Makapuku Forum

Makapuku Forum

2/Yazidi Communities bombings
8b288e91cb29aa624d88a9fb754f7fe1.jpg
8b57a3229519bdf8f739dddce206aeb4.jpg
9684e10127c30d4a748eee237fa9a58e.jpg

Hii pia ilitokea nchini Irak
Ilikuwa Agosti 14 mwaka 2007 wakati yalipotekelezwa matukio manne ya watu kujitoa mchanga(kujilipua) na kuua karibia watu 3k (2900+}

USA kumuondoa Saddam kumechochea sana kuvurugika kwa Irak yaani watu wanakufakufa km kuku huko matukio hayaishi
.......
 
3/Iraq May attacks
3c12ff46b3bd6aa0d597717b0514964c.jpg
2d4eae4c891ca30b2d4cae8e958d55a8.jpg

Ni mashambulizi yaliyotokea Irak mwezi May mwaka uleule wa 2013
Ulikuwepo mfululizo wa milipuko ya mabomu na watu kupigwa risasi katika mikoa ya Kaskazini na Katikati ya Irak
Watu zaidi ya 500 walipoteza maisha
......
Wale jamaa maisha yao ni mwendo wa milipuko tuu

Juzi walipata mlipuko mwingine tena mkuu.
 
1/September 11 attacks
4492f209df9b7a082b7163b4f734323e.jpg
85eb17287ac636fa1cdb4f1df55c4008.jpg
0017238d93527e85b463a69794b3ffda.jpg

Hhi wala siandiki maneno mengi...kila mtu anajua alichokifanya Osama Bin Laden mwaka 2001 lakini mwisho wa siku akasakwa na kuuawa
Watu karibia 3k (2996) walifariki huku zaidi ya 6000 wakijeruhiwa
.
.
.
.
.
.
Shukrani kwa mliosapoti mada
Tukutane kesho
..........
 
Muziki ni Kuwekeza.

Hivi kila ninapoandika haka kakipengele ni lazima nianze na salamu! Huna haja ya kujibu maana sijauliza swali. Habari za mihangaiko Makapuku wenzangu, najua wote tuko vema sana.

Ni tarehe moja na ndo inakatika, najua wapo ambao hawajarudi home maana mama/baba mwenye nyumba hajalala anasubiri kodi. Hongera kwa wamiliki wa nyumba wote mlio humu, na mtushukuru sana sisi wapangaji wenu tuliotulia tu humu, mngeitwaje baba/mama mwenye nyumba kama sio sisi? Heshima kwetu wapangaji 😀

Kiukweli leo niwe mkweli kwenu, sikupanga kuandika kitu kutokana na sababu zilizo ndani ya uwezo wangu. Lakini kutokana na vitisho vya mjomba wangu lee empire kuwa nisipoandika atanitoa kwenye plan ya simu (kajiunga na jazwa ujwaze ya Tigo, kaunganisha line nne, anajazwa anatupunguzia salio sis family yake, ila uko makini kama makinikia kutofanya mchezo na Tanesco na plan yao ya 'acha kulipa,....., asante mjomba).

Kisa cha mimi kuandika leo ni 'matters of the heart' kwa sana na nikaona ana hoja ambyo siwezi kuipuuza, mimi sio mpuuzi. So, akaniambia sisi Makapuku ni family na mwenzetu anapofikwa na la kumfika iwe yeye mtu wake wa karibu nasi tukajua basi tunasema pole kwa pamoja. Na anapoondoka na kurudi basi tunafurahi kwa pamoja na ndicho ninachofanya leo kwa ajili ya Shunie nikiwajumuisha wote waliopatwa na ya kuwapata bila kupakatwa.

Kikawaida katika kuitafuta Furahiday huwa napenda kuweka kitu motomoto, kitu cha mikatiko kama si mitikisiko, praktaratumbaa. yeah, kitu Yondo sister na gitaa la Alain Nkounkou.

Lakini leo ninaweka kitu maalum kwa member wote wa Makapuku ambao kwa sababu tofauti waliondoka humu jukwaani na wamerejea tuko pamoja nao, karibuni na it is so good to see you back.

Nitamuelezea siku nyingine maana sitaki kuandika sana kuhusu yeye bali nakuacha ufurahie gitaa tamu na sauti nzuri toka kwa mkongwe Don Williams.

Karibu



 
binamu umemsikia mjomba ako sio unakuja kwa mama mchuchu na kugonga like tu


Sijamsikia, itabidi nikae chini nimsikize, au kaniharibia! Maana huyu mjombaangu full matatizo si kaenda kumwambia BH kuwa tuliendaga kwa mganga wa kienyeji kuangalia nyota, huku akijua kabisa BH na wapiga ramli ni kitumbua na mchanga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom