Makapuku Forum

Makapuku Forum

UJUMBE MUHIMU KWA WANAUME WOTE.

Katika maisha mwanaume inakupasa kufahamu mambo ya msingi yatakayo fanya maisha yako yawe ya furaha, mambo hayo ni pamoja na:

1. Oa mwanamke ambae unaweza KUSALI nae na sio kwa sababu anajua KUFANYA MAPENZI vema.

2. Mwanaume bora KAMWE hapimwi kwa idadi ya wanawake alionao au aliotembea nao BALI kwa idadi ya wanawake aliowaambia "Mimi ni mume wa mtu" au ninae mtu tayari.

3. Kuna aina ya wanawake unatakiwa kuwaepuka kabisa kwa gharama yoyote ile, "wanawake wamaodhani uzuri wao ndio bora zaidi kuliko tabia zao"

4. Kila mwanamke anavutia akivaa nguo fupi inayoonesha maungo yake wazi, ila kama utakuta mwanamke amevaa nguo ndefu au za kusitiri mwili wake na bado anavutia, huyu ni dhahabu! Anathamini mali za mumewe!

5. Kamwe usimpe mwanamke mimba ya mtoto kabla hujampa mimba ya malengo na ukayatimiza.

6. Tafuta mwanamke ambae atakupa changamoto za maisha na kuongeza uwezo wako wa kufikiri na sio mwanamke wa kila kitu Ndio mzee!

7. Wanawake wakamilifu hawapatikani popote duniani, ila wanawake bora wapo kila mahali.

8. Mwanamke anaweza kukusaliti, ila Mungu hawezi kukusaliti, hivyo basi kabla hujapata mwanamke Mpate Mungu kwanza. Kuna raha sana kuwa ndani ya Mungu asikwambie mtu!

9. Kama unajijua umefikisha miaka 25 na kuendelea epuka mambo ya kivulana, kuvaa suruali katikati ya makalio, kuvaa hereni, kubadili badili wanawake kama unachambua mitumba ya karume etc

10. Usitumie kichwa chako kunyoa kiduku, tumia kichwa chako kuwaza mambo yenye tija ikiwemo kutafuta pesa na kuongeza hazina yako ya baadae.
Well said.
 
Daaaaah Udongo unameza ....R.I.P Ally wa Yanga ...

............Huyu mwanadamu alikuwa ni star katika mastar wanaoishi jukwaani katika kila mchezo wa Yanga na wa Taifa stars, huyu mwanadamu kila wakati alivutia kwa ubunifu wake jukwaani...... Nani alikuwa hamfahamu mwana Sanaa huyu, Nani alikuwa hamfurahii mwanadamu huyu...... Sio Mimi tu, sio wewe tu, hata camera za runinga zilimfurahia kila timu yake ilipokuwa inashangilia goli..... Alivutia wakati wa kushangilia goli kwa staili ya kuchinja lakini pia alivutia zaidi wakati ana kuhuzunika baada ya kufungwa.

Nenda sasa ukapumzike Ally Yanga, picha zako ni ushahidi tosha wa ufalme wako jukwaani kwa jezi za Yanga na taifa stars katika Sanaa yako. Mwenyezi Mungu aipe faraja familia yako katika kipindi hichi kigumu, lakini pia Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi AMEN.

Tangulia hiyo ndio njia yetu sote. Inalilah waina ilaih rajiun
3d6b3785868030421c0145c7927aff93.jpg
986adcbf8aec43c85791a7b5fd8f0a29.jpg
dfb77c8e37540d03e7ea9e287de5f3dd.jpg
6cb1759f74097ae84708cd44b6505f39.jpg
9391c59db6ad4121672b2c7b63b86523.jpg

Picha zinasisimua
RIP mwanajangwani mwenzetu
.
.
.
Juzijuzi tu Simba wamempoteza shabiki wao wa kike kwenye ajali ya Jonas Mkude
So sad
.......
 
ZABURI 34

1.Nitamtukuza Mwenyezi- Mungu nyakati zote,sitaacha kamwe kuzitamka sifa zake.

2.Mimi nitaona fahari juu ya Mwenyezi -Mungu wanyonge wasikie na kufurahi.

3.Mtukuzeni Mwenyezi - Mungu pamoja nami,sote pamoja tulisifu jina lake

4.Nilimuomba Mwenyezi-Mungu naye akanijibu ,na kuniondoa katika hofu zangu zote.

5.Mgeukieni Mungu mpate kufurahi ,nanyi hamtaaibishwa kamwe.

BABA Asante kwa kutuamsha salama,tunakushukuru sana kwani wapo wengi walitamani kuiona siku ya leo hawajaweza ,hatuna cha kukulipa bali kukushukuru,kukutukuza,kukuheshimu na kulisifu jina lako Takatifu daima.
Siku ya leo BABA tunakuomba tuponye,tufariji,tuongoze,tusaidie kukupenda wewe zaidi na zaidi,tuwapende wenzetu,tuwainue,tuwafariji tuseme nao kwa upendo,tufanye kazi kwa bidii na kukushukuru kwa kila jambo maana wastahili sifa Mfalme wa Amani.

Bariki kila kinachoendelea mahali hapa tukifanye kwa utukufu wa jina lako takatifu,mbariki kila KAPUKU mahali hapa auone ukuu wako na asipungukiwe Upendo,Amani,Mshikamano, Busara,Hekima na Maarifa maana umetuweka pamoja BABA na unalo kusudi nasi TUNAKUSHUKURU,Ondoa hofu kwa kila mmoja wetu BABA mwema.

ASANTE maana utatutendea sawa na mapenzi yako,Ondoa vikwazo na changamoto zinazoweza kutuweka mbali nawe.

Katika jina la YESU mpatanishi na mwokozi wetu Amen.

MUWE NA SIKU NJEMA WAPENDWA WANGU MBARIKIWE
Ameeeeeeiiiiiiniiiii mama mchuchu
 
Asante na iwe njema kwako pia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom