Muziki ni Kuwekeza.
Hivi kila ninapoandika haka kakipengele ni lazima nianze na salamu! Huna haja ya kujibu maana sijauliza swali. Habari za mihangaiko Makapuku wenzangu, najua wote tuko vema sana.
Ni tarehe moja na ndo inakatika, najua wapo ambao hawajarudi home maana mama/baba mwenye nyumba hajalala anasubiri kodi. Hongera kwa wamiliki wa nyumba wote mlio humu, na mtushukuru sana sisi wapangaji wenu tuliotulia tu humu, mngeitwaje baba/mama mwenye nyumba kama sio sisi? Heshima kwetu wapangaji
😀
Kiukweli leo niwe mkweli kwenu, sikupanga kuandika kitu kutokana na sababu zilizo ndani ya uwezo wangu. Lakini kutokana na vitisho vya mjomba wangu
lee empire kuwa nisipoandika atanitoa kwenye plan ya simu (kajiunga na jazwa ujwaze ya Tigo, kaunganisha line nne, anajazwa anatupunguzia salio sis family yake, ila uko makini kama makinikia kutofanya mchezo na Tanesco na plan yao ya
'acha kulipa,....., asante mjomba).
Kisa cha mimi kuandika leo ni 'matters of the heart' kwa sana na nikaona ana hoja ambyo siwezi kuipuuza, mimi sio mpuuzi. So, akaniambia sisi Makapuku ni family na mwenzetu anapofikwa na la kumfika iwe yeye mtu wake wa karibu nasi tukajua basi tunasema pole kwa pamoja. Na anapoondoka na kurudi basi tunafurahi kwa pamoja na ndicho ninachofanya leo kwa ajili ya
Shunie nikiwajumuisha wote waliopatwa na ya kuwapata bila kupakatwa.
Kikawaida katika kuitafuta Furahiday huwa napenda kuweka kitu motomoto, kitu cha mikatiko kama si mitikisiko, praktaratumbaa. yeah, kitu Yondo sister na gitaa la Alain Nkounkou.
Lakini leo ninaweka kitu maalum kwa member wote wa Makapuku ambao kwa sababu tofauti waliondoka humu jukwaani na wamerejea tuko pamoja nao, karibuni na it is so good to see you back.
Nitamuelezea siku nyingine maana sitaki kuandika sana kuhusu yeye bali nakuacha ufurahie gitaa tamu na sauti nzuri toka kwa mkongwe Don Williams.
Karibu