Makapuku Forum

Makapuku Forum

Jumapili: HKL

Ni Jumapili na inaishiria. Wote naamini mmekuwa na siku nzuri, wa kwenda kanisani, safi. Wenye Eid leo, hongera na ambao bado hatujauona mwezi, tuendelee, mufti kasema kesho mambo yanajipa, inshAllah.

Jumapili huhitaji makeke mengi, ni siku inayokuandaa na wiki nyingine ya kazi na michakato inayokupa maana ya kuishi. Unaikumbuka kazi ni Uhai? Hii ilikuwa ni moja ya 'motto' kama ilivyokuwa kilimo kwanza, siasa ni kilimo, elimu kwa wote na sasa hapa kazi tu.

Anaitwa Fally Ipupa, mwanamuziki muimbaji na mpiga gitaa kama ulikuwa hujui. keshafanya kazi ya kuimba na kupiga gitaa kwenye bendi ya Koffi Olomide- papa Mopao. Ana tuzo kibao za MTV na keshafanya wimbo na Olivia wa kundi la kina Big Poppa USA.

Sikupanga kukicheza leo kibao hiki nikiamini kimekaa kimikatiko, I was totally wrong, huu muziki wake kama ulivyodhaminiwa na Shunie umenifanya niingie chimbo kumsaka na kumwangalia zaidi. Maana nilizoea tu kile kibao chake cha Bakanja shika mu mbele🙂.

Hapa mwangalie katika clip hii ya YouTube akiimba kiulaini yaani hata umepanda bodaboda (siku hizi zina muziki wa subwufa- asante mchina) bila kuvaa helmet utaufurahia. Japo sijamwelewa hizo alizojifutika kiunoni ni shanga au nini, amua mwenyewe, usisumbuke kuhesabu yupo shululu atatoa tathmini (joke)

Asante mdhamini (ukumbuke tu kuniwekea dhamani kuleeeee) Shunie. Tuwe na wiki njema Makapuku wote, wafanyakazi kw wanafunzi. Yote tuliyopanga kwa wiki hii mpya angalau yafanikiwe.

Kabla sijasahau, nakukaibisha Eid hapo kesho: Eid Mubarak





HKL- Hii Kitu Laini ----(muziki laini leo)😵

Binamuuuuuuuu
Asante sana umeufanya usiku wangu kuwa mzuri naipenda sana hii nyimbo acha nikupe mauwa binamu yangu mimi

 
17f92f109ab06b0a9b5a4e0f8250a2cf.jpg
cea47ee76fd0ab70983534ed1c65de51.jpg

Ipupa & Olivia
......
Ni couple hao?!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom