Baadae kwenye amka na BBC kwa wale wapenzi utasikiaa....
[emoji117]Vyama viwili vya upinzani nchini Rwanda vyamtangaza Rais Paul Kagame kuwa ndiye mgombea urais kabla ya chama chake kufanya hivyo
[emoji117] Kwa mara ya kwanza bunge la Afrika mashariki lapitisha bajeti ya dola milioni miamoja na kumi nukta tatu kukuza kiswahili
[emoji117] Polisi nchini Uingereza imewakamata watu kumi na mbili mashariki mwa London na wanaendelea na msako katika eneo hilo.
[emoji117] Leo ni kilele cha siku ya Mazingira duniani , hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro imeahidi kuendelea kutunza na kuboresha mazingira ya eneo la Mrusungu ambapo ndipo ulipo mti mrefu zaidi barani Afrika.
[emoji117] Bendi ya Abaki Simba nchini Kenya inatumia ala za asili na kuhamasisha amani huku ikiwataka vijana kutotumiwa na wanasiasa.
[emoji117] Lakini pia Utasikia vijana wabunifu wa programme za simu nchini Tanzania kurahisisha maisha, kwa namna gani? AMKA NA BBC ufaidike