Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Tufurahi na Weekend

Muda mwingine tena Makapuku, na kama kawaida segement hii hukujia mara tu baada ya top 10 za Bitoz. Najua kabisa Ijumaa inaenda vizuri na sasa unajirejesha nyumbani au upo tayari ukijipanga nini ufanye weekend hii. Napenda ufahamu tu kuwa hakuna jambo zuri na lenye afya kama kutumia weekend ukiwa na familia. Kwa sasa niko bar yaani kama padri kanisani au shehe msikitini, hatutofautiani mimi, wewe na wao.

Furahiday sio ya maneno mengi sana, nikija kwako na maneno mengi jua kuwa nataka kukupiga mzinga/mkopo, kitu ambacho si kibaya.

Leo tuangalie reggae kidogo, ni kukumbushana tu mana muziki huu unaujua hata kabla siajuelezea. Hapo tayari ushafikira kina Bob Marley na wenzake, ushaangalia picha yangu na mawazo yako yashakupeleka kwenye kuhusisha reggae na bange. Pole sana.

Tunaangalia reggae laini 'riddim au rhythm' na tunamkuta jamaa anaitwa Eric Donaldson. Huyu ndiye mwimbaji wa kwanza kabisa wa wimbo uliowapa umaarufu UB40 Cherry oh Baby. na kwao Jamaica ana sifa zake nzuri tu zinazomfanya awe kati ya wanamuziki wenye kueleweka na jamii kubwa.

Mimi reggae sio kivile sana huku unavuta jani, yes, kuna tofauti kubwa sana kati ya jani na cocaine, ya pili haijawahi kumwacha mtu salama.

Kupunguza maneno nakuwekea vibao vyote kwa pamoja.na nimezitoa YouTube

Tuwe na weekend njema

Na hapa ni Eric akifanya yake (hii ni video mfu)
 
Makapuku.!Humu ndani kuna utani fulani hivi amazing.
Kuna groups wanataniana saanaa na hakuna ubaya.
Makapuku wengine wakijaribu kutania baadhi ya pairs au couples salalee.
Tafsiri ya makapuku ni watu wenye mtazamo mmoja mwelekeo mmoja na malengo yaliyo sawa.
Sasa daah! Mkwara unakuwa mzito sana.
Makapuku ni stress free zone. Pole mliokwazika na utani wangu.
Mkuu hakuna tatizo wala..

Kila mtu anaheshimiwa kaka..

Lakini kuna utani mwingine ni mbaya.

Huwezi kuja kimtukana mtu wakati humjui wala hujui yeye ni nani..

So far wengi humu tunafaamina maisha ya nje ya jf...sasa kama mtu analeta matusi humu sio ustaarabu wala sio heshima..

Otherwise kaa makapuku ujifunze humu watu wanaishi vipi..

Karibu mkuu.
 
Nimkubali mara ya ngapi...

Nilikuona mstaarabu saaana kumbe ilikuwa gia tuu..

Tuliyamaliza muda sanaaa, halafu wanaume kugombana na kupeana mipasho sio mpango!!!!

Kawaida ya Wanaume ni kukubaliana tuu, mipasho waachie wanawake tena wenye akili finyu
Mimi ni mtu mstaarabu sana kwa watu wastaarabu mrembo Sakayo.

Angekuja kistaarabu ningemuelewa siyo kuleta mambo mengine ambayo siyo.

Kama vipi mwambie awe anatembea akiwa amekubeba mgongoni ili usitongozwe Mrembo.
 
Makapuku.!Humu ndani kuna utani fulani hivi amazing.
Kuna groups wanataniana saanaa na hakuna ubaya.
Makapuku wengine wakijaribu kutania baadhi ya pairs au couples salalee.
Tafsiri ya makapuku ni watu wenye mtazamo mmoja mwelekeo mmoja na malengo yaliyo sawa.
Sasa daah! Mkwara unakuwa mzito sana.
Makapuku ni stress free zone. Pole mliokwazika na utani wangu.
Jishike usianguke

Wanasemaga haina ushee
 
1/Princess Lalla SALMA
3859835bdd009cad6a9454a4d576c63c.jpg
fafc4e3170f7e5bfc1a22648c9734493.jpg

Ana umri wa miaka 39
Ndiye mke wa King Mohammed VI wa Moroko mwenye umri wa miaka 54
Ndiye Mfalme bishoo aliyekuja bongo mwaka jana akiwa na mapozi na macho ya kurembua kiasi watu kumsimanga kwamba ni shoga ila Sizonje alilamba misaada
.
.
.
.
Shukrani kwa mliosapoti mada
Tukutane Jumatatu
Mwisho
......
 
Nimkubali mara ya ngapi...

Nilikuona mstaarabu saaana kumbe ilikuwa gia tuu..

Tuliyamaliza muda sanaaa, halafu wanaume kugombana na kupeana mipasho sio mpango!!!!

Kawaida ya Wanaume ni kukubaliana tuu, mipasho waachie wanawake tena wenye akili finyu
Just ignore the guy. Don't answer. Don't like. Nothing. Atachoka na kwenda zake japo kutongoza ni haki yake lakini naona ameanza ugomvi ugomvi...
 
Muziki: Tufurahi na Weekend

Muda mwingine tena Makapuku, na kama kawaida segement hii hukujia mara tu baada ya top 10 za Bitoz. Najua kabisa Ijumaa inaenda vizuri na sasa unajirejesha nyumbani au upo tayari ukijipanga nini ufanye weekend hii. Napenda ufahamu tu kuwa hakuna jambo zuri na lenye afya kama kutumia weekend ukiwa na familia. Kwa sasa niko bar yaani kama padri kanisani au shehe msikitini, hatutofautiani mimi, wewe na wao.

Furahiday sio ya maneno mengi sana, nikija kwako na maneno mengi jua kuwa nataka kukupiga mzinga/mkopo, kitu ambacho si kibaya.

Leo tuangalie reggae kidogo, ni kukumbushana tu mana muziki huu unaujua hata kabla siajuelezea. Hapo tayari ushafikira kina Bob Marley na wenzake, ushaangalia picha yangu na mawazo yako yashakupeleka kwenye kuhusisha reggae na bange. Pole sana.

Tunaangalia reggae laini 'riddim au rhythm' na tunamkuta jamaa anaitwa Eric Donaldson. Huyu ndiye mwimbaji wa kwanza kabisa wa wimbo uliowapa umaarufu UB40 Cherry oh Baby. na kwao Jamaica ana sifa zake nzuri tu zinazomfanya awe kati ya wanamuziki wenye kueleweka na jamii kubwa.

Mimi reggae sio kivile sana huku unavuta jani, yes, kuna tofauti kubwa sana kati ya jani na cocaine, ya pili haijawahi kumwacha mtu salama.

Kupunguza maneno nakuwekea vibao vyote kwa pamoja.na nimezitoa YouTube

Tuwe na weekend njema

Na hapa ni Eric akifanya yake (hii ni video mfu)

Asante Obe kwa music
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom