Makapuku Forum

Makapuku Forum

7cdbc9841a56436feaf2c0d39005d45a.jpg
 
Kawaida misitu ndo husababisha mvua sasa huko utasikia Amazon rain forest
Kama ulivyoona picha ule uoto ndo tuseme misitu ya Amazon yaani mto kama kawaida hukatiza porini
Hivyo kuna misitu ya Amazon na kuna mto Amazon ndo wanapoishi Anaconda nafikiri ushawahi kuiona ile muvi na ukaona huo msitu na mto
782df56f368b9e7ac4e66071d11235f8.jpg

Walicheza hiyo muvi Jeniffer Lopez na Ice Cube
Mssitu na mto vyote vipo Brazil
.......
Asante mkuu bitoz kwa ufafanuzi

 
Muziki: J3 kuelekea J4

Ni usiku mwingine tukielekea kuikamilisha Jumatatu, kapuku mheshimika ninakusalimia nikiamini siku ya leo ilikuwa nzuri sana na Jumatatu ilikuwa nzuri ukijipanga kuitafuta Jumanne siku ambayo ni ile ile kama J3 sema tarehe tu ndo zinabadilika na ukitizama kalenda yako hakuna kinachofanana na jana utakiona.

Ukijaribu kuzitizama hizi siku kikamilifu utagundua kabisa kuwa kadiri zinavyokwenda ndivyo wewe binafsi unazidi kubadilika, kiumbo hadi kiakili, unaanza kuitazama kesho na kuhakikisha kuwa kesho kutwa haikukuti ukiwa kama leo. Tutiane shime tuweze kufanikisha kila ndoto zetu halali tunazowaza.

Leo humu jukwaani kulikuwa poa sana, shukrani kwa Sakayo na Transcend kwa kutuchangamsha na kutuaminsiha kuwa migogoro ndo hutufanya tuwe thabiti katika kuhusiana kwetu, you guys are great pipo. Pole kwa BH kwa kusumbuliwa na miguu, atapona ana atarudi kuungana nasi tena hapa, salamu zimfikie.

Muziki sasa, unajua sisi hapa Mtwara naamini ni tofauti sana na wakazi wa mikoa mingine linapokuja suala la movies, huku sisi ni wapenzi wa'nachi' yaani Indian movies toka Bollywood, huku utakutana na kian Mithun Chakarabot, Govinda (sic) na kina nani sijui. Na hata tunapocheza soka, ukipigwa tobo (doba) basi kila mtu atashangilia. Bhaaa, ndo hivyo njomba, kunywa nipa na samaki nchanga mbona shega tu bwana wewe

Burudika muda huu tukijiandaa kusikiza chaguo la wasikilizaji

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom