Makapuku Forum

Makapuku Forum

928020d0c08c4ab1901b368867a5395e.jpg
I see
 
Leo katika dondoo za bbc ...


Mkazo umewekwa kwa nchi zinazowahifadhi wakimbizi kuangalia namna ya kuwahushisha wakimbizi kushiriki katika shughuli mbali mbali za kiuchumi.

Askari kumi na watatu wa Sudani Kusini wanaotuhumiwa kumuua mwandishi habari mmoja na kuwabaka wafanyakazi watano wa kigeni wa kusambaza misaada ya kibinaadamu, July mwaka jana, wamekana tuhuma zinazowakabili.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya wakimbizi elfu moja na miatatu wamezama katika bahari ya Mediterranean wakiwa katika harakati za kutaka kufika barani ulaya kwa mwaka huu pekee.
Miongoni mwa wakimbizi hao wenye ndoto za kupata maisha mazuri barani ulaya ni wenye uraia wa Somalia.

Kumezuka mgongano kuhusu benki ya A-Kusini inavyo endesha kazi zake
huku ikishutumiwa kuwa inajali zaidi maslahi ya raia wa A-Kusini kuliko kuangalia kupanda na
kushuka kwa sarafu ya A-Kusini.

Matayarisho ya mkutano kuhusiana na wakimbizi mjini Kampala yako mbioni.Waziri wa Uganda anayehusika na wakimbizi anasema lengo la mkutano huo ni kukusanya pesa zitakazoiwezesha serikali yake kuhudumia vema wakimbizi walioko nchini humo
WAPUMZIKE KWA AMANI WKIMBIZI WALIOZAMA NA KUPOTEZA MAISHA.

Suala la ukimbizi ni gumu kuisha mpaka mfumo wa maisha na usalama wa nchi za kiafrika urekebishwe...hao ni wale wanaoondoka kwa kujifichaficha ,nchi zetu pia zina watu wengi wameondoka kwa majina ya kwenda kusoma,kutembelea ndugu,kutibiwa lakini ukichunguza ni ukimbizi.

Hao wanaotajwa wauaji na wabakaji kwakweli wachunguzwe haraka na hatua za kisheria zichukuliwe ,naamini vithibitisho vipo,vifo na hao waliobakwa.

Lee wa Shunie asante sana kwa HADITHI,BBC ,UF NA BARAKA UBARIKIWE SANA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom