THE DOM
Sehemu Ya 8
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Instagram....
Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←
SON OF PRESIDENT GU
dokta, tunaomba ututolee huyu kijana na kubaiskeli cha wagonjwa... Afu kamanda kuti, naomba unikusanyie wanafunzi wote hapa kambini"
Aliongea general Nyange huku akiwa na hasira juu ya tukio hilo,....
"lazima tufahamu..... "
Nusu saa mbele, kundi la pili linawasili kambini kutoka mazoezini, wakati huo kundi la kwanza lipo katika paredi ya utulivu,.. Mbele ya paredi yupo yule gaidi alio tayari kwa kumtaja mtu aliohusika na tukio hilo..
Sasa sahi hajui hili wala lile,... Alitahamaki kuona sura ya yule gaidi ipo hai,..
"mungu wangu... Kumbe hili fara halijafa"
Aliongea sahi huku wasiwasi ukimjia, kwani nia yake ni kugundua mengi zaidi katika kambi hio, sasa endapo atagundulika mapema, itakuwa tabu
General leo ndio aliokuwa akiwapanga line wenyewe, yaani mpaka wanafunzi wote waka kaa sawa katika line zao,...
"gidi... Naomba utuonyeshe mhusika wa tukio la jana"
Sahi pale alipo moyo ulikuwa unakwenda mbio,.. Mana lazima ajulikane ni yeye,... Sasa kumbe huyu gaidi ha......
ENDELEA............
Wakati huo gaidi akiletwa hapo paredi, viongozi walikuwa makini sana na gaidi lile, mana ila General nyange anawajua watu hao sema tu anajibalaguza na kuwa na ujasiri ili akamatwe huyo aliewafanyia hivi, na licha ya hivyo, pia General ana wasiwasi sana na kibarua chake kuota nyasi, mana lazima kajulikana uharamia ambao anaufanyaga siku zote, sasa leo kabainika japo mtu aliombaini hajajulikana na ndio wanamsaka kwa udi na uvumba,...
Yule jamaa aliletwa mbele ya wanafunzi wote, mana hakuna aliefanya wa nje ispokuwa ni hawa hawa wanafunzi au walimu ambao hawaijui hio ishu,...
Rahim alikuwa kakaa tayari tayari kwa kutajwa mana ana kuna wakati alivyokuwa akiwanyonga alikuwa akiwapiga pocha kupitia saa yake, sasa ule mwanga wa flash huenda akawa kaonekana na mtu huyo, gani aliwekwa katika akiwa hajiwezi mana aliponea chupu chupu kufa,....
Sasa kumbe huyu gaidi hawezi kuongea kutokana na kile kinyongo alichokipata toka kwa sahi, sauti hana lakini kwa macho tu pia anaweza kumtambua mtu,... Sahi alikuwa na wasiwasi sana juu ya kujulikana,... Lakini sasa ujue sahi ni mpelelezi makini sana, tena ni mtu anaeipenda kazi yake,.. Alimwangalia yule gaidi alivyokuwa anapitishwa karibu lakini cha ajabu alikuwa haangalii sura, yeye alikuwa anaangalia mikono, na hapo ndipo akagundua kuwa mtu huyo alikuwa akiangalia saa za mikononi, mana ndio iliompiga picha, afu mbaya zaidi walikuwa wakikaribia karibu na sahi, afu sahi na ule msaa wake upo mkononi,... Kumbe gaidi hajaona sura ya mtu alio wanyonga, ila kile kitendo cha kuoigwa picha kwa kutumia saa, huyu gaidi ndio kitendo alichokikariri katika macho yake na sio vinginevyo.... Na wakati huo wanafunzi wote mikono mbele, hivyo sahi kuivua hawezi mana mstari umenyooka afu wamesimama kwa utulivu mkubwa, hivyo mtu mmoja akijigusa anajulikana....
Ghafla alikohoa mwanafunzi mmoja, General kasikia, akauliza
"nani analeta ujinga"
Aliuliza sahi mana hajui nani aliokohoa...
"samahani mkuu, naona ni vumbi vumbi tu"
Kumbe aliokohoa alikuwa ni sahi, na kudai kiwa amepatwa na vumbi, basi General ndiye aliekuwa anapointi macho ya gaidi pale yatakapotua basi ndio hapo hapo... Huku gaidi akiendeshwa kwa kutumia kibaiskeli cha wagonjwa.... Sasa walipofika karibu na sahi, General wasiwasi wake ni sahi, yaani hata asipo pointiwa yeye lakini ana wasiwasi na huyo kijana, japo ana kopi kopi za mtoto wake aitwaye Sharbiny ambaye nae alikufa katika mazoezi ya kijeshi,.... Sasa walipofika pale walisimamisha kibaiskeli ili tu gaidi apate muda wa kumkagua... Lakini pointi anayoitaka gaidi ni saa, lakini sahi kwa wakati huo hakuwa na saa mkononi,.... Yaani ushapu ni kitu kizuri sana, yaani kitendo cha kukohoa tu na saa imetolewa... Na alifanya hivyo kwasababu akikohoa ni lazima atikisike hivyo upenyo wa kuivua saa ulikuwepo mzuri wakati wa kukohoa... General alipitisha baiskeli mbele, lakini hawakufanikiwa kumjua mhusika,... Sasa hapo General kichwa moto, wakati huo gaidi anarudishwa hospitali, na General anaingia ofisini kwake....
Wanafunzi wengine hawajui kinachoendelea hapo,... Basi sahi akavaa saa yake na hapo wakaendelea na mazoezi ya hapo hapo kambini mana walishapoteza muda mwingi katika sakata hilo la kumjua mtu aliohusika kuwauwa hawa magaidi na kuzifanya silaha kurudi mikononi mwa kambi ya jeshi
Mazoezi yakiwa yanaendelea, mwaju alikuwa akimtazama sana sahi,... Mwaju ni mwanafunzi lakini ana muda mrefu hapa shuleni, hakosi miaka miwili au mitatu, na alikuwepo hata kipindi cha mtoto wa General alipokufa huyu mwaju alikuwepo, hivyo hata yeye anamshuku kuwa mtoto wa General, lakini tofauti yao ni sura, yaani sura hawafanani hata chembe, mana Sharbiny alikuwa maji ya kunde afu ana Kidoti kwenye sura upande wa kushoto chini ya jicho lake
Lakini hayu ni mweusi afu hana kidogo, na oia hawafanani hata kidogo, na huyu anaitwa salehe, na huyo anaitwa Sharbiny, ni watu wawili tofauti kabisa... Lakini mwaju kile alichokiona kqenye simu, kinazidi kumpa mashaka juu ya kijana huyo..
"mwaju"
"yes mkuu"
"nakuitaji ofisini"
General nyange alimwita mwaju aje ofisini kwake huenda kuna kitu anataka kumuuliza, ila mwaju nae ana ham ya kuongea na General kwa kile alichokiona kwenye simu ya sahi,
Mwaju pasina uoga wa aina yeyote aliingia ofisini kwa General na anajua kitu anacho itiwa
"hivi huyu kijana umeshapata fununu zozote"
Aliuliza mr Nyange au general Nyange
"yes, jana usiku nilikuwa katika chumba chake"
"enhee, umemkuta anafanya nini"
"Kiukweli sikumkuta"
"what??.... Ulikwenda saa ngapi"
"ilikuwa ni mida ya saa saba mpaka saa nane za usiku"
Sasa general Nyange kusikia mida hio ndio alikuwa porini kule wanapakia silaha,...
"enhee, alirudi saa ngapi"
"Kiukweli hajarudi, nadhani ni mpaka asubuhi mana nimetoka akiwa bado hajarudi"
"yes,... Lazima atakuwa ni yeye tu.... Huyu kijana ni wa kumuondoa"
Aliongea general nyange, maneno yaliomfanya mwaju kushtuka sana
"General..... Kwanini lakini... Huenda yule ni mtoto wako"
"ina maana mtoto wangu humjui wewe?... Mtoto wangu anafanana na yule kweli... Yaani hata sura haziendani labda sauti tu"
"lakini mbona kwenye simu yake nimekutaka picha ya mke wako"
"ati unasemaje?... Picha ya mke wangu mimi"
"ndio... Ila ni picha ya mama sheby yule mke mkubwa... Ambae ni mama yake sheby"
Sasa huyu mwaju, anaijua vizuri familia ya General nyange....
"huyu kijana ni nani.... Hebu nenda ntakuita kwa wakati mwingine"
General alijikuta mawazo yakizidi kumpanda katika kichwa chake,...
"najua sio mtoto wangu, lakini kwanini awe na picha ya mke wangu katika simu yake??.... Huyu kijana kuna kazi imemleta kwa ajili yangu,.. Atakuwa hayupo kijeshi hapa kambini"
Mzee general alianza kuhisi kuwa sahi atakuwa hajaja kimafunzo japokuwa kaletwa kwa ajili ya mafunzo,...
Sasa mwaju alikuwa anakumbuka miaka ya nyuma kipindi akiwa na sheby,... Kumbe sheby na mwaju walikuwa ni wapenzi waliopendana sana, wakiwa hapo hapo kambini, lakini sheby alipofariki kwenye mazoezi ndipo kupenda kwake kukaishiaga hapo,... Mpaka leo hajapenda tena mtu wa aina yeyote, sasa anapomuona sahi anamfananisha na sheby mtoto wa General nyange, na wakati mtoto wa General alishakufaga kwa mlipuko wa bomu, katika mabomu ya kufanyia mazoezi kuna moja lilikuwa ni la kweli, hivyo alikufa..
Sasa huku kwa General alimwita mkubwa mwenzake ambae wanalingana vyeo kidogo tu, ila nyange ndio kuu la majeshi....
"me deo? Unajua huyu kijana mgeni toka aje yaani mimi sipati usingizi kabisa yani"
Aliongea mr nyange huku akitamani hata kulia, mana wakimpangia njia za kumuua, chuo kitaonekana kina matatizo, mana wanafunzi wanakufa tu, hivyo miaka inayokuja hakutokuwa na wanafunzi, na miaka kadhaa mbele kutakuwa hakuna jeshi, hivyo kumuua hawawezi kwa kubofia nchi kuingia hatarini kwa kukosa jeshi,...
"kwanza kabla ya yote mi naona ule mzigo tumkabidhi mwenyewe kwanza... Mana huyu kinana akiuona.. Itakuwa tabu"
"lakini deo, kwanza tumjue huyu kijana ni nani"
"wala haina haja sana bwana nyange,.. Huyu kijana ni mdogo sana kwetu, na wala hajatumwa huyu.. Sema sisi ni wasiwasi wetu tu"
"deo usichukulie jambo hili mzaha mzaha"
"sikiliza... Huyu mtoto ni wa kuwa nae karibu, kama umegundua ana uwezo basi ni wa kukaa nae karibu"
"ukae na hatari tena..."
"kwani una asilimia ngapi za kumhisi"
"aahhhh nyingi sana, tena na vile kamanda alivyoniambia kiwa ni mtaalamu wa kuruka ruka, ndio nahisi atakuwa mpelelezi huyu"
"hapana hisia zako tu... Sasa mpelelezi hawezi kuja jeshini... Sasa sikia ngoja tumuite"
General Deo alitoka nje na kumuita sahi, sahi bila kujua mipango ya mageneral hao alikuja na kuingia, lakini sasa ile anaingia tu ile saa ikawaka taa nyekundu kuashiria hapo ndani kuna kamera, sahi aliizima haraka haraka kabla hajashtukiwa na mageneral, sahi alipiga saluti kubwa kuwapa heshima yao kutokana na vyeo vyao
"kaa katika kiti"
Aliongea mr deogratias tena kwa kumbembeleza kwa utaratibu wa hali ya juu, na hawa nao ni mageneral wa zamani wanajua jinsi ya kumteka mtu,
"jana saa nane ulikuwa wapi"
Aliuliza mr nyange, huku sahi akiwa na wasiwasi sana, mana anajua jana hajaonekana kumbe kaonekana....
"nilikwenda msalani"
"msalani kwa masaa mangapi"
General anauliza maswali yale yale ya kumkamata, mana kapewa ifo zote kuhusu jambo la jana,.....
"nilikuwa nasumbuliwa na tumbo la kuendesha"
Mara mr deo akaingilia kati,...
"sikiliza kijana.... Jana tumeona ulichokifanya kule porini,... Sasa endepo hutokuwa na sisi, tunakutimua hapa jeshini... Na wala usitake kubisha, hana umeuwa watu wawili, na mmoja ndio huyo yupo hospitali hoi hoi.... Hii ni kesi"
Sasa sahi yeye alijua tu hapa anapelelezwa kichini chini...
"nilitokea wapi kwenda huko"
"tunakujua, na aliekuleta tunamjua wala usitake kutuumiza kichwa... Umeshajua sisi ni wauzaji wa silaha hapa jeshini... Sasa unachokifanya hakitokuseidia lolote.... Ungana nasi.. Yule mgonjwa katuambia kila kitu sema hatujataka kukudhalilisha mbele za watu pale paredi.... Yule mgonjwa kasema, ulikuwa umevaa saa kubwa,.. Afu hio saa inawaka taa... Hapa jeshini waliovaa saa ni walimu tu, sasa je? Wewe ni mwalimu"
Alipomaliza kuongea mr deo, mara mr nyange akatoa briefcase ya pesa na kuiweka mezani huku akisema
"kijana... Kabla ya yote... Kuna milioni 100 hii hapa... Yaani ukikubali tu, chukuwa hizo pesa"
Itaendelea........
Je? Sahi atakubali kujiunga na hao watu,... Mana sahi anamiliki Discate kasoro codes zake ndio hana.....
ITAENDELEA.....