Makapuku Forum

Makapuku Forum

Jumapili: HKL

Ni Jumapili na inaishiria. Wote naamini mmekuwa na siku nzuri, wa kwenda kanisani, safi. Wenye Eid leo, hongera na ambao bado hatujauona mwezi, tuendelee, mufti kasema kesho mambo yanajipa, inshAllah.

Jumapili huhitaji makeke mengi, ni siku inayokuandaa na wiki nyingine ya kazi na michakato inayokupa maana ya kuishi. Unaikumbuka kazi ni Uhai? Hii ilikuwa ni moja ya 'motto' kama ilivyokuwa kilimo kwanza, siasa ni kilimo, elimu kwa wote na sasa hapa kazi tu.

Anaitwa Fally Ipupa, mwanamuziki muimbaji na mpiga gitaa kama ulikuwa hujui. keshafanya kazi ya kuimba na kupiga gitaa kwenye bendi ya Koffi Olomide- papa Mopao. Ana tuzo kibao za MTV na keshafanya wimbo na Olivia wa kundi la kina Big Poppa USA.

Sikupanga kukicheza leo kibao hiki nikiamini kimekaa kimikatiko, I was totally wrong, huu muziki wake kama ulivyodhaminiwa na Shunie umenifanya niingie chimbo kumsaka na kumwangalia zaidi. Maana nilizoea tu kile kibao chake cha Bakanja shika mu mbele🙂.

Hapa mwangalie katika clip hii ya YouTube akiimba kiulaini yaani hata umepanda bodaboda (siku hizi zina muziki wa subwufa- asante mchina) bila kuvaa helmet utaufurahia. Japo sijamwelewa hizo alizojifutika kiunoni ni shanga au nini, amua mwenyewe, usisumbuke kuhesabu yupo shululu atatoa tathmini (joke)

Asante mdhamini (ukumbuke tu kuniwekea dhamani kuleeeee) Shunie. Tuwe na wiki njema Makapuku wote, wafanyakazi kw wanafunzi. Yote tuliyopanga kwa wiki hii mpya angalau yafanikiwe.

Kabla sijasahau, nakukaibisha Eid hapo kesho: Eid Mubarak





HKL- Hii Kitu Laini ----(muziki laini leo)😵
 
Bora umekuja anko, unadhani nisingeuchuna ule msala ningeumalizaje? Yaani full majanga, sikukuu siku mbili huyu chimumuna huyu Shia. Ndo utajua haikuwa rahisi.

Umesharudi?
Binamu sio fair kabisa au ndo kale ka kauli kako ka kuniamini nusu ...ujue ukiyakorogaa mm ndo unanipa kaziii...na ujui kule nimekutana na naniii.m

Kurudii nimerudii ilaa shughuli ilikuwa pevuuu
 
Binamu sio fair kabisa au ndo kale ka kauli kako ka kuniamini nusu ...ujue ukiyakorogaa mm ndo unanipa kaziii...na ujui kule nimekutana na naniii.m

Kurudii nimerudii ilaa shughuli ilikuwa pevuuu


...wwe mwenyewe unaniamini robo bora mimi nakuamini nusu na robo. Vipi umekutana na nini? Ila najua yule hana makeke, yaani siku ile amekuomba umnunulie dela la sikukuu nikasema hollymolly yaani rahisi sana. Ila yule mwingine sasa, komesha ngenge, ulimununulia lile wig-zag
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom