The Little Magic angel
Sehemu ya tatu
Ndani ya Miami Beach
Ilipoishia
....
.....
.....
Kwa kuwa Chief Commander alijua kuwa anapambana na kiumbe asichokijua, kiumbe ambacho kinaaminika kuwa kimedondoka kutoka juu, aliwaza labda kiumbe hicho kinaweza kuwa alien; na kinaweza kuwa kiumbe cha ajabu na hatari. Alitumia ujuzi wa kijeshi kwa kujaribu kuwaambia wanajeshi wake wazime tochi pia wakae kimya. Alitaka kujua kama hicho kiumbe kinaona na kinasikia. Na kinatumia njia na silaha gani katika kujilinda? Hayo ndiyo yalikuwa mawazo ya haraka haraka ya Chief Commander McClaw.
Ukimya wa dakika tano bila kufanya chochote kile.sauti za watu waliokuwa wakiomba msaada zilisikika.
McClaw alilijua hilo alitambua fika kuwa watu wanaolia niwazi kuwa walijeruhiwa na kiumbe huyu ambaye mpaka sasa hawajajua ni nani?.
Haikuwa rahisi kuweza kujua nikiumbe gani sababu ya kiza kinene usiku ule.
McClaw alihisi labda kiumbe walichokuja kukabiliana nacho.
Kwa uweledi mkubwa alionao aliamua kufyatua risasi moja angani. lengo kujua kama kiumbe kipo maeneo hayo au kimeondoka?
Baada yakuona hakuna reaction yoyote ile iliyotokea aliaamulu kikosi chake kifanye upekuzi kwa kila kona ya Miami Beach.
Walifanikiwa kukuta miili ya watu 16 waliokwisha fariki na majeruhi 8.
McClaw alipiga simu hospital iliyo karibu na Beach hiyo.ilikuwa ni Mercy Hospital kuita gari ya wagonjwa kuweza kutoa msaada wa haraka kwa wahanga.
Majeruhi walikuwa na hali mbaya sana. Majeraha yao yalionekana ni kama yameunguzwa na moto mkali sana na sio risasi.
Hali hiyo ilimpa mawazo Chief Comander watu "wameunguzwa kiasi hiki na nikiumbe gani ambacho kinatumia moto kama siraha yake yakujikinga?"McClaw alikuwa akijiuliza
Alibaini wenda akawa ni Dragon au Dinosaur "lakini mbona wanyama kama hawa walitoweka dunia miaka mingi iliyopita"aliendelea kujiuliza bila majibu yoyote.
Alimwita kando Detective Kelvin Ago waongee kuhusu vita hii wasiyo ielewa.
"nimepigana na vita nyingi tokea nizaliwe lakini hii sijawahi kuiona"McClaw alifungua maongezi.
"Mkuu chakufanya hapa ni kuwa makini kwa kila hatua tunayopiga"Detective alijibu.
"hakika usiku umeingia sana pia nimechoka sana tukutane kesho asubuhi tupange mbinu mpya ya kupambana na hivi viumbe"alimpa maagizo kisha akapanda gari yake akaondoka.
Ndani ya San Francisco
Wakati Chief Commander anarudi nyumbani baada ya kazi ngumu ya usiku njiani gari yake ilipata tatizo(Jam)"shiiit"alilalama huku akishuka na vifaa kwa hasira hili alitengeneze.
Wakati anaendelea kulitengeneza uso kwa uso na kiumbe kinafanana kabisa na binadamu lakini ni kirefu(giant) sana na kinaonekana kuwa na hasira sana kanakwamba kimekula pili pili.
Je nini kiliendelea hapo usikose sehemu ya nne hapa hapa makapukuz