Makapuku Forum

Makapuku Forum

Jamani habari za asubuhi,,, MSAADA jamani maisha mgumu baada ya kumaliza CHUO cha nursing. Nikaa tu cjaajiliwa ujuzi wangu utapotea nisaidieni. Nafasi ya ajira jamani hata ya kuuza duka LA madawa au kituo cha Afya ,,cha serikari au binafsi..... Kwa mawasiliano nicheki APA ..nipo tayari mda wowote.
Ongera sana kwa kumaliza chuo ila ushauri wangu unaweza kuufata au ukasoma ukapotezea

Vijana wengi mnamaliza chuo mkiwa na matumaini ya kuajiriwa moja kwa moja hasa kwenye professionals zenu ni jambo zuri na ni baya pia ...make kiakili hujipambanui na uhalisia wa maisha ...maisha ya chuo ni maisha mazuri ila ni maisha yanayodanganya wengi na pale mnapoagana kila mtu akaenda kivyake muhimu kwa sasa mtabaki kujuliana hali kwenye magroup yenu ya whatsapp ...

Yawezekana wewe uko interested sana na ulichokisomea bhasi fanya hivi kuna kitu muhimu siku hizi vijana mnakikwepa ila ni suluhisho ...KUJITOLEA KATIKA ENEO HUSIKA ...mfano nenda kituo unachopenda we omba kutolea ata usafi mle ndani na kusaidia saidia kazi ndogondogo utaona mwisho wake ...hapa usiwaze pesa kwanza

mimi mfano ninao hai kipindi najifunza umakanika enzi zile niliteseka ila mpaka sasa ni fundi mzuri usiulize fundi wa nini na nakumbuka mdogo wangu alitaka kufanya kazi saloon nikamshauri awe anashinda saloon na kukubali kutumwa na kufagia kwa sasa anamiliki barber shop kubwa mjini

Kupanga ni kichagua mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom