
ISAYA 40
31."Bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya;watapanda juu kwa mbawa kama tai;watapiga mbio wala hawatachoka.
TUOMBE
Baba asante kwa kutufikisha umbali huu,asante kwa wema wako na fadhili zako zisizo na mwisho.
Bariki kazi,ndoa,familia,wasafiri.
Ponya wagonjwa,watie moyo wafiwa ,yatima.
Tutie nguvu ya kukungoja wewe na kukutegemea siku zote za maisha yetu.
Baba tunakupenda,tunakuheshimu,tunakutukuza,kunakushukuru kwa yote tunayoyapitia..upo nasi daima Mfalme wa Amani.
Roho Mtakatifu tawala maisha yetu,tufundishe kusamehe,Upendo na uvumilivu daima
Katika jina la Yesu Kristo mpatanishi na mwokozi wetu..Amen
MUWE NA SIKU NJEMA ,MBARIKIWE