Makanisa yavunje MoU na Serikali...

Makanisa yavunje MoU na Serikali...

Ritz,

Hakika wenzenu wanajitoa fahamu kwa hilo na kujifanya hawajui hisabu basi muwaulize hata kuhisabu hamjui.

Kama Mou Hiyo ingetumika Serikalini mpaka sasa 20 Yrs mngekuwa na hospital kubwa za level ya wilaya (kama Amana au Mwananyamala) 20 ambazo zingetapakaa nchi yenu yote na vyuo vikuu 20 ambavyo vingekuwa karibu mikoa yenu yote. Kwani kwa upande wa Serikali ya JMTz ingewatumia wataalamu wale wanaofanya kazi kwa sasa katika hospital za kanisa na vifaa vile wanavyowekeza katika hospital hizo. Nina imani hospital za kanisa nyingi zingekufa kifo cha mende.
Kumbuka KANISA LIMEWEKEZA KATIKA MAJENGO YA HOSPITAL lakin sio kwa WATAALAMU, VIFAA VYA HOSPITAL NA MADAWA. kwani vyote hivyo kwa sasa wanapata toka Serikalini.

Mnalalamikia MoU, je zile hela mlizoficha uswizi zingejenga shule na hospitali ngapi? Na yule jamaa aliyejigeuza njiwa kila siku anapaa kwa kutumia kodi zetu, je hata hiyo hamuoni kama ni hujuma. Ninyi kweli hamnazo!!!
 
Hiyo Elimu yako imekusaidia nini kama Mtanzania?Ila mbona Chadema wakiandamana na vurugu zikitokea mnailaumu Serikali?kwa kuwa leo Waumini wa Kiislam wametaka kufanya km ya Chadema basi lawama kwao,mi sioni tatizo la maandamano ya amani,ilitakiwa wapewe ulinzi waende huko wanapotaka kwenda......!!Tatizo ni Polisi!!
 
Barubaru,
Pesa nyingi sana wanapewa na serikali, halafu kuna mtu analeta hadithi za kitindiga eti hospital ya sikonge wanatibiwa bure inahusu.
agha khan pia wanapokea hela ya serikali..waislam wanashindwa nini kuingia MOU na serikali?au akili ya kuanzisha hospitali na shule hawana?hapo kwenye red,.kwa mwanaume kutumia hilo neno ni hatari!unless you are a SHE..no offence just enlighten you
 
Hiyo Elimu yako imekusaidia nini kama Mtanzania?Ila mbona Chadema wakiandamana na vurugu zikitokea mnailaumu Serikali?kwa kuwa leo Waumini wa Kiislam wametaka kufanya km ya Chadema basi lawama kwao,mi sioni tatizo la maandamano ya amani,ilitakiwa wapewe ulinzi waende huko wanapotaka kwenda......!!Tatizo ni Polisi!!
you almost convinced me...tatizo source ya maandamano yenu ndio tatizo!!mmechoma makanisa,muhuni aliyechochea na wahuni wenzie wametiwa rumande,kesho yake mnaandamana kushinikiza watoke..subirini mahakama itawapa dhamana,endeleeni na shughuli za kulijenga taifa
 
Kwa kweli ndugu yangu nakuonea huruma sana na nadhani kutokana na upeo wako kuwa mdogo ndiyo maana umeposti thread hiyo. Serikali haikulazimishwa na wakristo kuingia ktk mkataba unaoudai au kuulaumu.

Pia nadhani hata mkataba wenyewe bado hujauelewa kutokana na pointi ulizozitoa na hata hivyo waislamu hawajakatazwa kufanya mkataba na serikali bali ninachokiona hapa ni kukosa uelewa yaani elimu ya kutosha kwa ndugu zetu hawa waislamu.

Kuhusu hospitali za makanisa hakuna hata hospitali moja hapa Tanzania inayotoa tiba kwa misingi ya udini wala kutoza waumini wa kiislamu kwa bei tofauti na wanayotozwa wakristo.

Shule zilizojengwa na wakristo ziko za aina mbili seminari kwa ajili ya kuwaandaa viongozi wa kiroho pamoja na zile ambazo zinasomesha wanafunzi wa madhehebu yote.huwezi kupeleka mwanafunzi wa kiislamu kwenye shule zinazoandaa mapadre au wachungaji labda wabadili dini zao.kuhusu kodi ndugu fungua kichwa chako na uanze kufikiri deeply.

Hospitali na mashule ya wakristo hayafani biashara hiyo hutoa huduma tu sasa kama kweli akili yako iko sawa sawa utozaji kodi kwa mradi ambao hauna faida? Je, kodi hutozwa kwenye hasara.

Anzisheni shule zenu kama mnadhani mnabaguliwa pamoja na hospitali zenu. Serikali haijawakataza tatizo ni udini wenu, ufinyu wa kufikiri, kufuata mapokeo yasiyo na staha pamoja na kujikita kwenye elimu ya aina moja. Acheni mambo ya waarabu. Misaada ya waarabu itawamaliza. Someni elimu dunia nafasi za kazi zipo tu na wala hazina ubaguzi wa kidini
 
Kanisa haliwezi, na halitaweza kujiendesha bila kubebwa na serikali, Just for your information, sasa hivi hadi posho za madaktari serikali inagharamia tofauti na zamani ambapo posho zilitoka mahospitalini.

Natamani nijue elimu yako mkuu.......
kichwa chako sijui kina nini......
ukiwa a real profesional huwezi toa takataka hiyo....
 
Serikali inasaidia kutoa mchango mdogo sana kwenye huduma zote za jamii ambazo huendeshwa na private sector which include religious NGO's......
Mfano unaweza anzisha hospital,ukaiomba serikali ikuletee watumishi....ikiona inafaa huwa inafanya hivyo..ndo maana Bugando,Hydom,KCMC,Agha Khan....huwa wanapata hiyo favor
 
Sikonge,

..hata mimi naunga mkono hoja yako 100%.

..kwasababu serikali inashindwa kuchukua hatua, basi Makanisa yachukue hatua ya kuvunja MOU na serikali.

..suala hili linaleta chuki na uadui ktk taifa, kwasababu serikali imeshindwa kujitokeza na kutetea uamuzi wake wa kuingia MOU na mashirika ya dini.

NB:

..suala lingine ambalo serikali inapaswa kulitolea majibu ni huu mgogoro unaofukuta baina ya Waislamu na NECTA.
 
Last edited by a moderator:
Barubaru,
Pesa nyingi sana wanapewa na serikali, halafu kuna mtu analeta hadithi za kitindiga eti hospital ya sikonge wanatibiwa bure inahusu.

hehehe mipasho humu 'inahusu' ukubali, ukatae, ukweli ni kuwa, pale ambapo serikali haijafika na kanisa au bakwata imefika, na jengo lina ubora uliothibitika, na ukataka wananchi wote wafaidike bila kujali imani zao, ni lazima kuwe na MoU ya modality ya kufanya hayo, otherwise kwa nia njema kabisa utoke ndanda, au sikonge au rombo utembee mpaka mawenzi hospital kutibiwa na serikali, kubali , kataa ndio hivyo, waziri wa afya na naibu wake ni waislamu na rais ni muislam kama ameona economies of scale kunywa maji punguza hasira
 
Sikonge

Kwa hiyo hapa tunaongelea kuongeza gap la ubaguzi kati ya wakristo na waislam. Huoni kama huu mtindo wa sasa wa kwenda hospitali ya kanisa na kutibiwa bila kuulizwa dini yako ulikuwa unapunguza ubaguzi wa kidini? sasa hivi tukianza kuulizana dini mashuleni na hospitalini mnafikiri tutafika wapi? Kwa hakika hilo litaongeza mpasuko kuliko.

Na bahati mbaya sana serikali haina uwezo wa kusupply huduma zote ndiyo maana mashirika binafsi yameruhusiwa kutoa huduma. Hivi mahospitali makubwa kama KCMC, au PERAMIHO, mtu uulizwe dini yako, mnafikiri itakuwaje? tuache kabisa upuuzi huu!
 
Last edited by a moderator:
Sikonge

Mimi sikubaliani na wewe, kwani hii kitu MoU imejadiliwa sana ndani ya jamvi hili. MoU haiwabagui waislamu. Nawataka watoe ushahidi hapa kwamba kuna taasisi ya kiislamu inayotoa huduma za jamii imenyimwa ruzuku kwa maana ya misamaha ya kodi katika uingizaji wa vifaa vya huduma.

Usiunge mkono majungu na wivu usiokuwa na mpango!
Hawa wana agenda pana kuliko upeo wako wa kuelewa! Je makombora yanayorushwa dhidi ya Marehemu Baba wa Taifa kwamba ndo muasisi wa huo mfumo feki wanaouita Mfumo Kristo, je chuki hiyo nayo itatoka kwa kuvunja MoU?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nitonye, nafikiri unamfahamu Mkandara wa JF ambaye ni mtu anaishi nje ya Tanzania hadi sasa kama sikosei. Ni msomi mzuri tu na mtu mwenye heshima yake kubwa sana hapa JF. Mie pia nimejifunza mengi sana kwa makala zake.

Ila nakuomba uende ukurasa huu: https://www.jamiiforums.com/habari-...ofu-lakutana-mbagala-latoa-tamko-zito-11.html

Na ukishasoma Maelezo yake, nafikiri utanielewa kwa nini nilianzisha hii thread. Ukiona Wasomi wa Kiislaam wanaandika hivi, basi huko kijijini hesabu maumivu. Labda wakiona Waislaam vijijini wanabadili dini kwa wingi ili wapate huduma (Makanisa yanaweza hilo kabisa kulifanya ingawa mie SILIPENDI na ningelipenda ni SERIKALI ilifanye, ila ndiyo Serikali yenyewe hiyo tunayo) basi Wasomi hawa na hao wadhamini wao wataanza kufunguka macho.

Ni njia moja KALI sana ila nisingelipendelea kufika huko. Kama alivyosema Jasusi ni kuwa hata MOU ikivunjwa, baso watu watalialia. Ila ukweli unabaki kuwa sasa watajilaumu wenyewe.

Ni Kama Zanzibar ambavyo wanalilia kuvunja Muungano. Unawapa wajitawale kwa miaka 5 na baada ya hapo ndipo mnakutana tena mezani kama "vipi muungano uvunjwe sasa au mnarudi kuwa mkoa wa Tanzania?"

Ni kujaribu tu kuangalia kipi kifanyike ili kumaliza hizi kelele za kila siku kuhusu Mfumo Kristo ambazo hata Wasomi wazuri kama wale waliopo NSSF ila kwa kuwa wapo dini nyingine basi wamekuwa vipofu.
Mkuu wangu kwanza nashukuru umewaletea watu kitu hiki ambacho nimekisoma na kuwasoma baadhi ya watu na kwa uhakika imethibitisha UDINI uliopo nchini hauwezi kuzimwa kirahisi. wadanganyika ni WABINAFSI sijapata kuona maishani..

Mmejaribu sana kujenga hoja na hata kuendelea kuwatukana waislaam lakini, Je sii mawazo haya haya wana CCM husema kuhusu Chadema?..Iweje leo inapofikia swala la dini nyie wenyewe wana Chadema mnabadilika wakati mnajua fika CCM inawakandamiza wananchi japokuwa wapo watu watajiri na wanaofanya vizuri.. Majority ni maskini. Mbona sioni matusi haya kwa maskini wakulima na wafanyakazi ya kwamba hata wakikamatwa mafisadi bado mtaendelea kulalamika!..Nilikuwa nawaamini sana vijana wa Chadema kuwa wasomi na wenye kuelewa lakini sasa naanza kuingiwa na shaka kubwa sana..

Nimemsoma Jasusi, Mtu wangu na amenisikitisha sana kwa sababu swala sio waislaam wanataka nini isipokuwa jambo lililofanyika ni kinyume cha sheria. CSSC ni shirikisho la dini tofauti kabisa na NSSF ambalo ni shirika la Taifa na board yake inatokana na serikali iliyopo madarakani sio kama CSSC ya makanisa. Halafu maneno ya kujilinda anaposema hata MoU ikivunjwa Waislaam wataendelea kulalamika! kumbe mnajua hawa sii kama nyie eeeh! hatuko pamoja ila kuna wao na sisi. Bila shaka wataendelea kulalamika ikiwa kuna makundi na kutakuwa na jambo jingine maana nijuavyo hawajarudishiwa shule zao.

All am asking for ni fairplay. iwepo policy moja kwa wote na sio kundi la watu. kama tuna Private schools sheria zake ziwahusu shule zote za Private, ikiwa kuna ruzuku zitapewa zote kulingana na aidha wananfunzi wanaosoma pale, na muhimu zaidi serikali yetu ijikite ktk kuwalipia ada na matuzmizi wanafunzi badala ya kuziendesha shule hizo. Hivyo kila shule zita compete na real market price itajitokeza wakati huo huo serikali ikiziboresha shule zake...

Binafsi yangu naamini kabisa Tambaza ya wakati wa Nyerere sio Tambaza ya leo kiwango cha Elimu nchini kimeshuka kiasi kwamba wanafunzi wanamaliza darasa la saba wengine hawajui kusoma wala kuandika na hii ni across the board..Shule na Hospital zimekuwa utapeli mwingine ambako madawa na huduma fake zinapatikana kwa wale wasiokuwa na uwezo..
 
Uislam na Ukristo!! Memorandum of Understanding!!!! Kwani Waislam wakiagiza vifaa vinavyohusiana na huduma za kijamii wanatozwa kodi? Kodi ilifutwa kwa mashirika yote ya dini, iwe muislam au Mkristo ili mradi vifaa/bidhaa ni kwa manufaa ya jamii?!!! Hivi nani kasema serikali inapeleka tena kasma kwenye hizi hospital za kikristu? Kama ipo ni ndogo sana!! Hivi Hospital kama KCMC iliyo na component ya msamaria mwema na serikali kidogo inatibu wakristu tuu? Wanaolazwa pale ni kina Joseph na Abdala wanafukuzwa? Bugando Je? Kule Serian na Dareda hospital je?

Kwa shule za kanisa, kinachomfanya mwanafunzi aingie pale ni kufaulu!!! wanaofanya mtihani ni wakristu na waislam wanaotaka na katika ushindani wanatupwa nje!!! Mbona wakristo wako FEZA boys na wanafaulu? Mwanafunzi Bora aliyetokea FEZA si mkristu, tena mchaga!!! Sasa imefika wakati futikirie zaidi ya UKRISTU/UISLAM!! Turejeshe amani iliyokuwepo kipindi cha marehemu Baba wa Taifa na Mkapa aliwapa tena majengo ya Shule Morogoro!!!! Kwani wakati huo UKRISTU na UISLAM na hizo MOU hazikuwepo?

Haya yanayotokea leo yana mambo mazito nyuma yake na tukiyalea, wataumia wote Waislam na Wakristu!! Tujifunze kupitia huko kwa kina Boko Haramu!!! Syria, Misri, Libya japo kule Waislam ni wengi but matokeo ya vita wanayapata wote, hata wale Christian minority. Ngoja nitoke kidogo nirudi!!!!
 
hehehe mipasho humu 'inahusu' ukubali, ukatae, ukweli ni kuwa, pale ambapo serikali haijafika na kanisa au bakwata imefika, na jengo lina ubora uliothibitika, na ukataka wananchi wote wafaidike bila kujali imani zao, ni lazima kuwe na MoU ya modality ya kufanya hayo, otherwise kwa nia njema kabisa utoke ndanda, au sikonge au rombo utembee mpaka mawenzi hospital kutibiwa na serikali, kubali , kataa ndio hivyo, waziri wa afya na naibu wake ni waislamu na rais ni muislam kama ameona economies of scale kunywa maji punguza hasira
Mkuu umenena
 
Mkuu umenena vyema. Nsiande, nakugongea like!!! Hawa hawaelewi wanazungumza nini
 
Last edited by a moderator:
Mimi sikubaliani na wewe, kwani hii kitu MoU imejadiliwa sana ndani ya jamvi hili. MoU haiwabagui waislamu.
Kama wewe ungekuwa ni mgeni hapa jamvini sawa, lakini imeshajadiliwa hapa kuwa Mahospitali ya Wakristo hayawabagui Waislamu kwa sababu za kibiashara! ni kama vile wewe Mkristo uwe na duka utaikataa hela ya Muislamu? Baniani, Singasinga, Rastafarian?!
Kibaya zaidi faida yote ya mahospitali,vyuo na mashule inaenda Kanisani! wanaochangia ni wananchi wote kupitia MoU na Serikali faida inakwenda Kanisani dah! jumlisha na misamaha ya kodi.
Je makombora yanayorushwa dhidi ya Marehemu Baba wa Taifa kwamba ndo muasisi wa huo mfumo feki wanaouita Mfumo Kristo, je chuki hiyo nayo itatoka kwa kuvunja MoU?
Anataka kupewa "utakatifu" kwa ajili ya kuitumikia nchi au Kanisa? jibu tafadhali.
Huyu mtu wala usimtaje wacha watu wajadili vipi jinsi ya kujitoa kwenye hili, maana yeye (Nyerere) ndiye aliyetufikisha hapa.
Kama vile haitosha akaporomosha tusi la mwisho kwa Waislamu katika hotuba yake ya kuaga kuwa "anaondoka madarakani huku akiwa ameondoa upogo wa kielimu kati ya Waislamu na Wakristo"
 
kwa ufupi mambo mengi sana hapa tanzania yanachangiwa na serikali kudharau na uona malalamiko ya waisalmu kuwa si ya maana.hivyo basi haya yataendelea mpaka pale serikali inakaa na kuchukua maamuzi sahihi kuhusiana na malalamiko haya,pia kukamata ,kupiga,kutumia nguvu,wala sio suruhisho la jambo hili bali ni kutumia busara.
 
Uislam na Ukristo!! Memorandum of Understanding!!!! Kwani Waislam wakiagiza vifaa vinavyohusiana na huduma za kijamii wanatozwa kodi? Kodi ilifutwa kwa mashirika yote ya dini, iwe muislam au Mkristo ili mradi vifaa/bidhaa ni kwa manufaa ya jamii?!!! Hivi nani kasema serikali inapeleka tena kasma kwenye hizi hospital za kikristu? Kama ipo ni ndogo sana!! Hivi Hospital kama KCMC iliyo na component ya msamaria mwema na serikali kidogo inatibu wakristu tuu? Wanaolazwa pale ni kina Joseph na Abdala wanafukuzwa? Bugando Je? Kule Serian na Dareda hospital je?

Kwa shule za kanisa, kinachomfanya mwanafunzi aingie pale ni kufaulu!!! wanaofanya mtihani ni wakristu na waislam wanaotaka na katika ushindani wanatupwa nje!!! Mbona wakristo wako FEZA boys na wanafaulu? Mwanafunzi Bora aliyetokea FEZA si mkristu, tena mchaga!!! Sasa imefika wakati futikirie zaidi ya UKRISTU/UISLAM!! Turejeshe amani iliyokuwepo kipindi cha marehemu Baba wa Taifa na Mkapa aliwapa tena majengo ya Shule Morogoro!!!! Kwani wakati huo UKRISTU na UISLAM na hizo MOU hazikuwepo?

Haya yanayotokea leo yana mambo mazito nyuma yake na tukiyalea, wataumia wote Waislam na Wakristu!! Tujifunze kupitia huko kwa kina Boko Haramu!!! Syria, Misri, Libya japo kule Waislam ni wengi but matokeo ya vita wanayapata wote, hata wale Christian minority. Ngoja nitoke kidogo nirudi!!!!
Ndugu zangu wakristu ni lazima kwanza muelewe HOJA ya Waislaam kabla hamjatoa majibu yenu. Kwa nini mnazusha vitu ambavyo hawakusema isipokuwa mnaposikia tu maoni ya Sikonge serikali ivunje Mufaka wake na kanisa tayari mnaaza kuweweseka..

Kwanza kausome Muafaka wenyewe, halafu yasikilize malalamiko yao na ndipo unaweza kutoa jibu maana hii ya msamaha wa kodi haiwahusu waislaam na kama ipo basi ni wananchi wapenda haki na walipa kodi wanataka hivyo..Kinachogomba hapa ni serikali yetu kuingia UBIA na shirikisho la Kiimani kuendesha huduma za AFYA na ELIMU kama ilivyokuwa wakati wa Mkoloni. Mfumo huu ndio pekee unaopigiwa kelele.

Ubia baina ya serikali naKanisa ndio unaozungumziwa maana hata bajeti yetu ambayo inategemea misaada toka nje hasa ktk ELIMU na AFYA inawahusu pia kanisa ni wadau. Hivyo wao wanakatiwa na wanahusika moja kwa moja na uendeshaji wa elimu nchini kama IDARA ya serikali. Katiba yetu inasema nini? nchi yetu haina dini sasa inakuwaje chombo cha dini kinahusishwa na uendeshaji wa elimu nchini kama idara, kwa nini wao wasiwekeze ktk elimu kama biashara sawa na watu wengine ama asasi nyinginezo na walipe kodi, mahesabu yao watazamwe na mkaguzi mkuu wa serikali kama yanavyokaguliwa mashirika mengine..

Nchi zote duniani zinatoa policy moja kwa mashirika yote. Iwe ktk ELIMU au AFYA inapokuwa Private school hakuna mmoja kupendelewa zaidi ya mwingine. Shule na Hospital za makanisa zijiendeshe zenyewe kama shule za watu binafsi, kwani nako sii wanasoma watoto wote bila ubaguzi?. Halafu nimesoma mahala mtu mmoja akisema hata AghaKhan anapewa fedha hizi anapewa vipi ikiwa shule zake bado ni mali ya serikali?. Chache tu kama Mwanza sec na Tambaza ni lini huyo mdosi amerudishiwa?..Pengine kuna watu binafsi nao walitaifishwa mali zao, warudishiwe kwa wenye mali hizo ikiwa wengine wamerudishiwa.. Haki ifanyike kwa wote..
 
Ritz,

Hakika wenzenu wanajitoa fahamu kwa hilo na kujifanya hawajui hisabu basi muwaulize hata kuhisabu hamjui.

Kama Mou Hiyo ingetumika Serikalini mpaka sasa 20 Yrs mngekuwa na hospital kubwa za level ya wilaya (kama Amana au Mwananyamala) 20 ambazo zingetapakaa nchi yenu yote na vyuo vikuu 20 ambavyo vingekuwa karibu mikoa yenu yote. Kwani kwa upande wa Serikali ya JMTz ingewatumia wataalamu wale wanaofanya kazi kwa sasa katika hospital za kanisa na vifaa vile wanavyowekeza katika hospital hizo. Nina imani hospital za kanisa nyingi zingekufa kifo cha mende.
Kumbuka KANISA LIMEWEKEZA KATIKA MAJENGO YA HOSPITAL lakin sio kwa WATAALAMU, VIFAA VYA HOSPITAL NA MADAWA. kwani vyote hivyo kwa sasa wanapata toka Serikalini.

Usieneze uwongo mwingine. Mimi niko kwenye bodi ya marafiki wa hospitali ya Shirati. Hii hospitali ilijengwa na kanisa la Mennonite katika miaka ya 40 na kwa miaka yote imekuwa inahudumiwa na michango ya kanisa. Mitambo ya x-ray, mitambo ya umeme wa jua, tunalipia sisi kutokana na michango tunayokusanya kila mwaka hapa Marekani, hasa kutoka kwa Wamarekani waliowahi kufanya kazi katika hospitali hiyo na maeneo mengineyo ya mkoa wa Mara. Bajeti yetu kila mwaka ni kama dola laki mbili. Kuna vifaa vingine tumepewa bure na baadhi ya hospitali hapa Marekani. Kazi yetu ni kuvisafirisha tu na kuhakikisha vinafika Shirati. Mkuu wa hospitali ni dakta Chirangi anayelipwa na kanisa. Serikali, miaka michache iliyopita, iliamua kuifanya hospitali hiyo kuwa ya rufaa katika mkoa wa Mara. Waliahidi kutoa madawa,na kulipa mishahara ya wafanyikazi. Sisi tutaendelea kuchangisha hela za kulipia mitambo mbalimbali. Lakini kufikia leo, 2012, serikali haijatoa dawa au malipo ya wafanyikazi. Kwa hiyo unaposema kuwa kanisa liliwekeza katika majengo tu unasema uwongo wa mchana kweupe. Kama hujui kitu ama uliza au nyamaza. Kuna madaktari wa Kimarekani hujitolea wakati wa likizo zao, kwenda kufanya kazi bure pale kwa wiki mbili au tatu kila mwaka.
 
Kutokana na kulalamikiwa saana na Waislaam kuwa Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Makanisa (MOU) yanafanya nchi hii iwe na "Mfumo Kristo" na hivyo kuwanyanyasa Waislaam na hata kuwatawala, inabidi ifike wakati Makanisa yaanze kufikiria jinsi ya kuvunja mkataba huo na kurudi kama ilivyokuwa zamani.

Kwa sababu hili swala limeonakana likichochea sana vurugu, mie napendekeza lifuatalo:

- Wavunje mkataba wa MOU na Serikali.

-Waislaam wawe wanalipia gharama kwa bei ya kawaida ya kutibiwa kwenye Mahospital ya Kanisa.

-Waislaam wawe wanalipia gharama kwa bei ya kawaida ya kutibiwa kwenye Mashule ya Kanisa nk.

-Makanisa na vitengo vyake, viwe vinalipa kodi kwa kufanya biashara ya Hospitals, Shule nk.

-Gharama kwa walio Wakristo, ziwe zinapunguzwa kwa wingi kwa sababu wao hutoa michango mingi tu ya kuendeleza kanisa na sadaka za kila Jumapili.

-Kwa wasio Wakristo na hapo wanapoishi hakuna hospital ya Serikali au ya dini yao, basi itabidi wailazimishe Serikali MPYA ya Tanzania ambayo haitakuwa na Mfumo Kristo tena ili wawajengee Hospitals za Serikali.

Kama Serikali ikishindwa basi wajiandae kulipa gharama kubwa kwenye huduma hizo za jamii au KUBADILI DINI. Kama siyo hilo basi na wao na dini zao wajenge hizo huduma za jamii ili kushindana na za Makanisa.

Nafikiri muda umefika wa kuonyesha kuwa Viongozi wa Makanisa ni Wasomi wa hali ya juu na siku zote "Akili kubwa hutawala akili ndogo......" Vinginevyo, akili zao zitakuwa kazi bure kama hawawezi kutatua matatizo yaliyowazunguka.

Kama kuna kundi jingine au Serikali litakuja na mbinu mbadala na kuweka huduma hizi za jamii katika bei nafuu zaidi, basi ina maana huduma za jamii kutoka kwenye Makanisa tutakuwa hatuhitaji tena. Maendeleo yanakuja kwa mashindano. Muda umefika Makanisa kutangaza mashindano kwa kutoa huduma za JAMII VS dini nyingine au Serikali.

**************
HOJA YAKO KIASI ULICHOLENGA KIMEELEWEKA INGAWA HUKUELEWEKA KATIKA MAENEO MENGI, MFANO HAYO MAANDISHI MEKUNDU NILIYOKOLEZA. NI KWELI KWAMBA HOSPITALI ZA WAKRISTO, WAISLAMU WANALIPA GHARAMA KUBWA KULIKO WAKRISTO ? NAKUSHAURI ONGEZA MASAA YA KUFANYA KAZI ZA KUKUONGEZEA KIPATO BADALA YA KUZURULA KUANZIA J3 HADI J2 IKIWEMO SIKU YA IJUMAA. KAZI KWAKO.

Back
Top Bottom