Muziki: Tufurahi na Weekend
Muda mwingine tena Makapuku, na kama kawaida segement hii hukujia mara tu baada ya top 10 za Bitoz. Najua kabisa Ijumaa inaenda vizuri na sasa unajirejesha nyumbani au upo tayari ukijipanga nini ufanye weekend hii. Napenda ufahamu tu kuwa hakuna jambo zuri na lenye afya kama kutumia weekend ukiwa na familia. Kwa sasa niko bar yaani kama padri kanisani au shehe msikitini, hatutofautiani mimi, wewe na wao.
Furahiday sio ya maneno mengi sana, nikija kwako na maneno mengi jua kuwa nataka kukupiga mzinga/mkopo, kitu ambacho si kibaya.
Leo tuangalie reggae kidogo, ni kukumbushana tu mana muziki huu unaujua hata kabla siajuelezea. Hapo tayari ushafikira kina Bob Marley na wenzake, ushaangalia picha yangu na mawazo yako yashakupeleka kwenye kuhusisha reggae na bange. Pole sana.
Tunaangalia reggae laini 'riddim au rhythm' na tunamkuta jamaa anaitwa Eric Donaldson. Huyu ndiye mwimbaji wa kwanza kabisa wa wimbo uliowapa umaarufu UB40 Cherry oh Baby. na kwao Jamaica ana sifa zake nzuri tu zinazomfanya awe kati ya wanamuziki wenye kueleweka na jamii kubwa.
Mimi reggae sio kivile sana huku unavuta jani, yes, kuna tofauti kubwa sana kati ya jani na cocaine, ya pili haijawahi kumwacha mtu salama.
Kupunguza maneno nakuwekea vibao vyote kwa pamoja.na nimezitoa YouTube
Tuwe na weekend njema
Na hapa ni Eric akifanya yake (hii ni video mfu)