Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mkuu Transcend ushauri wako wa mmi kutoka porin sahau ....porin raha sana ....
babc9bf0895098d0c3889009b1442d02.jpg
Shemela nilikuambia muende wote porini, umeona sasa
 
Muziki: Jumapili Bila Muziki, kweli😵

Habari Makapuku, wikend imeisha na sasa ni mwanzo kabisa wa wiki mpya. Itakuwa poa naamini.

Nilikaa kusubiri burudani ya Jpili, well ninapenda gospel zaidi ya gossip so nikakaa kumsubiri Sweetiepie akuje alete oldies lakini sijui yeye na EMMYGUY wamepotelea wapi, isiwe ishu, maana kama BlessedHope yuko kwenye maombi basi demi atakuwa anajiandaa na wiki mpya. Nikaona kama vipi wacha tupate japo muziki kiduuchu huku gitaa likitawala.

Kuna vitu kadhaa ambavyo mtu kamili anapenda ama kwa kupenda au kulazimika kuvipenda, mosi, kula na kunywa, pili, kujamiiana, tatu, kuwa na marafiki, nne, kufanya kazi. Na tano, kusikiliza muziki na hiki ndicho nakuletea muda huu ukijiandaa kuitafuta wiki mpya siku zilezile.

Wikend yangu ilikuwa vizuri na niseme tu ilikuwa nzuri sana maana wakati nimekaa mahali naangusha moja moja kwa mpango akaja jamaa ana duka mkononi (TRA msitoe macho) na akaniuzia spika yeye kasema ina bluetooth, sijaijaribu kuamini lakini niliinunua nikiwa under influence ya Safari. Niache porojo.

Inawezekana ushawahi kusikia wimbo huu ila muimbaji umekuwa huna hakika sana, maana ni wimbo wa kitambo sana lakini bado ukiusikiza utadhani ndo kwanza unanukia kama wali nazi au mishkaki ya kwa Mfojo au kwa Gideon (kile kichochoro cha Billz) au mishkaki ya kwa Igasha, well natamani kusema shurubati ya Salma koni kwa waliowahi kufika mza miaka ya zamani.

Anaitwa Emmylou Harris, ana tuzo 13 za Grammy kibindoni na keshafanya kolabo na wanamuziki nguli unaowasikia katika Country music.

Msikize hapa katika wimbo huu If I needed You. Ukiwa na muda usake ambao kafanya na Don Williams

Muwe na wakati mzuri watu wazuri wa humu Makapuku.


Asante kwa music kiongozi Obe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom