THE DOM
Sehemu Ya 9
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Instagram....
Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←
SON OF PRESIDENT GU
nilikuwa nasumbuliwa na tumbo la kuendesha"
Mara mr deo akaingilia kati,...
"sikiliza kijana.... Jana tumeona ulichokifanya kule porini,... Sasa endepo hutokuwa na sisi, tunakutimua hapa jeshini... Na wala usitake kubisha, hana umeuwa watu wawili, na mmoja ndio huyo yupo hospitali hoi hoi.... Hii ni kesi"
Sasa sahi yeye alijua tu hapa anapelelezwa kichini chini...
"nilitokea wapi kwenda huko"
"tunakujua, na aliekuleta tunamjua wala usitake kutuumiza kichwa... Umeshajua sisi ni wauzaji wa silaha hapa jeshini... Sasa unachokifanya hakitokuseidia lolote.... Ungana nasi.. Yule mgonjwa katuambia kila kitu sema hatujataka kukudhalilisha mbele za watu pale paredi.... Yule mgonjwa kasema, ulikuwa umevaa saa kubwa,.. Afu hio saa inawaka taa... Hapa jeshini waliovaa saa ni walimu tu, sasa je? Wewe ni mwalimu"
Alipomaliza kuongea mr deo, mara mr nyange akatoa briefcase ya pesa na kuiweka mezani huku akisema
"kijana... Kabla ya yote... Kuna milioni 100 hii hapa... Yaani ukikubali tu, chukuwa hizo pesa"
ENDELEA.........
Mr Nyange aliona hakina njia nyingine ya kumteka kijana huyo, ispokuwa pesa tu,... Lakini sasa ubaya wao ni kwamba hawa hawajui kama sahi ni mpelelezi wa serikali, tena mwenye kiwango cha hali ya juu mno,... Kwahio wanachokijua kwa sahi wao wanadhani ni kijana tu ambae anapenda haki hapendi vitu viende tofauti, kumbe sivyo, bali sahi ni mpelelezi tena aliepitia ujeshi nchini korea,.. Lakini hawa hawalijui hilo kuwa sahi ni mpelelezi wa serikali, wanajua ni kijana mpenda haki na ndio mana akazuia silaha kusafirishwa,...
Sahi alitoa macho kuona lile briefcase la pesa taslimu shilingi milioni 100, na ni zake endapo atakubali kujiunga nao,...
"sawa,... Ila kila kinachoendelea kwenu nami napaswa kukifahamu"
Huezi amini sahi alikubali kujiunga nao, na kadhihirisha kuwa yeye ndie alie wauwa wale magaidi kule porini,
"hilo ondoa shaka kijana, kila kikao lazima tukuhusishe"
"sawa,...nipo tayari kujiunga nanyi"
Sahi aliisaliti serikali yake, ila sahi alionekana msaliti kabla, mana kabla hajaja jeshini alionekana na kifaa cha pesa kiitwacho Discate of money (DOM).... Na kifaa hicho kinatafutwa na serikali yake na yeye ndie aliepewa kazi, na yeye ndie anae kimiliki kifaa hicho,... Yaani sahi ni msaliti kabla hivyo hapa kadhihirisha usaliti wake....
"ok... Ila kijana kuna swali naomba kuuliza. Kuna picha nilishawahi kuiona katika simu yako... Ile picha una uhusiano gani nayo"
Sahi kabla hajajibu aliitoa simu yake na kuiweka mezani huku akisema..
"nina rafiki yangu mmoja nilisoma nae, aliitwa Sharbiny... Alikuwa ni rafiki yangu sana, na yeye alikuwa jeshini, mimi nilikuwa sipendi kujiunga na jeshi, lakini rafiki yangu alipofariki dunia, ndipo nikaamua kumuunga mkono... Nakumbuka kabla ya yeye kujiunga tulikuwa tukienda sehemu ya mazoezi ya mapigano,... Na yeye alikuwa akinisihi kujiunga na mafunzo ya jeshi, na aliahidi kunisaidia kwakuwa baba yake alikuwa mkuu wa jeshi,.. Lakini pia sikutaka kujiunga... Nilikuja kujua umuhimu wake pale alipokufa, ndipo nikaamua kujiunga na jeshi... Nilimpenda sana rafiki yangu na ili nimuenzi na kumkumbuka, ndio nimeweka picha ya mama yake katika simu yangu, mana hata mama yake alikuwa ana upendo nami kwakuwa nilikuwa rafiki wa mtoto wake"
Sahi alimaliza kuongea ukweli wake wa hapo awali,...
"je huyo baba yake unamfahamu"
"hapana, sijawahi kumuona"
"mbona ndio mimi baba wa Sharbiny.. Na ndio mana nikakuuliza kuhusu hio picha"
"waooooooo.... Kumbe nimefanikiwa kukutana na baba wa rafiki yangu"
"ndio... Karibu kwenye ulimwengu wa wanajeshi"
"Ahsante sana mzee wangu"
Sasa mzee kaamini moja kwa moja kuwa sahi ni rafiki wa mtoto wake, na General Nyange na deo, wanajua kuwa sahi ana wiki ya jeshi na ana wiki ya TSS, basi sahi aliondoka huku akiwa kashika kibegi chake cha pesa akielekea chumbani kwake,
Wakati huo mageneral wawili wakiwa hapo ofisini kwao, walikuwa wakigongesheana mikono kwa kumjua kijana machachari kama huyu
"Deo, huyu kijana anafaa tumtumie kwenye kazi zetu,... Tena uzuri ni kwamba kazi yake ina Options mbili.. Anafanya hapa TMA na TSS, sasa urahisi wa kupata ule mzigo uliobakia kule ni mkubwa sana kupitia huyu kijana"
"Nyange una akili sana, unajua kupata kijana jasiri kama huyu ni ngumu sana"
"vijana wote tuliowaweka mbele, wamekwisha kufa,.. Hawakuwa na uwezo, sasa kama huyu peke yake kauwa qale wajinga na silaha zikabaki"
"deoooo.... Hapa tutawini, mana kijana ana kazi za Dar es Salaam, hivyo ni rahisi kufanikiwa kwa urahisi"
Sasa wakiwa wanazidi kuingea mara ghafla mwaju kaingia,...
"ooohhh binti karibu"
Mr deo alimkaribisha mwaju
"sasa binti, kazi yako tuliokupa imekwisha, sasa huna haja ya kumfuatilia tena, ila ukiona jambo lolote baya kwale, tunaomba utudokezee.... Kwanza shika milioni tano hizi.. Ahsante kwa kazi nzuri, mana bila wewe jana kwenda ndani kwake, imeturahisishia sana kumbana kijana mpaka akakubali"
"Ahsante sana generally, nitafanya kama ulivyosema, na nitazidi kuwa nae karibu pia"
Aliongea mwaju huku, akiziweka pesa zake vizuri.. Na pesa hizo ni zile walizouza silaha na hazijakwenda.. Sasa hizo pesa ndio hizi wanazogawa gawa mpaka sasa,...
Sasa huku nchini Kenya, katika kambi ya waasi waliokuwa wakisubiri silaha toka Tanzania, lakini mpaka sasa ni hewa..
"mbona hawa watu hawafiki na watakuwa wamepatwa na nini"
Aliongea mkuu wa kikosi hicho, kila wakipiga simu hazipatikani... Na gari lao huku Tanzania limetelekezwa porini hivyo hakuna hata wakisema wafuatilie watashindwa kujua kilichoendelea, na maiti zimesha zikwa muda mrefu sana... Na yule mgonjwa alishauwawa kwa kauli ya sahi, mana sahi ni mpelelezi na anajua jangili akiwa hai ataleta athari gani... Sasa huku kenya wamechafukwa wanataka silaha na watu wao,...
Baada ya wiki moja kupita, sahi akiwa anawasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mafunzo ya Tss, sasa huku ndipo kazi inapomhusu yeye,. Sahi aliingia katika jumba lake la kifahari, huku akiwa na briefcase ya pesa taslimu shilingi milioni 100,...alizopata kule kambi ya jeshi baada ya kukubali kujiunga na mageneral wauza silaha,... Jumba hilo la serikali ambalo ni maalum kwa maisha ya sahi, lina kamera kila kona lakini kasoro chumba chake cha kulalia ndio hakijawekwa kamera,... Basi alitoa pesa zake na kuzipangilia vizuri katika begi maalum linaloweza kufichika kwa urahisi mzuri... Alitafuta sanduku lake na kuitoa ile DOM (Discate Of Money).. Na kuiangalia kwa kucheka...
"lazima imjue mwenzake alipo"
Aliongea sahi akimaanisha kuwa ni lazima ajue codes Number zake zilipo, mana bila codes number haiwezi kuchapa pesa hata kidogo..
Kesho yake asubuhi akiwa katika gari yake yenye Number za usajili wa usalama wa taifa,.. Kwanza transmission ya sikioni ilikuwa hewa,
"GU naongea..."
"ndio mkuu hali yako"
"salama.. Nakuona umeingia mjini"
"ndio mkuu na sasa naelekea TSS"
"ok... Kuwa mpole na kazi yako"
"sawa mkuu"
Rais GU ana mawasiliano na sahi kwa kitumia transmission za siri sana, lakini sasa transmission nyingi huonekana katika sikio, sasa mbona ya sahi haionekani, je imeunganishwa vipi mpaka isionekane, mana sikio jeupee, halina kinasa sauti lakini sahi anasikia... Katika geti la TSS, sahi anafunguliwa kama mgeni katika kitengo hicho... Mpaka akaingia katika kile kibanda kilicho kama gereji lakini ukifika hapo hio sehemu inabonyea chini na kukushusha chini, ambako ndio makao makui ya tss,...
Sasa kuna wakuu wa kitengo hicho, kama mageneral, na General mmoja anamjua sahi, ila kuna general mwingine huyo kijana kijana sana, aitwaye JJ huyu ni mtoto wa rais kapewa cheo kutokana na elimu yake, lakini sasa kijana huyo alipo mwona sahi, alishangaa sana zile hatua anazopiga sahi,.. Yaani huyu JJ alikuwa akimshangaa sana BB...
"mkuu vp mbona unamtazama sana huyu mgeni"
Aliulizwa na kijana mmoja aliopo katika kitengo cha computer,...
"huyu mtu ana hatua kama rafiki yangu,.. Yaani anatembea hivyo hivyo"
Aliongea JJ huku akizidi kumtazama sahi,... Sasa saho nae kajua kuwa anaangaliwa sana na General JJ...
"habari yako generally JJ"
Sasa JJ alizidi kutaharuki pale aliposikia sauti ya sahi,... Yaani vinafanana na rafiki yake kasoro sura tu ndio havifanani kabisa...
"salama tu hali yako"
"nzuri... Ahh mimi ni mgeni, naitwa salahe Rashidy, nilikuja juzi hapa lakini kwa bahati mbaya sijaweza kuku kuta General wangu"
"sawa kabisa.... Hakuna shida na hiki ndicho kitengo husika"
JJ alikuwa akiongea lakini hisia zake zinahisi ni rafiki yake tu, hata iweje, japo rafiki yake alifariki dunia akiwa mazoezini,.. Yaani JJ au Joseph John alikuwa na urafiki mkubwa sana yule mtoto wa General wa jeshini, yaani yule mkuu wa majeshi kule kambini....
Sahi yeye alipitiliza mpaka katika computer yake, mana siku ile ile, alipatiwa kisehemu chake chenye computer, na sio yeye tu bali ni watu wote wa vitengo hivyi, ni lazima ajue maswala ya computer, na kazi kubwa hufanywa na computer, hivyo lazima uijue computer,....
Sasa sahi alipofika katika computer yake, aliingiza program ya ile DOM kisha akaanza kuichambua kwa undani wake,.. Ipoje na inafanya kazi vp, na mashine yake ni ipi... Lakini akiwa anaendelea kufanya hivyo mara alibanwa na haja ndogo, hivyo akaacha kile alichokuwa akikifanya kisha akaelekea toilet, mana hapo ni ofisi moja lakini imegawanywa vijichumba vidogo dogo kusudi kila mmoja akae sehemu yake apeleleze kitu chake,.. Sasa sahi yeye kaja kama mwanafunzi lakini kitu alichokiacha katika computer yake, ni kitu kikubwa sana ambacho kilitakiwa kufuatiliwa na mageneral wakubwa ila sio mwanafunukama huyo,... Sasa JJ akawa anakuja katika ofisi ya BB,... Alishangaa sana kwa kile alichokikuta katika skrini ya sahi,...
"hii si DOM hiii??... Huyu anaitafuta kama nani"
Aliongea JJ lakini alikuwa kama anajiuliza mwenyewe,.. Joseph hakuridhika na jambo hilo alitoka na kuelekea chooni kule kule alipo sahi ila Joseph hajui kama sahi yupo huko,.. Sasa JJ ndio anapiga simu lakini haijulikani alikuwa akimpigia nani ila ilionekana ni simu ya siri sana... Na huyu ni mtoto wa rais,..
"halo habari yako mkuu"
"salama.. Vp mbona kama una wasiwasi hivyo"
Sasa sahi anasikia ishu nzima ya JJ anavyoongea na huyo mtu... Kama kawaida ya saa yake kurekodi,..
"kuna kijana ananipa mashaka sana hapa kitengo"
"ana nini"
"Naona ana program ya DOM sasa huyu ni nani na ni mwanafunzi"
"whaaaat?? Unasema ana program ya DOM??.... Kaipata wapi?"
"siwezi kufahamu, ila mkuu nina wasiwasi na wewe, mana kijana huyu ni mgeni katika kitengo hiki, iweje ajue siri hii.... Kwanza niambie hio DOM ipo"
"ndio ninayo... Na yule mnunuzi anakuja kuichukuwa mwezi ujao sasa DOM Codes ndio inatakiwa haraka sana"
Itaendelea.....
Je? Huyu anaeongea nae ni nani...
ITAENDELEA.....