Daaaaah Udongo unameza ....R.I.P Ally wa Yanga ...
............Huyu mwanadamu alikuwa ni star katika mastar wanaoishi jukwaani katika kila mchezo wa Yanga na wa Taifa stars, huyu mwanadamu kila wakati alivutia kwa ubunifu wake jukwaani...... Nani alikuwa hamfahamu mwana Sanaa huyu, Nani alikuwa hamfurahii mwanadamu huyu...... Sio Mimi tu, sio wewe tu, hata camera za runinga zilimfurahia kila timu yake ilipokuwa inashangilia goli..... Alivutia wakati wa kushangilia goli kwa staili ya kuchinja lakini pia alivutia zaidi wakati ana kuhuzunika baada ya kufungwa.
Nenda sasa ukapumzike Ally Yanga, picha zako ni ushahidi tosha wa ufalme wako jukwaani kwa jezi za Yanga na taifa stars katika Sanaa yako. Mwenyezi Mungu aipe faraja familia yako katika kipindi hichi kigumu, lakini pia Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi AMEN.
Tangulia hiyo ndio njia yetu sote. Inalilah waina ilaih rajiun