Makapuku Forum

Makapuku Forum

Leo katika Historia


1934 - John Dillinger anauwawa.
Ni Jambazi maarufu aliyetikisa katika wizi wa kuvamia Benki huko Marekani. Pia alikuwa ni mahiri kwenye kutoroka jela.
Anachukuliwa kama mmoja kati ya wahalifu waliowahi kusumbua vyombo vya dola nchini Marekani.
e2b2a7628892db0d6660717d451658a4.jpg
ac5a17068aa7a3a3cfae69579d8a2af3.jpg
e16367145a5da672160f8e73aec42a05.jpg

Yeye pamoja na akina Pretty boy Floyd na Baby face Nelson waliisumbua sana Marekani
Ila Mkurugenzi wa FBI Edgar J Hoover akafanikiwa kuwatuliza kimyakimya mmoja baada ya mwingine
......
 
THE DOM

Sehemu Ya 2

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Instagram....

Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

SON OF PRESIDENT GU

"kwahio mkuu, wale vijana ni makomando wale"
"ndio... Wale ndio moja wa vikosi vyetu vya kikomando"
"aahhhh mbona ni wadhaifu kiasi kile"
"kwasababu mafunzo yako wewe ni ya hali ya juu, na ndio mana umewaona ni wadhaifu"
"Kiukweli hawaingii hata chembe katika mwili wangu"
"nalijua hilo.... "
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya kijana huyo na Mheshimiwa rais, na walionekana kujuana kuliko kawaida
"sasa, nataka ukapumzike... Lakini nataka utoe vitambulisho vyako vyote, vikiambatana na kadi zako za benki zoote, yaani kila kilichohusisha jina lako, naomba uviweke hapa mezani haraka sana, tena bila kufikiria"
Aliongea mheshimiwa raisi huku kijana huyo akitafuta vitu hivyo katika begi lake, pamoja na waleti,... Baada ya Dakika mbili alikamilisha agizo la raisi, aliweka kadi na vitambulisho vyake vyote,...Tukianza na Vitambulisho vyake.. KITAMBULISHO CHA MKAZI... KITAMBULISHO CHA MPIGA KURA... KITAMBULISHO CHA KITAIFA... KITAMBULISHO CHA JESHI... KITAMBULISHO CHA SHULE..... BILA KUSAHAU KITABU CHA KUSAFIRIA (PASPOT)..... Ikifuatiwa na kadi Za bank zifuatazo... CRDB BANK.... NMB BANK.... EQUTY BANK... KCB BANK... WESTERN UNION BANK... Vitu vilikuwa vingi mpaka rais akachoka.....
"haaaaa... Kijana hivi VITANZI vyote ni vyako??"
"Ndio."
"nakagua kimoja baada ya kingine, angalia usije ukawa jipu"

ENDELEA.........

Aliongea mheshimiwa rais huku aki vikusanya vitanzi (Vitambulisho Vya kitanzania) (VITANZI) hivyo wakati huo kijana hakuwa na wasiwasi hata kidogo kwasababu anakumbuka huyo ndiye aliemkatia vitanzi vyote hivyo, sasa iweje leo aje awe jipu,...
"vitanzi vyote ulinikatia wewe, sasa sijui kwanini umesahau"
Aliongea huyo kijana huku akiweka vitu vyake sawa baada ya kutoa vitanzi vyake vyote,..
"kwani ulifikiri nakumbuka? Ata sikumbuki mana ni toka nilipokuwa waziri wa ujenzi, mpaka leo siwezi kushindwa kusahau"
Aliongea mheshimiwa raisi, huku akiviweka vitanzi vile katika begi lake yeye rais,... Wakati huo kijana katulia tuli akisubiri mwongozo toka kwa raisi,.. Kuna kitu alibonyeza mheshimiwa rais pale pale kwenye meza kana kwamba anahitaji mtu aje hapo,.. Kweli alikuja askari wake na kumuamuru kuwa
"mpeleke katika nyumba yake"
Kijana alishangaa kuambiwa mpeleke katika nyumba yake, alitaka kuuliza lakini raisi alikunja sura kana kwamba alitakiwa kufata amri na sio jinsi alivyotaka,... Kijana alionekana kuwa na makazi tofauti na makazi ya serikali yaani kijana ana kwao lakini mheshimiwa hataki kusikia kijana akaishi kwao, na hapo ni aende akapumzike tu na mambo mengine kesho,... Kijana hakuwa na budi kwenda,
"alafu sikiliza hutakiwi kutoka mpaka kesho"
Aliongea mheshimiwa rais huku kijana akizidi kuingiza hofu juu ya swala hilo...
"kwanini mzee"
"nimeshasema hii ni amri na sio ombi"
Roho ilimuuma sema tu hakuwa na uwezo wa kutenda kitu tofauti na rais

Kijana alitolewa hapo kwa gari ya private, mana akitolewa na gari ya serikali, waandishi wanaweza kufuatilia ili kujua gari ya raisi au waziri inakwenda wapi,.. Na kitu kikubwa kijana huyu ni siri ya serikali haitakiwi mtu yeyote kufahamu uwepo wa kijana huyu, sasa hatujui ni kwanini ni siri kuwepo kwa mtu huyu,...
"sikiliza kijana, najua bado hujapewa mwongozo wa kazi, lakini wewe ni mpelelezi wa siri, wewe ni askari wa siri, yaani anaetakiwa kukujua wewe ni sisi watu wa karibu wa raisi, na ndio mana mheshimiwa rais hataki serikali yoye ijue uwepo wako na ndio mana ukapelekwa kusoma kisiri siri"
Aliongea askari aliokuwa anampeleka kijana huyo katika makazi yake,
"sawa, mimi Sikatai lakini sio mpaka makazi nichaguliwe pakukaa"
"weww tayari ni mfanyakazi wa serikali, hivyo lazima uwepo katika mazingira hayo"
Kijana hakuwa na la kuongea zaidi ya kufuata kile kinachotakiwa, kijana alipelekwa mtaa wa Ostarbay jijini Dar es Salaam, mtaa wa watu wa hali nzuri kiasi fulani,.. Alishangaa anaingizwa katika jumba moja la kifahari ambalo geti lake tu linafunguka kwa rimoti kontroo, maana yake hakukuwa hata na mlinzi wala mfanyakazi,...
"hapa ndio nyumbani kwako kuanzia leo,.. Kisheria kwa kazi yako haruhusiwi kuishi na mtu mwingine humu ndani, uwe wewe peke yako"
"yaani jumba lote hili niishi peke yangu"
"ndivyo inavyotakiwa, yaani hata mlinzi hatakiwi hapa"
Aliongea askari huku akimzungusha nje ya nyumba hio, na hio nyumba haijawahi kukaliwa na mtu toka imejengwa,
"alafu mbona kama hii nyumba haijawahi kuishi mtu"
"ni kweli, nyumba hii ilijengwa spesho kwa ajili yako, kwasababu mheshimiwa raisi anajua kazi yako hivyo kujenga nyumba hii kutokana na kazi yako ya upelelezi wa siri"
Kijana alizidi kuwa kimya,... Sasa kwenye milango, kila mlango una loku ya namba, yaani ukifika mlangoni kuna screen inakuangalia utie namba kisha mlango ufunguke,.. Nyumba nzima imezungukwa na kamera za siri yaani CCTV za siri, sio zile ukiingia tu umeziona hapana, hizo mpaka uzione yataka kutumia vyombo maalum vya kuangalia kamera kama zipo....
"hii nyumba imezungukwa na kamera kote, kuanzia ndani mpaka nje"
Aliongea askari, huku kijana akiangalia hio nyumba,...
"usiangalie kijana, huezi kuziona.. Ni kamera za siri"
Aliingea askari huku yule kijana akicheka sana
"nisikilize mzee,.. Mimi nimekwenda korea kwa masomo haya ya upelelezi, jeshi, na mapigano... Katika masomo ya upelelezi tumesomea kamera aina zote,... Kabla hujanionyesha hizo kamera, mimi ndio nakuonyesha hizo kamera"
Askari alishangaa sana kuona kijana anajua kila kitu
"hebu Nionyeshe hata tatu za hapa nje"
Aliongea askari huyo huku kijana akigeuka nyuma na kunyoosha kidole
"moja hii hapa"
Kiukweli kamera hizo bila vyombo maalum huezi kuona, lakini kijana huyo aliona..
Askari alitulia kimya huku akizidi kuonyeshwa kamera hizo,...

Basi baada ya mida kijana alibaki nyumbani hapo na uzuri zaidi kuna magari mapya hapo uwani, yaani mapaka magari kanunuliwa, sasa sijui huyu kijana ni nani zaidi ya upelelezi... Wakati huo askari keshaondoka hivyo kijana kubakia mwenyewe katika jumba hilo lenye ulinzi wa vyombo maalum na sio watu,.. Kijana alichukuwa begi lake na kutoa vitu vyake vya muhimu ana laptop maalum iliojaa systems za kamera na programu za upelelezi zaidi,.. Kwanza kabla ya yote aliisogelea kamera moja na kuitoa kisha kuna namba alizichukuwa katika kamera ile,... Alipomaliza aliirudishia mana ni kamera za kupachikwa tu katika sehemu za siri sana, yaani ni kadogo kama zile earphones ndogo za masikio,.. Alipochukuwa namba katika moja ya kamera, aliingiza katika mtambo wake wa kompyuta kisha akazisachi,.. Ghafla katika screen ikamwonyesha jumba zima hilo analo ishi kwa sasa.. Ghafla akazizima kamera zote,... Yaani uwezo aliokuwa nao huyu kijana sio wa kuigwa, yaani ukiiga hapa umeumia, elimu imekaa hapo, anacheza na kompyuta hata mzungu mjinga... Yaani utafikiri kuitengeneza yeye kumbe yeye ni mtumiaji tu,..
Mara simu ikaita kucheki ni Mheshimiwa rais
"haloo mzee"
"kuna nini huko"
"wapi"
"naona kamera zimezima"
Sasa kijana ndio anashangaa, ina maana systems nzima ya kamera hizo kumbe zimeunganishwa katika screen ya raisi, hivyo jengo hilo linaonekana na rais...
"kuna waya niliugusa hapa hebu ngoja niuunganishe"
Alidanganya, kisha akabonyeza mitambo yake kamera zikaendelea kufanya kazi,...
"hapo vp"
"acha hapo hapo usiziguse, afu pumzika kesho uje tukupe fomula nzima ya kazi"
"sawa"

Lakini kijana huyo naye ana familia lakini sasa haijulikani ni familia gani, sasa sijui kama huyu ndio mtoto wa raisi au vp,.... Kijana alitoa picha ya mwanamke mmoja hivi alionekana kumpenda sana mwanamke huyo, ila hatujui ni nani yake, mana ni mama mtu mzima, na sio mschana, inaashiria ni mama yake.... Mana aliikumbatia picha hio huku akisema
"I love my mom"
Aliongea huku akilia kiume, ilionekana mama yake amefariki dunia...

Kesho yake akiwa yupo njiani kuelekea Ikulu, kwa ajili ya kupewa kazi yake, wakati huo alikuwa akiendesha gari yenye preti Namba ya usalama wa taifa, yaani ni ya serikali...
Maramoja kijana alifika Ikulu na kuingia mpaka ndani,... Alimkuta waziri mkuu, pamoja na makamu wa rais, huku mlinzi wa rais akiwepo nyuma ya raisi, maana yake walikuwa watu wanne na kijana huyo alikuwa mtu wa tano,...
"shkamoni"
Alisalimia viongozi wote aliowakuta hapo lakini kabla hajakaa, alishangaa vitanzi vyake kumwagwa mezani,.. Lakini kumwagwa kwa vitanzi hivyo sio kitu, kitu ni kwamba vitanzi hivyo vilimshangaza sana kijana huyo, hivyo alishikwa na shauku ya kuuliza
"kwanini imekuwa hivi"
Aliuliza kijana, ambae mpaka sasa hatujalijua jina lake,.... Na hapa ndipo tutakapo lijua jina lake rasmi na kazi yake, bila kujua yeye ni nani na alikuwa nani hapa nchini.....

Je? Huyu kijana ni nani... Na ni mtoto wa nani??... Na kwanini anaishi kwa siri hapa nchini???

ITAENDELEA.....
 
ha hahahahaha, hiki kicheko nimeandika mimi, maneno yanayofuata sijaandika mimi na huna haja ya kudhani nimeandika mimi maana naongelea uzoefu sijafanya utafiti

ukiwa na kitambi unakuwa kit.ombi sana, utafiti ni wa anko wangu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Leo katika Historia

1992 - Pablo Escobar anafanikiwa kutoroka gerezani huko Medellin nchini Colombia.
Ni mmoja kati ya wafanyabiashara hatari na tajiri wa Madawa ya Kulevya kuwahi kutokea katika uso wa Dunia. Enzi hizi pia alikuwa akitamba yeye pamoja na mwanamama Griselda Blanco, Marekani inawatambua vyema watu hawa
Alikuwa na utajiri wa kutosha lakini hakuwahi kutambuliwa kwenye orodha ya matajiri wa dunia kwa kuwa vyanzo vya mapato yake ni biashara haramu.
58858de7fad8c330368732abe5f2cb01.jpg
70700f29113efc9ad26fa9bdc5165854.jpg

Alifariki 1993 akiwa na miaka 44
.....
 
Back
Top Bottom