Obe
Platinum Member
- Dec 31, 2007
- 10,278
- 35,639
ZABURI 20
1.Mwenyezi MUNGU akujibu uwapo taabuni;jina la MUNGU wa Yakobo likulinde.
2.Akupelekee msaada kutoka hekaluni mwake;kutegemeze kutoka mlima Siyoni.
3.Azikumbuke sadaka zako zote;azikubali dhabihu zako za kuteketezwa .
4.Akujalie unayotamani moyoni mwako,aifanikishe mipango yako yote .
5.Tutashangilia kwa ajili ya ushindi wako ;tutatatweka bendera tukilitukuza jina la Mungu wetu ,Mwenyezi -Mungu akutimizie maombi yako yote!
MUNGU BABA WA MBINGUNI asante kwa siku ya leo,tunaomba toba kwa yote tuliyokosea kwa mawazo,maneno,matendo uturehemu twakusihi usiku huu tunajikabidhi mikononi mwako ituzingire,damu takatifu ya Yesu Kristo itufunike na inene mema,malaika walinzi wazunguke nyumba zetu na vitanda vyetu watulinde na kutuangalia usiku kucha watuepushe na mabaya yote,hila na uovu wa shetani,na BABA tunaomba utuamshe asubuhi salama.
Asante BABA maana utatenda sawa na mapenzi yako katika jina la Yesu Kristo Amen.
USIKU MWEMA MBARIKIWE![]()
![]()
Asante kwa sala BH
Usiku mwema kwako. Njozi njema
ZABURI 20
MUNGU BABA WA MBINGUNI asante kwa siku ya leo,tunaomba toba kwa yote tuliyokosea kwa mawazo,maneno,matendo uturehemu twakusihi usiku huu tunajikabidhi mikononi mwako ituzingire,damu takatifu ya Yesu Kristo itufunike na inene mema,malaika walinzi wazunguke nyumba zetu na vitanda vyetu watulinde na kutuangalia usiku kucha watuepushe na mabaya yote,hila na uovu wa shetani,na BABA tunaomba utuamshe asubuhi salama.
sema bh yupo kigamboni sijui inabidi tumfate huko tukakutane nae mitaa ya huko si unajua kigamboni kumetulia sehemu nyingi beach nyingi