Makapuku Forum

Makapuku Forum

1968 - Robert F. KENNEDY anafariki Dunia siku moja baada ya kupigwa risasi huko Los Angeles alipokuwa anafanya kampeni za Urais.

The Kennedy Curse:

Huu ni msemo unaorejelea Vifo tata vya wanafamilia wa Kennedy.

Wanafamilia wengi wa Ukoo wa Kennedy wamekufa vifo vyenye utata mkubwa na vya kuhuzunisha. Inaonekana kama kuna watu kadhaa nyuma ya mpango huu wa siri ambao hawakuipenda kabisa familia ya Kennedy ishike madaraka ya aina yoyote nchini Marekani.
 
2016 - Taarifa mbalimbali zisizo rasmi zinadokeza kuwa Bibie Hillary Clinton huenda akatangazwa kama Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Democrats na kuwa mwanamke wa kwanza kufanya hivyo katika miaka 240 ya historia ya Marekani.
 
1939 - Jaji Joseph Force Crater anatangazwa rasmi amefariki Dunia baada ya kutafutwa bila mafanikio baada ya kupotea kwa miaka 9.

Jaji Crater alipotea mwaka 1930 alipokuwa na kashfa za kisiasa na hakuwahi kuonekana tena, hali hiyo ikawafanya FBI na Polisi kumtafuta lakini baada ya miaka tisa toka kupotea kwake wakatangaza amefariki.

Jalada la Kesi yake lilikuja kufungwa miaka 40 baadae baada ya kupotea kwake.

OMBI:

Mkuu Bitoz itapendeza siku tukapata top 10 ya watu waliopotea na kushindwa kuonekana tena. Wapo akina Jimmy Hoffa na DB Cooper.
6ba416565b4621de5539789097090975.jpg
84653a01cd41d1fb77512e3486dbf1f8.jpg

Alizaliwa mwaka 1889
Alikuwa ni Jaji wa Mahakama Kuu ya New York
Mara ya Mwisho(last seen) ilikuwa ni alipotembelea West 45th Street huko Manhattan ambapo alionekana akitoka kwenye mgahawa maarufu
.
.
.
Ombi lako litashughulikiwa
.......
 
1969 - Fernando Redondo anazaliwa.

Kiungo fundi wa Kiargentina ambaye pia aliwahi kutamba na Real Madrid na Inter Milan.

Anakumbukwa kwa kumpiga tobo beki wa Man Utd Hening Berg kwa kisigino katika pambano la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
1968 - Robert F. KENNEDY anafariki Dunia siku moja baada ya kupigwa risasi huko Los Angeles alipokuwa anafanya kampeni za Urais.

The Kennedy Curse:

Huu ni msemo unaorejelea Vifo tata vya wanafamilia wa Kennedy.

Wanafamilia wengi wa Ukoo wa Kennedy wamekufa vifo vyenye utata mkubwa na vya kuhuzunisha. Inaonekana kama kuna watu kadhaa nyuma ya mpango huu wa siri ambao hawakuipenda kabisa familia ya Kennedy ishike madaraka ya aina yoyote nchini Marekani.
5027fe0913a81e4f486165d36a196811.jpg
367fa50cd4b17349f892055b2cd2f0f1.jpg
51575b5467634407985b8fe6abcac40f.jpg
4df9dabbe4989c3ec9ac8190d5bd9bc9.jpg

Mmoja kati ya ukoo wenye nuksi zaidi duniani

Tumeaswa kuchunguza koo wanazotokea wachumba/wapenzi wetu maana kuna koo ni balaa
.......
 
ISAYA 40

31."Bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya;watapanda juu kwa mbawa kama tai;watapiga mbio wala hawatachoka.

TUOMBE

Baba asante kwa kutufikisha umbali huu,asante kwa wema wako na fadhili zako zisizo na mwisho.

Bariki kazi,ndoa,familia,wasafiri.

Ponya wagonjwa,watie moyo wafiwa ,yatima.

Tutie nguvu ya kukungoja wewe na kukutegemea siku zote za maisha yetu.

Baba tunakupenda,tunakuheshimu,tunakutukuza,kunakushukuru kwa yote tunayoyapitia..upo nasi daima Mfalme wa Amani.

Roho Mtakatifu tawala maisha yetu,tufundishe kusamehe,Upendo na uvumilivu daima

Katika jina la Yesu Kristo mpatanishi na mwokozi wetu..Amen

MUWE NA SIKU NJEMA ,MBARIKIWE
Amen mama mchungaji, nawe pia siku njema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom