambie mtu wote wanaobet walishaliwa.

Nimekumbuka kitu leo na nikafurahi nikaona kama mimi nilifurahi nawe unaweza kukifahamu na hulazimiki kufurahi maana kinaweza kukukumbusha uliyosahau. na si unajua uhuru uko kwenye kusahau, hebu fikiria kama tungekuwa hatusahau? Sisi wenye vitambi vya kawaida ungetuonea wapi, vitambi vya kawaida maana yake ni vitambi vile una uhakika wa kula kiporo asubuhi kwani usiku wa jana ulikula kitu fresh na hudaiwidaiwi na kama kiporo kimechacha yaani kiko kwenye siku zake basi jua kuwa kuna chumvi za kichina zinakata ukiporo.

Muziki sasa, leo ni zamani kidogo, yes, hakuna kiporo cha leo na ndo maana bora kuungana na makaveli10 asiyetaka mambo ya kununua kitu orijino, unaenda kwa kitu kilichotumika maana hapo unakuwa na uhakika wa ubora


Umenikosha sana hapo kwenye masuala ya used spare part...


Aisee shukrani ndugu obe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom