Makapuku Forum

Makapuku Forum

Asante sana T wa Sakayo kwa nukuu,hili jambo ni kitendawili...nimewahi kushiriki miradi wa kurudisha mabinti mashuleni,kuwajengea uwezo wamama wadogo kujitegemea ,kuwashauri mabinti kutoshiriki ngono kabla ya wakati(wamalize masomo kwanza) katika ngazi ya kaya,jamii,kanisa nk

Hawa watoto wengi huwa hawapati ujauzito kwa kukusudia,au starehe au mpango maalumu...hutokea tu kama kufumba na kufumbua ..na nakuhakikishia viongozi wengi ni wahanga wa hii changamoto wao wenyewe au wanafamilia...si jambo jema lakini likitokea ni muhimu kuwasaidia hawa watoto sio kuwa tenga...na mara nyingi walifanya vizuri kimasomo na kimaisha ...sina uhakika sana nini kitatokea kuanzia sasa...tumuombe Mungu atupe ufunuo katika hili.Ila mimi msimamo wangu hili likitokea katika familia yangu ATASOMA TU KWA GHARAMA YOYOTE.NITAOKOTA HATA CHUPA,VYUMA CHAKAVU,VIBARUA,NIPATE KIPATO NIMPELEKE SHULE
barikiwa kwa mamneno kuntu mamaa
 
ZABURI 37

5.Mkabidhi Mwenyezi -Mungu maisha yako;mtumainie yeye naye atafanya kitu.

BABA Mwema tunakuja mbele yako mchana huu tukikushukuru kwa yote unayotenda,asante kwasababu unatupenda tunaomba endelea kutuimarisha tuendelee kukutumainia wewe tu maana utafanya kitu,utatuponya,utatupa riziki,utatupa upendo,utatupa ajira na mahitaji yetu sawa na mapenzi yako.asante kwa sababu ya mahali hapa MAKAPUKU pamekua sehemu yetu njema na tunajifunza na kushirikiana kwa upendo endelea kutusimamia mfalme wa amani maana utatupa kushinda.
Waangalie kwa wema wanaopitia changamoto mbalimbali wape matumaini na ufumbuzi wa kila jambo.
Tunomba yote katika jina la Yesu Amen

MCHANA MWEMA MBARIKIWE SANA
 
Santorini island, Greece
ed3bbaf7277f6f624f448c3ff13231f0.jpg
Pazuri sanaaa
 
barikiwa kwa mamneno kuntu mamaa
Yaani inaumiza ,hayo tunaambiwa walala hoi watoto wao yakiwakuta wanawapeleka ulaya,india,malasia,kenya,uganda ...nk wanasoma vizuri....wengine mimba wanapewa na haohao wakubwa na hata hawashitakiwi...nikisema hv nimeona na kusikia mengi..Mungu atusaidie tu kuwasimamia watoto na vizazi vyetu ndio zawadi pekee Mungu aliyotupa hatuna utajiri mngine,tuwaleee katika maadili ikitokea tuwasaidie tu wasonge mbele
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom