Makanisa yavunje MoU na Serikali...

Makanisa yavunje MoU na Serikali...

Ninachojua ni hicho alichokieleza Joka kuu kwenye thread namba 297. Kwahiyo ukubali tu kwamba Nyerere aliwafanyia favor kwa kuwapora mashule wengine ili na wale wasio na shule zao kama waislamu wapate access kwenye shule ambazo kimsingi zilikuwa ni kwa ajili ya watu wa dini fulani tu. Huo ndo ukweli, ukubali ukatae, Nyerere aliwabeba waislam katika suala la elimu, full stop.
Hajaeleza kitu maana Jokakuu kauliza swali, wewe nambie zile shule ulizijenga wewe au wazazi wetu walizijenga?.. Na kwa nini unasema kuna shule za Wakristu hawa walikuwa kina nani?
 
Wakoloni walijenga shule za serikali, na makanisa yalijenga shule za wakristo wao. Inaonekana hata huelewi kwamba kabla ya uhuru shule ya wakatoliki walikuwa wanasoma wakatoliki, ya waanglikana ni kwa ajili ya waanglikana etc. Na serikali ya kikoloni ilikuwa na shule zake ambazo hazina uhusiano na dini yoyote. Inaonekana hilo hujui, unabwabwaja tu.
Ina maana unataka kuniambia kuwa pamoja na usomi wako huo umeshindwa kujua kuwa Wakoloni kila wanapokwenda wanakwenda na Wamisionari?! umeshindwa kujua kuwa Tanganyika pia walikuja pamoja na Wamisheni?
Umesema kuwa Wakatoliki walikuwa wakisoma shule za Kikatoliki, Waanglikana wanasoma Shule za Kianglikana hujasema pesa za ujenzi na uendeshaji zilitoka wapi, na ni katika mwaka gani Kanisa lilitenganishwa na Serikali!
Tunakwenda sehemu nzuri ambapo utakuja kujihakikishia kuwa MoU ni muendelezo wa ukoloni hasa ukizingatia kuwa aliyeshiriki kuuratibu ni former colonial Master (Mjerumani)
......kajipange!
 
Hajaeleza kitu maana Jokakuu kauliza swali, wewe nambie zile shule ulizijenga wewe au wazazi wetu walizijenga?.. Na kwa nini unasema kuna shule za Wakristu hawa walikuwa kina nani?
.

ndiyo maana mimi hizi dini za kikoloni nazichukia sana. ni chanzo kikuu cha vurugu na ndizo zitakazokuwa kiini cha vita vikuu vya tatu vya dunia...note my words...

Pili, ningefarijika sana kama ningekuwa na namna ya kujua kwa uhakika pasi shaka yoyote kuwa haya mawazo ya kina Mkandara ndiyo kweli mawazo ya waislamu walio wengi hasa wale wa hali za kati na chini. Kama ndiyo mawazo ya waislam walio wengi basi jibu ni kuwa kanisa livunje hizo MoU haraka sana...dont argue with a fool coz people might not notice the difference. Mkandara nikuulize...je unao ushahidi wowote kuwa kuna wakti wowote hapa Tanzania kanisa lilishindwa kujiendesha kifedha au ki-menejiment ama lenyewe au taasisi zake na hivyo kuhitaji msaada wa serikali? Je una maelezo yoyote yatakayothibitisha kuwa MoU zikivunjwa basi taasisi za kanisa zitadumaa na hivyo taasisi za madhehebu mengine zitapata nguvu ya kushamiri kiasi cha kuzifikia na hata kuzipita za makanisa?Je unajua chochote kuhusiana na dhana ya Public Private Sector Pertnership na operational mechanisms zake? Je Tanzania kwa sasa ipo katika mfumo gani wa kiuchumi kati ya kipepari(soko huria) na kijamaa? Unajua soko huria lina-dictate nini linapokuja suala la wajibu wa serikali katika utoaji wa huduma za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wake? Hivi unajua kuwa Katika MoU siyo serikali inasaidia kanisa bali ni kanisa linaisaidia serikal? Jukumu la kutoa huduma za kijamii si la kanisa wala msikiti, ni la serikali. Lakini serikali yako ya kifisadi kama hii inayoongozwa na huyu mwiislam mwenzako haiwezi kamwe kuhudumua wananchi walio wengi na wasiyo na uwezo. serikali yako inahudumia mafisadi wachache. Kanisa kwa kuona hivyo na katika kutimiza lengo na madhumini na filosofia ya uwepo wake wa kuhudumia na kuponya roho na mwili wa mwanadamu ndiyo likaanzisha huduma hizi za kijamii na kiuchumi pia. Kwa bahati mbaya au nzuri huduma zinazotolewa na kanisa ni bora mara dufu ya zile za serikali. sababu ni nyinyi lakini za msingi ni kama mbili. ya kwanza-Kanisa limejijenga juu ya msingi wa elimu, ujuzi maarifa na ufahamu. kanisa linafanya tafiti nyingi na makini, zote za kimungu na za kidunia. kanisa ni mkusanyiko wa wanataaluma waliobobea, watu wanofikiri kwa uwigo mpana, maono ya mbali ya miaka hata mia mbili ijayo, ni watu ambao kwa sasa wanachokifikiria ni vitu kama ni kwa namna gani wataweza kwenda kuanzisha kanisa na huduma ambatishi za kijamii na kiuchumi huko mwezini na/au huko mars. hawa jamaa hawafiri na kulia machozi sababu mtoto kakojolea kitabu(whatever the book that is). These thinkers mean business. Ya pili- Kanisa lina mfumo makini na dhabiti wa kimenejimenti ya mali zake na rasilimali zake na hasa rasilimali watu. huwezi sikia watu wanateka misikiti huko. huwezi sikia waumini wanampinga Malasusa au Pengo. Ndani ya hiyo mifumo yao makini ya kimenejiment kuna chachu kamilifu ya utii, nidhamu, upendo na haki.

kAnisa na taasisi zake pote duniani zitaendelea kukua, kupanuka na kuwa na impact kubwa sana kwenye maisha ya wanadamu coz kanisa lipo efficient, effective na lina good governance. Katika kutoa huduma za kijamii itachukua miaka mingi kabla serikali yako ya kifisadi ya Tanzania kuweza kujinasua kwenye kuhitaji mashirikiano na kanisa ili iweze kutoa huduma kwa wana wa nchi. kanisa lina uwezo wa kufika(nA kwa hakika tayari limeshafika) pale ambapo serikali(hasa serikali inapokuwa ya kifisadi KAMA HII YAKO) haiwezi kufika na/au itawachukua miaka mingi serikali kufika na kutoa huduma kwa kiwango cha ubora unaotolewa na makanisa. Fedha inayopelekwa na serikali kule KCMC hosipitali siyo msaada kwa kanisa. ni kwamba serikali haina uwezo wa kumiliki hospital kama KCMC. KANISA TAYARI LINAMILIKI hospital ya kiwango cha KCMC, TENA SI MOJA NI NYINGI. Kwa hiyo serikali kwa kutambua kuwa wajibu wa kutoa huduma ya afya kwa wananchi kimsingi ni wa serikali, na kwa kutambua kuwa hata hivyo "haina uwezo" (kama vile isivyokuwa na uwezo wa mambo mengine yote) wa kutoa huduma hizo kwa kiwango na ubora wa Kanisa basi serikali inaliomba kanisa kuwa washirikiane; serikal itoe ruzuku(sehemu ya gharama za uendeshaji) ili kanisa litoe huduma kwa bei nafuu na kwa kutumia physical infrustructure za kanisa kwa faida ya maskini walio wengi wakiwemo mimi (possibly na Mkandara). Mkandara, huwezi kuzuia maendeleo ya jirani yako kwa kumloga, jifunze kafanya nini kufika pale na wewe fuata njia hiyo kama ilivyo au kwa kuiboresha zaidi. Mkandara you cant eat your cake and have it. nyinyi mnatia mkazo zaidi kwenye vitu vya akhera ili mpate dhawabu huko mbinguni, so ngojeeni dhawabu zenu. kanisa linazingatia akhera na duniani pia. matokeo ndo hizi tofauti mnaziona. na kwa taarifa yenu kanisa (na taasisi zake) lilivyo leo mjue kabisa ni matokeo ya uwekezaji wa karne na karne, si jambo la leo au jana kaka. nyie mnadanganya watu MoU ikivunjwa basi kufumba na kufumbua waislamu watakuwa wapo byee...dhubutu yake. Anzeni sasa kuwekeza kwenye elimu, matokeo yake hutayaona wewe mukandara wala watoto wako. pengine mjukuu wa watoto wako ndo wanaweza kuanza kufaidi tena kama mtakuwa makini, agressive and hard working. Sasa wewe mkandara mfungia mke wako manguo lukuki mwilini kiasi kwamba yanamwelemea hadi anashindwa kwenda kuchacharika kuuza nyanya kule kariakoo halafu ushindwe kusomesha watoto wako then ubakia kujidanganya wewe na wenzako eti kanisaaa kanisaa, kalaghabaho!!! wake za waarabu kule saudia wanaweza kufanya hivyo(uchumi wao unaruhusu) lakini kibongobongo ni ngumu kaka. mazingira ni tofauti. lakini huwezi kuelewa hii kitu ni hadi uwe una-think outside the box.

Mwisho wa siku(na hasa ukishaweza kufikiri outside the box) kumbuka kuwa religion is nothing but an opium of the people...
 
Mkuu Barubaru, Leo Ijumaa, kusema maneno yanayopishana na UKWELI kwa mtu kama wewe si vizuri. Sidhani kama Allah anapenda hilo. Nitakuambia tena na tena, SIKONGE Hospital ya Wamoravian, hawalipwi hata senti tano na Serikali kwa siku nyingi. Hata madawa kwa sasa wanatumia yanayotolewa nje ya nchi. Sanasana kwa yale magonjwa hatari kama Ukimwi, Ukoma nk Ukitaka naweza kukupa simu ya Kiongozi mkubwa tu wa Hospitals na atakupa maelezo yake yote kuhusu ugumu wanaoupata kwa kutokupewa pesa na Serikali. Najua una fahamiana na watu wengi hapa TZ, basi waulize kwa mwaka huu tu wameshapeleka SHILINGI ngapi Sikonge Hospitals? Pana wakati walikuwa na deni kubwa sana la mafuta kutoka kwa Hemmed Nassor na ikabidi tu wamlipe kwa kumpa gari ambayo ilikuwa imeletwa kama msaada. Enzi hizo hata umeme hakuna na inabidi wawashe Generator kama wanataka kufanya upasuaji wa mtu yeyote bila kujali ni nani. Leo nasikia eti WANATAJIRIKA. Fanya homework yako tena. Vinginevyo utasikia hata ndugu zako wa SIkonge wanabadili dini ili waweze kutibiwa. Sidhani kama utaweza kuwasaidia wote kwa matibabu maana kifamilia kikubwa sana..
Sikonge.

Tunarudi pale pale kuwa hujui maana niliyobainisha pale nilipopambanua MoU yenu niliposema Admin Cost na Ops Cost.

Ulizobainisha ni sehemu tu ya Pps cost. labda nikuulize je mishahara ya wafanyakazi wake kuanzia madaktari, wauguzi na watu wa maabara wanalipwa na nani?

lakin kubwa ili kuleta maendeleo huko tabora lazima kupatikane barabara za Uhakika, Usafiri mzuri wa Reli na kupatikana kwa nishati ya Umeme.

nahene
 
Barubaru,

Ndiyo hicho ninakisema muda wote. Labda niseme tena kwa ufupi:

MISHAHARA ya Wafanyakazi, madawa na vifaa, SERIKALI HAITOWI hata SENTI TANO. Narudia tena, kuwa kwenye mkataba wa MOU, wanatakiwa wawe wanapeleka Tsh.20 milioni kwa mwezi, ila kwa sasa wanapeleka TSh. 00,000 milioni kwa mwezi.

Sasa kama ungelikuwa wewe ndiyo MUHASIBU wa Hospital hiyo, na elimu yako uliyonayo sasa, UNGELIFANYA NINI?

Halafu eti Tsh.20 milioni kwa mwezi utegemee KANISA litajirike. Hivi Mshahara wa Gavana wa BoT ni Tsh ngapi vile?

Mengine nakubaliana kabisa na wewe pia Mkandara kwamba:
  1. Wajibu wa kutoa huduma za Jamii, lazima urudi MIKONONI mwa Serikali ya Tanzania na hizi MOU zivunjwe. Ila kama walivyosema baadhi ya wadau, MOU kizivunjwa leo, kutatokea PENGO kubwa sana kati ya Waislaam na Wakristo. Hilo pengo linaweza kuwa hatari sana huko mbeleni.TUVUNJE MOU? Ndiyo zivunjwe ila kwa kutumia AKILI na bila papara. Serikali ianze KUBEBA msalaba wake yenyewe kwa kuwajibika kwa wapiga kura wake. Tumebaki kuwa kama Makinda ya ndege yatima kwa kupata au kulilia misaada kutoka kwa Wazungu/Waarabu/Waasia. Mara makanisa, mara umoja wa Kiislaam uje utowe misaada, mara Wajapan watoe misaada. Serikali ya nini basi kama haiwezi kujiendesha? Labda tuwakaribishe hao wanaotoa misaada ndiyo wawe wanasaidia KUENDESHA NCHI.
  2. Hapo kwenye RED hakuna la kuongeza wala la kupunguza.

Naona wote tunaongea jambo hilo hilo moja ila kila mtu kasimama sehemu nyingine. Nafikiri Mkitusoma vizuri, mtatuelewa.
Sikonge.

Tunarudi pale pale kuwa hujui maana niliyobainisha pale nilipopambanua MoU yenu niliposema Admin Cost na Ops Cost.

Ulizobainisha ni sehemu tu ya Pps cost. labda nikuulize je mishahara ya wafanyakazi wake kuanzia madaktari, wauguzi na watu wa maabara wanalipwa na nani?


lakin kubwa ili kuleta maendeleo huko tabora lazima kupatikane barabara za Uhakika, Usafiri mzuri wa Reli na kupatikana kwa nishati ya Umeme NA MAJI.
nahene
 
ni kama baba wa familia anayeiacha familia ya ndoa yake ikiteseka na kwenda kuneemesha familia ya hawara......aibu sana na hawara na familia yake wanashangilia kuona upande wa pili wakilala njaa........pesa hizo zinazokwenda kanisani si zingetumika hata kuwaboreshea walimu, madakitari na watumishi wengine wa serikali......huu ni ufisadi.....halafu unataka uraisi 2015 aaaaah haiwezekani........labda ulitumie kanisa maana ndio mafisadi wenzako....
 
Shule zao wanafundisha karate(kung fu) sijui wanajiandaa na nini aisee,ushahidi ukiwa nyuma ya Block C Mabibo Hostel asubuhi na Jioni utawaona na kuwasikia pale Ubungo Muslim:hail:
 
INGEKUA VIPI KAMA ISINGEKUAPO NDANDA HOSP.NYANGAO HOSP,IFAKARA,PERAMIO,KITUO CHA AFYA MBAGALA(MBAGALA MISSION),BUGANDO HOSP.KCMC HOSP.....NA NYINGINEZO NISIZOFAHAMU,
AU INGEKUA VIPI VYOTE NILIVYOTAJA VINGEKUA VINAUDUMIA WAKRISTO TU,
ushauri wa bure ni kwamba,ukimuona jirani yako amevuna mahindi mengi shambani mwake jiulize utamzidi vipi mavuno hayo na si kwenda kwa mganga kutafuta dawa ya kumroga.

huruma hospital,kairuki mission hospital zipo nyingi nikianza kuzitaja zote hapa itakuwa aibu
 
ebu sikilizeni niwaambie nyie WAKRISTO naomba mufaham kua waislamu wameamka na wanaelewa jinc gani mambo yanavoenda hakuna hasiefahamu dini ya kikristo inavobebwa na serikali katka nyanja mbalimbali za maisha nchini na kinachonickitisha ni kwamba hamjui kusoma alama za nyakati kwa kung"ang"ania kulazimisha watu wataje njano hali ya kua ni nyekundu na kusahau kua waislam cku moja moja watazinduka na kuhoji mambo yanvoenda.kwa nia njema naomba nawakumbushe kutumia plopaganda i.e waislam wanavunja amani ya nchi,waislam ni maghaid n.k c suluhisho la matatizo tuliyonayo kwani hata waandishi mbalimbali wa dini yenu kama DR. JOHN SIVALON wameelezea kwa kina suala hilo.PIA niwakumbushe kua hakuna mtu hasiye na uchungu na dini yake na acheni mchezo na imani za watu vile vile naomba mtambue kua hakuna mtu yeyote anayependa kuona nchi yetu inaingia kwenye machafuko na MOLA IBARIKI TANZANIA ila mi ninaamini kwa misingi hii ya makanisa kutaka kuiongoza nchi kwa manufaa yao itabadilisha HISTORIA ya nchi yetu mda c mrefu na mkitaka kulifahamu hilo tembeleeni kwenye mtandao na mcheki THE POLITICAL FUTURE OF TANZANIA.Haipingiki kusema kusema NYERERE kafanya jitihada kubwa kuliweka kanisa mahala hapo mlipo ktk nchi ila mi ninaamini WAKRISTO mda c mrefu mtakuja kulia kwa kusaga meno huku mkijuta kwa nini NYERERE alichukua uamuzi kama huu na hii ni kutokaka na expirience yangu ya kusoma alama za nyakati.Nawaomba ndugu zangu muamke na maunglie nini cha kufanya kwa usalama wa dini yenu na kwa usalama wa nchi yetu TANZANIA,Nawaomba msiwe kama NYERERE ambaye alitumia mda wake wa uongozi kuwapumbaza watu waamini njano ni nyekundu na nyekundu ndo njano kama alivofanya BI KILEMBWE ktka nchi ya GININGI kuwalazimisha watu waamini kitu kisicho sahihi ikibidi kwa kuwaua watu wenye mawazo tofauti na yeye na mwisho wake kujikuta anasalitiwa mpaka na viungo vyake vya mwili.
'MUNGU IBARIKI TANZZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA"
 
..halafu tukidai kwamba shule ni za wakoloni, what about Makanisa na Misikiti?? Je, tutakuwa tumekosea kusema kwamba kuna Misikiti na Makanisa ya wakoloni??.
Hutakosea kama utasema kuwa kuna Maknisa yaliyojengwa na Mkoloni (mengine kupitia wamisionari) kwa pesa za nchi.
Lakini utakosea kama utasema kuwa kuna Misikiti ya Wakoloni, unless leo utuambie kuwa Muarabu aliwahi kuikalia Tanganyika kama koloni lake!...zile ni pesa za jasho la Waumini wenyewe aidha iwe Waarabu au Waafrika.
Joka Kuu said:
NB:

..kuna shule za madhehebu ya dini zilijengwa kwa njia ya kujitolea na waumini wa eneo husika.
Hakuna mwenye shida au kelele na Shule,Mahospitali na Makanisa yaliyojengwa kwa njia hii.........ila vilivyojengwa baada ya kusainiwa MoU vinabidi kuchunguzwa kama havikutokana na pesa ya MoU moja kwa moja au faida ya biashara za Mahospitali na vyuo vilivyofaidika na MoU.

Masuala haya ni lazima yajadiliwe sasa hivi kama sio hivyo basi yatakuja kuhojiwa na vizazi vya baadaye katika lugha isiyopendeza.
Isiwe kama Nyerere ambaye alikuwa na solutions za muda mfupi katika haya masuala.
 
INGEKUA VIPI KAMA ISINGEKUAPO NDANDA HOSP.NYANGAO HOSP,IFAKARA,PERAMIO,KITUO CHA AFYA MBAGALA(MBAGALA MISSION),BUGANDO HOSP.KCMC HOSP.....NA NYINGINEZO NISIZOFAHAMU,
AU INGEKUA VIPI VYOTE NILIVYOTAJA VINGEKUA VINAUDUMIA WAKRISTO TU,
ushauri wa bure ni kwamba,ukimuona jirani yako amevuna mahindi mengi shambani mwake jiulize utamzidi vipi mavuno hayo na si kwenda kwa mganga kutafuta dawa ya kumroga.

Kumbuka kuwa Hospital sio MAJENGO bali hospital ni vifaa, watendaji kwa maana ya madaktari na wauguzi na watu wa maabara.

kanisa limewekeza katika majengo ya hospital na sio vifaa, wataalamu wa afya na madawa. Hizo zote zinagharamiwa na Serikali. Na pesa wanazokwapua za Mou ni kwa ajili ya Admin cost sio ops Cost.
 
Inaonyesha mtoa mada ni mtu ambaye madarasa ameyaona ila ule ukungu wa udini na kuzungukwa na wanadini wenzake ambao uwezo wao wa kufikiri huishia kusema tumuachea mungu (mfumo kristo) hata kwenye mambo yaliyo ndani ya uwezo wa akili ya binadamu. Fikiri kama mtu anaugua kipindupindu na kupoteza maisha mwisho wa siku mnasema tumuachie mungu kwani kazi yake haina makosa. Kuvunja MOU sio tatizo kama unavyo fikiri ni kitu rahisi sana lakini kwenye serikali yako ambayo walioko juu ni wenzio katika imani lakini wanatanguliza uhalisia katika kufanya maamuzi ndo maana walibatilisha uamuzi wa kufuta kodi kwenye mashirika ya kidini (muulize Jenista Mhagama Mb) Napenda kumalizia kwa kumnukuu mzee msekwa alipo kuwa speka wa bunge alisema, "......huo ni wivu wa kike..." Kama wenzio wameweza wewe ushindwe una nini??? Fanya tafiti kunako taasisi zenu za kidini utapata majibu ya hoja yako
 
Haya ni mawazo mgando kwani yanaonyesha udini hasa, hivi kwa mawazo yako kwa nini hao waislamu wasianze kutoa huduma hizo za bei nafuu ili watu wengine waende huko na ama wao kuwa na MOU na serikali kwani nani kawakataza au kuna faida gani kwa muislamu kung'ang'ania huduma za gharama kubwa anazojua zinafuja kodi yake kama hanufaiki nazo?

Hata hivyo hujalazimishwa kutumia huduma za kanisa kama unaona kutumia huduma hizo ni mfumo kristo tumia za kiislamu maana una uhuru huo wala hulazimishwi. Hiyo misamaha na hata hiyo MOU unayosema haijazuiwa kwa waislamu na sijaona ukishauri kuwa waislamu wawe na MOU na serikali maana misamaha ya kodi tayari tunanufaika nayo.

Si waislamu wote wana mawazo ya udini kama haya kwani wanaelewa athari zake.

Ni wachache sana mkuu.. (hapoo kwenye blue)
 
Wenzenu wanaitisha harambee kuchangisha fedha za kuanzisha miradi ya maendeleo nyie mnasubiri OIC iwaletee vya bure.

kwani nyie mashule na mahosipitali mengi si mlijengewa na wakoloni?

Au vyote mlijenga wenyewe?
Mlijengewa na wakoloni kisha mkaviendeleza, kwanini hamtaki na sisi tujiunge na Oic ili tupate pa kuanzia?
 
Dear Barubaru

niliattend kikao kwa mualiko rasmi kama mtaalamu mshauri, hivyo ni haki yangu kupokea bahasha baada ya kutoa utaalamu husika;

tukirudi kwenye pole yako kwangu kuwa sio ruzuku bali ni msamaha wa kodi, naomba nikupinge tena na kukurudishia weye pole yako, ni kuwa kwa sasa private hospitals zinapokea government cash ili kusaidia kuboresha huduma ya afya pamoja na kutoa unafuu

nanukuu:
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Now private hospitals to receive govt cash
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]Send to a friend
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Friday, 11 November 2011 22:26
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
nyoni-blandina-wiafya.jpg
Permanent Secretary for Health and Social Welfare, Ms Blandina Nyoni.

By Songa wa Songa
The Citizen Correspondent
Dar es Salaam. In what has been described by observers as a major policy shift, the State will soon start allocating substantial amounts of money to private hospitals to facilitate more and better health service delivery in disadvantaged rural communities.

It has emerged that the government and donors have reached an agreement to channel half of the Sh168 billion in health budget support funds directly to public and private hospitals at the grassroots.

According to the government and the donors, this is a deliberate move to drive quick health delivery results through local councils throughout the country.Areas targeted include those that are highly disadvantaged, it was revealed yesterday by the ministry of Health and Social Welfare.

The donors who are expected to contribute some Sh168 billion this financial year noted that the new cash injection system would expand access and quick health service.

Through the initiative, about half of the funding or Sh81 billion will be channeled directly to local government authorities. This amount will go into financing front line health services in both private and public institutions.
The move to directly channel health funds to the councils would be welcome news following widespread complaints of embezzlements by the many layers of State bureaucracy. "


asante Barubaru, ni kwania njema serikali inafanya ifanyayo kupitia wafadhili wakuu ambao ni global fund ( muungano wa nchi zinazokubali ushoga , nchi zenye mfumo kristo tena wa kanisa katoliki etc...) ili kunufaisha jamii ya watanzania kwa umoja wao wa kiislamu, kikristu na kipagani...
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Nsiambe,

Kwa kweli kuna mengi sana unahitaji kujifunza kutoka nchini mwako ikiwemo tarbia ya wanasiasa na viongozi wenu.

Kumbuka kuwa Kama utapitia makadirio yya Bajeti ya JMTz 2010/2011 zilikadiriwa na kupitishwa 12.6 Trilion lakin zilizopatikana na kutumiwa kwa muda huo wa fedha ni 7.3 Trillion. Na hivo kusababisha miradi mingi ya maendeleo kukwama kutekelezeka.

Lakin vile nikipitia kwenye Bajeti ya wizara ya Afya na ustawi wa jamii ya mwaka 2010/2011 na 2011/2012 sioni pesa hizo kutengwa. Labda unisaidie zimetengwa katika mfuko gani wa bajeti yenu ili nasi tuone.

Lakin vile vile kwa mujibu wa bajeti ya Wizara ya Afya zimebainisha wazi Kuwa Pesa za Global Fund zinatumiwa na wenyewe kupitia kwa organization mbalimbali katika kfadhili miradi ya Afya ya mama na mzazi, HIV na malaria.

Na zile zinazoingizwa Serikalini kwenye wizara ya Afya zinaingia Kwenye mfuko wa BASKET FUND. na ukiangalia mfuko huo hakuna kitu kama hicho.

naomba ufafanuzi wako je pesa hizo watazitoa kwenye fungu/mfuko gani.

 
Usieneze uwongo mwingine. Mimi niko kwenye bodi ya marafiki wa hospitali ya Shirati. Hii hospitali ilijengwa na kanisa la Mennonite katika miaka ya 40 na kwa miaka yote imekuwa inahudumiwa na michango ya kanisa. Mitambo ya x-ray, mitambo ya umeme wa jua, tunalipia sisi kutokana na michango tunayokusanya kila mwaka hapa Marekani, hasa kutoka kwa Wamarekani waliowahi kufanya kazi katika hospitali hiyo na maeneo mengineyo ya mkoa wa Mara. Bajeti yetu kila mwaka ni kama dola laki mbili. Kuna vifaa vingine tumepewa bure na baadhi ya hospitali hapa Marekani. Kazi yetu ni kuvisafirisha tu na kuhakikisha vinafika Shirati. Mkuu wa hospitali ni dakta Chirangi anayelipwa na kanisa. Serikali, miaka michache iliyopita, iliamua kuifanya hospitali hiyo kuwa ya rufaa katika mkoa wa Mara. Waliahidi kutoa madawa,na kulipa mishahara ya wafanyikazi. Sisi tutaendelea kuchangisha hela za kulipia mitambo mbalimbali. Lakini kufikia leo, 2012, serikali haijatoa dawa au malipo ya wafanyikazi. Kwa hiyo unaposema kuwa kanisa liliwekeza katika majengo tu unasema uwongo wa mchana kweupe. Kama hujui kitu ama uliza au nyamaza. Kuna madaktari wa Kimarekani hujitolea wakati wa likizo zao, kwenda kufanya kazi bure pale kwa wiki mbili au tatu kila mwaka.

Ahali yangu naona umekurupuka na kukimbilia kujibu bila kusoma nimebainisha nini.

lakin kwa kukusaidia zaidi kumbuka kuna mahospital ya taasisi za kidini lakin yanatumiwa na Serikali kama ilivyo Bugando, KCMC na nyingine za ngazi za wilayya kama ile ya kule Ngara. Hizo zinapata au wafanyakazi wake wanalipwa na Serikali na ni waajiriwa wa Serikali kuanzia madaktari, wauguzi na watu wa maabara na vile vile Serikali yenu inatoa pesa kwa ajili ya vifaa na madawa kutoka MSD.

Hizi ndio mananisa yanapokea Admin cost ambayo ndio hiyo MoU.

lakin vile kuna hospital zinazojiendesha zenyewe kama Agha Khan, Hindu mandal, na nyingine kama hiyo ulioitaja ambazo zinaendeshwa na taasisi binafsi bila kula pesa za MoU. Hospital hizo hazipati wataalamau wa Afya ambao ni waajiriwa wa Serikali ya JMTz na kila mtu analipwa na taasisi inayomiliki kama hiyo yenu.

Pole sana nisome vizuri utanielewa.

 
Ahali yangu naona umekurupuka na kukimbilia kujibu bila kusoma nimebainisha nini.

lakin kwa kukusaidia zaidi kumbuka kuna mahospital ya taasisi za kidini lakin yanatumiwa na Serikali kama ilivyo Bugando, KCMC na nyingine za ngazi za wilayya kama ile ya kule Ngara. Hizo zinapata au wafanyakazi wake wanalipwa na Serikali na ni waajiriwa wa Serikali kuanzia madaktari, wauguzi na watu wa maabara na vile vile Serikali yenu inatoa pesa kwa ajili ya vifaa na madawa kutoka MSD.

Hizi ndio mananisa yanapokea Admin cost ambayo ndio hiyo MoU.

lakin vile kuna hospital zinazojiendesha zenyewe kama Agha Khan, Hindu mandal, na nyingine kama hiyo ulioitaja ambazo zinaendeshwa na taasisi binafsi bila kula pesa za MoU. Hospital hizo hazipati wataalamau wa Afya ambao ni waajiriwa wa Serikali ya JMTz na kila mtu analipwa na taasisi inayomiliki kama hiyo yenu.

Pole sana nisome vizuri utanielewa.


Nimekusoma vizuri sana. Hukusema hivyo mwanzoni. Ulisema makanisa yalijenga majengo ya hospitali na serikali ikalipia vifaa, something which is simply not true. Hii ya kulipia wafanyikazi na madawa nimeitaja vile vile.
 
Nimekusoma vizuri sana. Hukusema hivyo mwanzoni. Ulisema makanisa yalijenga majengo ya hospitali na serikali ikalipia vifaa, something which is simply not true. Hii ya kulipia wafanyikazi na madawa nimeitaja vile vile.

Jasusi,

Nisome vizuri tena kwani mimi sikubainisha hivyo ila nimesema MAKANISA YAMEWEKEZA KATIKA KAJENGO YA HOSPITAL TU Lakin Serikali yenu ya JMTz inagharamia mishahara ya wote kuanzia madkari, wauguzi na watu wa maabara bila kusahau Vifaa na madawa ktoka bohari yenu kuu a madawa MSD.

Nisome vizuri na pasi na shaka utanielewa tu.

Pole sana
 
Sikonge,

Naona ni vizuri tuanzishe mnakasha maalum kuhusu mkoa wa Tabora kwani kuna wengi wameni PM na wengine kunipigia simu. na hii inadhihirisha kuwa JF inasomwa na wengi sana na hata katika msafara wa JK hapa Oman kuna watu waliniuliza kuwa ndie wewe barubaru
?

lakin Sikonge, ni vizuri kujua kuwa Siku zote chachu ya maendeleo inafanywa na wananchi wenyewe na SIO WAGENI. sasa wenyeji jitahidini kutoa miongozo na kujenga kwenu SIO KUOGOPA KULOGWA.
 
Hutakosea kama utasema kuwa kuna Maknisa yaliyojengwa na Mkoloni (mengine kupitia wamisionari) kwa pesa za nchi.
Lakini utakosea kama utasema kuwa kuna Misikiti ya Wakoloni, unless leo utuambie kuwa Muarabu aliwahi kuikalia Tanganyika kama koloni lake!...zile ni pesa za jasho la Waumini wenyewe aidha iwe Waarabu au Waafrika.
Hakuna mwenye shida au kelele na Shule,Mahospitali na Makanisa yaliyojengwa kwa njia hii.........ila vilivyojengwa baada ya kusainiwa MoU vinabidi kuchunguzwa kama havikutokana na pesa ya MoU moja kwa moja au faida ya biashara za Mahospitali na vyuo vilivyofaidika na MoU.

Masuala haya ni lazima yajadiliwe sasa hivi kama sio hivyo basi yatakuja kuhojiwa na vizazi vya baadaye katika lugha isiyopendeza.
Isiwe kama Nyerere ambaye alikuwa na solutions za muda mfupi katika haya masuala.

Sideeq,

..YES, Muarabu aliwahi kuikalia Tanganyika kama koloni lake.

..kuna kipindi eneo la pwani ya Afrika Mashariki lilikuwa chini ya miliki ya Sultani wa Zanzibar/Oman.

..Pia baadhi ya Watawala wa kienyeji wa Tanganyika walikuwa wanashirikiana na Waarabu ktk ukamataji wa watumwa, pamoja na uwindaji wa ndovu na faru.

..Kwasababu mhimili wa uchumi na biashara ktk Tanganyika ya zama za Mwarabu ilikuwa ni biashara ya UTUMWA kwa kweli hapo tunazungumzia DAMU na siyo jasho tu.

..Mimi nadhani tukiamua kuchunguza dini za Ukristo na Uislamu ziliingia vipi hapa Tanganyika/Afrika, na kwa malengo gani, basi tunaweza kukuta mambo ya kutia aibu na kusikitisha. Kwa mfano: maeneo kama Angola, Mreno alikuwa akikamata watumwa na kabla hajawapakiza kwenye meli watumwa wote walikuwa wakibatizwa!!

..naunga mkono hoja yako kwamba uchunguzi ufanyike kuhusu suala zima la MOU. Zaidi ijulikane kwanini MOU ililetwa wakati wa utawala wa Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Vilevile uchunguzi ufanyike ili kubaini kama kulikuwepo na ubadhirifu wa aina yoyote kwa pesa za walipa kodi kutumika kwa malengo tofauti na yale ya kutoa huduma za afya kwa jamii nzima bila ubaguzi wa kiimani, kikabila,na kijinsia.

NB:

..kuhusu NYERERE naomba nikufahamishe kwamba serikali yake ndiyo ilitaifisha shule za madhehebu ya kidini. Tena ukichunguza utakuta kwamba Wakatoliki ndiyo waliopoteza shule na hospitali nyingi kulinganisha na madhehebu mengine. Sasa hebu nieleze leo hii kama yupo kiongozi mwenye uwezo wa kufanya kama alivyofanya Mwalimu Nyerere.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom