Makanisa yavunje MoU na Serikali...

Makanisa yavunje MoU na Serikali...

kauli zingune zinaonekana kabisa ni za kibaguzi,hospitali za madhehebu ya kikristo huwa zinapokea wagonjwa wa kila aina na huwa wanatibiwa kwa gharama sawa kulingana na matatizo yanayowasibu kiafya na hawaulizwi wanasali/wanaswali dini gani.Badilika rafiki,tudumishe upendo wa kindugu bila kujali dini wala kabila.
 
makanisa yamenufaika sana na yanaendelea kunufaika na MOU pamoja na misamaha ya kodi.

Ndiomana serekali ilipojaribu kufuta misamaha ya kodi kwa taasisi za dini wakapiga kelele mpaka ikashindikana.

Serekali haijashindwa kujenga hosptali au shule, makanisa yaendeshe shule zake na hospt na yaache kutegemea kodi tunayolipa watanzania wote inufaishe watu wachache.

Tuangalie chanzo cha malalamiko ya waislam na tukitibu na sio kujaribu kutibu matokeo kama lilivyofanya tamko la maaskofu leo.

Kuishia kulaumu waislam sio suluhisho, makanisa yajitoe kwenye MOU na yasiingilie mambo ya waislam kama walivyofanya kwenye tamko lao la leo walipozungumzia suala la mwinyi kupigwa kofi au kugomea sensa.

Naomba nikusaidie kwanza ili uweze kuelewa..!!! Special Relief zilizotolewa kwenye sheria za kodi sio kwa Christian Organization bali sheria imesema "Religious Institutions". So hata waislamu wana haki ya kutumia hiyo misamaha ya kodi unless mlikuwa hamjui...!!!

Pili hivi mnajua maana ya MoU...??

Tatu; hapo kwenye bold text; una uhakika au unaishi nchi gani ndugu...??

Nafikiri ni kusoma documents zote including yale makubaliano ya serikali na nchi kadhaa then ndio tuanze kuongea...!!
 
Dr slaa, maaskofu na wakuu wa kanisa hamtaficha ukweli wa ulongo milele, hata PAPA II aliwaasa muishi vizur na waislam

kaeni mtafakari, mtoto amekojolea, umepagawa mnamvyooshea kidole kila juma, hussein, ahmada, kuweni makini sana
 
Huku ni kujikanganya. Binafsi sina pingamizi kuhusu mapendekezo yake ingawa mwisho wa siku waislamu (na wasiowaumini wa dini husika) hawatafaidika kama wanavyofaidika sasa kwa huduma kutoka wakristo + MoU.

Ukifuta MoU usizungumzie kuwa wasio wakristo watibiwe vipi katika hospitali za dini kwani baada ya kufuta MoU inabidi tuziachie dini zinazotoa huduma kuamua wenyewe pamoja na waumini wao (financiers) zitakavyoitoa huduma yao.

Swala la wahudumiwe vipi, kulipia au kutokulipia huduma halitahusu tena dini zingine. Ni kweli hata kabla ya MoU huduma za dini ya kikristo zilikuwa hazibagui ukizingatia zamani walipata misaada kutoka kwa wenzao nje ya nchi lakini kwa background hii hatujui itakuwaje. Kama alivyofafanua mwenyewe huduma hizi ni pamoja na hospitali na shule.
 
kazi kweli kweli, kwa mapendekezo yako kwa nini: waislam wachangaie gharama kidogo katika taasisi kikristo?
eehe, na sie tunaotaka kwenda kusoma Kinondoni (muislim) Secondary tulipe ada kiasi gani (ya kikristo au kiislaam?)
Hivi mgonjwa akienda hutibiwa kwa sababu ya dini yake au ugonjwa wake?
 
MOU si kwa ukristo tu na inawasaidia wananchi wengi sana na ipo kwa taasisi yoyote inayoweza sio ukristo tu. Kushirikiana na serikali ni jambo jema waislamu mjifunze hayo. TATIZO SIO MOU NI ELIMU ambayo waislamu wengi wanaianza vibaya kwa kukariri madrasa. BADILIKENI HAKUNA NAMNA.
 
Mkandara, unasema haya kwa kuwa unajisikia kusema au unasema haya kwa kuwa unaelewa hivyo? Hivi privatization ya government institutions ilikuja kutokana na nini? Kwanini sekta nyingi za serikali zilibinafsishwa, na do you real know kwamba idadi kubwa ya hospitali, na mashule makubwa ya serikali unayoyafahamu hapa nchini yalikuwa yanamilikiwa na makanisa? Mshukuruni sana Nyerere aliyeamua kuyataifisha haya mashule na mahospitali ili na ninyi waislam mpate kusoma. Vinginevyo tungeshawabatiza wote, maana ili muweze kupata elimu ya kikristo mngelazimika kubatizwa na kulishwa nguruwe.

Back to the point: kama hiyo serikali ilikuwa na uwezo wa kujenga hayo mashule na mahospitali kwanini iliyanyang'anya haya mashule na hospitali kutoka kwa wakristo? Hili si tatizo la serikali ya Tanzania tu bali ni serikali zote duniani na ni kanuni za uchumi pia, zinazosema kwamba huduma za jamii ziendeshwa na sekta binafsi halafu serikali ikusanye kodi. Hivi unataka kusema kiasi cha mchango inachotoa serikali kuendesha hospitali ya peramiho ni sawa na kiasi ambacho ingetoa kuendesha ile hospitali kama mali yake? Kwa maana ya kulipa wafanyakazi kununua madawa na ukarabati? Ndiyo maana na wewe mwenyewe unakiri kwamba shule nyingi zilizochukuliwa kutoka kwenye mashirika ya dini sasa hivi zimechoka hata hazikarabatiwi, na mahali pengine, serikali inazirudisha zile shule makanisani baada ya kuona mambo ni magumu.

Sasa wewe unaongea kitu gani kwamba eti hutarajii serikali ishindwe kutoa huduma za kijamii? So far mchango wa serikali kwenye haya mashirika hadi hivi sasa una walakini mkubwa kwa kuwa inasemekana kwamba tangu mwake 2008 (chini ya uongozi wa muislamu mwenzenu), mashirika mengi yanayotoa huduma za jamii hayajapokea ruzuku kutoka serikalini. Kwa hiyo yanachofaidi haya mashirika ni punguzo la kodi wakati wa kuingiza madawa na vipuri, ambalo hata waislam wanapata. Sasa kelele ni za nini? Mimi nafikiri ukosefu wa akili tu ndo unawasumbua waislamu.
Mkuu wangu mimi sintajibu maswali ya Kjinga kama haya ikiwa wewe Mtanzania leo unanambia mimi nimeshukuru Nyerere kwa kutaifisha mashule ya Mkoloni, halafu unataka mimi niamini kwamba mimi na wewe tuko pamoja. Shule za Mkoloni zimeshakuwa shule za Wakristu nchini wanaojiita Huru na kupongeza jitihada za wazee wetu kupigania UHURU..Hii mentality hii ndio imetufikisha hapa tulipo na UDINI unatokana na watu wenye kufikiri kama wewe. Kwa hiyo unataka kunabia kesho tukiwafukuza wae waarabu wa Loliondo mali ile itakuwa haki mali ile wapewe waislaam? Ujinga gani huu jamani na taifa gani tunalijenga ikiwa watu tunafikiri kiasi hiki...something is very wrong na education system yetu.

Ujamaa maana na lengo lake ni kuweka njia zote za Uzalishaji Uchumi zinamilikiwa na serikali - Period. Ndio mfumo tulochukua na haujalishi kama mali zilikuwa za Makanisa, Misitiki, bepari, mkoloni au nani, hivyo hata leo Saudia wakiamua kuwa Wajamaa watachukua mali za matajiri waislaam wenzao imefanyika China Urus na hata Ethiopia. Ujamaa haukulenga kuwaweka chini wakristu kwa saabu ya shule na Hospital zao... Na Privatization ni mfumo wa kiuchumi unaolenga free market economy haujalishi kama viwanda vilikuwa vinazalisha enzi ya Ujamaa au laa! Jambo nalolizungumzia mimi sio makanisa kurudishiwa mali zao, isipokuwa serikali kuingia UBIA na makanisa wakati shule na Hospital za watu wengine bado zimeshikwa na serikali na zinazofunguliwa ni Private hazina mahusiano yoyote na serikali. Huwezi kuita hii ni Privatazation ili hali serikali bado ni Mbia mkubwa wa mtaji tu pasipo ku share faida..

Nchi yoyote yenye uongozi bora hujenga SERA kwa wawekezaji wote SAWA (sheria moja) pasipo kubagua ama kupendelea. Kama shule za makanisa ni Private basi zi operate kama Private nyingine zote nchini. Kama kuna Ubia basi ubia huo uwe kwa wote maana elimu ni vita ya Kitaifa. Huu mpango wa wao kupewa fedha kuwezeshwa wao kujenga mahospital na shule kibao nchini halafu mnadai ni zenu kama mnavyojieleza humu ndilo nisililikubali. Muweza siku zote hawezeshwi yeye bali yeye ndiye husaidia, kama serikali ilishindwa kwa nini mnachukua fedha zake?.. wasaidieni wao waweze na mali hizo zijulikane ni za serikali that's only logic inayowezekana kati ya msaidiwa na msaidizi. Kodi ya Mtanzania inaendesha Hospital za makanisa mkidai ni zenu na kama sisi tuna uwezo tujenge zetu.. Hii habari ya NYIE vs SISI ndio siikubali na sitaiuna mkono..

Hata hivyo nashukuru sana kwa majibu yenu nadhani naanza kuielewa vizuri Chadema..
 
Negotiations na MOU za namna hii ziko duniani kote. mm sioni ubaya na kimsingi ilikuwa ni serikali yenyewe iliyodai kuwana MOU nao kutokana na ukweli kuwa wao walikuwa na shule nyingi na hospitali katika maeneo ambayo serikali ilikuwa haijafikishi huduma za jamii

mm nakumbuka hata JK aliwahi kuwaambia waislamu wasilalamike, kama wao wana shule na hospitali katika maeneo ambayo serikali haijafikisha huduma za afya na elimu basi wapeleke maombi serikali itayatizama watajailiana na wakikubaliana watasaini MOU. Mpaka leo hawajaenda sasa wanalalamika nini?

tuje kwenye facts waislamu ukiondoa chuo kikuu walichopewa na Mkapa ambacho kilikuwaa chuo cha TANESCO Morogoro wamejenga kingine wapi cha kwao. je wana hospitali ngapi ambazo serikali inaweza kutia mkono wake. hata shule za sekondari za maana wameshindwa kujenga na hata walizojenga zina matokeo mabaya kila mwaka, sasa wasaidiweje?

mm nafikiri waislamu waache kupiga kelele za kulalamika waangalie ni wapi wao na viongozi wao walipokosea kisha warekebishe kasoro zao
 
Mkuu wangu mimi sintajibu maswali ya Kjinga kama haya ikiwa wewe Mtanzania leo unanambia mimi nimeshukuru Nyerere kwa kutaifisha mashule ya Mkoloni, halafu unataka mimi niamini kwamba mimi na wewe tuko pamoja. Shule za Mkoloni zimeshakuwa shule za Wakristu nchini wanaojiita Huru na kupongeza jitihada za wazee wetu kupigania UHURU..Hii mentality hii ndio imetufikisha hapa tulipo na UDINI unatokana na watu wenye kufikiri kama wewe. Kwa hiyo unataka kunabia kesho tukiwafukuza wae waarabu wa Loliondo mali ile itakuwa haki mali ile wapewe waislaam? Ujinga gani huu jamani na taifa gani tunalijenga ikiwa watu tunafikiri kiasi hiki...something is very wrong na education system yetu.......
Tafadhari niombe radhi, uchadema umeingiaje hapa. Na uwaombe radhi CHADEMA kwa kuwahusisha na mijadala isiyowahusu. Unataka kusema huo msimamo wako ndiyo pia msimamo wa CUF?

Katika yote uliyosema sijaona hata hoja moja ya msingi. Na nimefuta zile fikra zangu za kwamba wewe ni msomi. Nafikiri ni just ordinary person ambaye uelewa wako upo sawa sawa na huo wa ordinary people.

Maana unashindwa kutofautisha shule za wakoloni na shule za makanisa. Wakoloni walijenga shule za serikali, na makanisa yalijenga shule za wakristo wao.

Inaonekana hata huelewi kwamba kabla ya uhuru shule ya wakatoliki walikuwa wanasoma wakatoliki, ya waanglikana ni kwa ajili ya waanglikana etc. Na serikali ya kikoloni ilikuwa na shule zake ambazo hazina uhusiano na dini yoyote. Inaonekana hilo hujui, unabwabwaja tu.
 
Tafadhari niombe radhi, uchadema umeingiaje hapa. Na uwaombe radhi CHADEMA kwa kuwahusisha na mijadala isiyowahusu. Unataka kusema huo msimamo wako ndiyo pia msimamo wa CUF?

Katika yote uliyosema sijaona hata hoja moja ya msingi. Na nimefuta zile fikra zangu za kwamba wewe ni msomi. Nafikiri ni just ordinary person ambaye uelewa wako upo sawa sawa na huo wa ordinary people. Maana unashindwa kutofautisha shule za wakoloni na shule za makanisa. Wakoloni walijenga shule za serikali, na makanisa yalijenga shule za wakristo wao. Inaonekana hata huelewi kwamba kabla ya uhuru shule ya wakatoliki walikuwa wanasoma wakatoliki, ya waanglikana ni kwa ajili ya waanglikana etc. Na serikali ya kikoloni ilikuwa na shule zake ambazo hazina uhusiano na dini yoyote. Inaonekana hilo hujui, unabwabwaja tu.
Siandiki wka ajili yako bali wengine ambao wewe umeniuliza kwanza. Nisingeandika haya kama sio wewe kunitaja miye hivyo zingatia uloyaanzisha mwenyewe . kama huliwezi joto la Jikoni ondoka mkuu wangu. Sijasema hata siku moja mimi msomi, elimu yangu ya Madrasa inanitosha kabisa kupembua pumba hizi hasa wewe unayejivunia mali ya Mkoloni na kutuletea mfumo wa kikoloni kwa kusifia Ukristu halafu unakataa sio mfumo Kristu..
 
Mkandara, Sikonge,

..yaani St.Francis, St.Andrews, Aga Khan Boys and Girls, etc etc zilizotaifishwa na Mwalimu Nyerere unaziita shule za mkoloni??! Mzee mwenzangu naomba urekebishe makosa hayo ili kuutendea haki mjadala huu.

..binafsi naomba wana JF wajielekeze kwenye historia inayohusu zoezi zima la kutaifisha shule za madhehebu ya dini. Particularly, wasome kuhusu mijadala iliyokuwa inaendelea kati ya KANISA na Mwalimu Nyerere.

..Kwa mtizamo wangu lengo la Nyerere halikuwa kuishia na kutaifisha shule za madhehebu ya dini tu, bali kujenga mfumo wa elimu ambao utakuwa sawa kwa wa-Tanzania wote. Makanisa yalikuwa yanampinga ktk azma hiyo.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu wangu mimi siwezi kubadilisha msimamo wangu. Shule na Hospital za Kanisa na AghaKhan zilikuwa za wakoloni na walikuja kuwekeza nchini ktk utawala wa mkoloni.

Hivi AghaKhan akirudishiwa hizo shule unafikiri itakuwa waislaam wamerudishiwa shule zao au ni shule zake yeye karudishiwa!. Kwa Ujinga wa baadhi yao watashangilia lakini mwenye mali ni Aghakhan wala hatuhitaji kuwa na shule za Waislaam nchini isipokuwa zile zinazofundisha dini. Nyerere alipotaifisha mashule na mali zao wote walikimbilia Edmonton, Canada akawanunulia hadi land kubwa mbona huyo Aghakhan hakuondoka na Waislaam weusi?.

Nakubaliana sana na wewe unapozungumzia mfumo wa Nyerere, huyu alipigwa na makanisa na misikiti pasipo watu kuelewa umuhimu wa zoezi lile...Na kibaya zaidi tuna watu kama kina Mohammed Said ambao wanatetea Udini, hawaijui historia ya nchi yetu ktk maswala haya wakidhania ya kwamba Nyerere aliwatenga Waislaam kumbe wale wazee waislaam wenyewe walitaka kuipeleka nchi hii upande wao pasipo kujali kuna Wakristu pia nchini..Binafsi yangu naanguka na Marehemu baba wa taifa anytime na atakuwa rohoni mwangu maisha..We will never have a leader like him..
 
Mkandara, Sikonge,

..yaani St.Francis, St.Andrews, Aga Khan Boys and Girls, etc etc zilizotaifishwa na Mwalimu Nyerere unaziita shule za mkoloni??! Mzee mwenzangu naomba urekebishe makosa hayo ili kuutendea haki mjadala huu.

..binafsi naomba wana JF wajielekeze kwenye historia inayohusu zoezi zima la kutaifisha shule za madhehebu ya dini. Particularly, wasome kuhusu mijadala iliyokuwa inaendelea kati ya KANISA na Mwalimu Nyerere.

..Kwa mtizamo wangu lengo la Nyerere halikuwa kuishia na kutaifisha shule za madhehebu ya dini tu, bali kujenga mfumo wa elimu ambao utakuwa sawa kwa wa-Tanzania wote. Makanisa yalikuwa yanampinga ktk azma hiyo.
Duh, bora unisaidie mkuu. Maana kuna watu humu ndani ni wabishi hata kama hawajui wanabishia nini!
 
Mkuu wangu mimi siwezi kubadilisha msimamo wangu. Shule na Hospital za Kanisa na AghaKhan zilikuwa za wakoloni na walikuja kuwekeza nchini ktk utawala wa mkoloni.

Hivi unafikiri AghaKhan akirudishiwa hizo shule unafikri itakuwa waislaam wamerudishiwa shule zao au ni shule zake yeye karudishiwa!. Kwa Ujinga wa baadhi yao watashangilia lakini mwenye mali ni Aghakhan wala hatuhitaji kuwa na shule za wakristu na Waislaam nchini isipokuwa zile zinazofundisha dini. Nyerere alipotaifisha mashule na mali zao wote walikimbilia Edmonton, Canada akawanunulia hadi land kubwa mbona hakuondoka na Waislaam weusi?.

Nakubaliana sana na wewe unapozungumzia mfumo wa Nyerere, huyu alipingwa na makanisa na misikiti pasipo watu kuelewa umuhimu wa zoezi lile...Na nkibaya zaidi tuna watu kama kina Mohammed said ambao hawaijui historia ya nchi yetu ktk maswala haya wakidhania ya kwamba Nyerere aliwatenga Waislaam kumbe wale wazee waislaam wenyewe walitaka kuipeleka nchi hii upande wao pasipo kujali kuna Wakristu pia nchini..Binafsi yangu naanguka na Marehemu baba wa taifa anytime na atakuwa rohoni mwangu maisha..We will never have a leader like him..
Naona hatimaye umekula matapishi yako mwenyewe kwa kukubali kwamba baba wa taifa alifanya hayo yote kuwezesha kila mtanzania bila kujali dini yake aweze kupata elimu. Nice.
 
Naona hatimaye umekula matapishi yako mwenyewe kwa kukubali kwamba baba wa taifa alifanya hayo yote kuwezesha kila mtanzania bila kujali dini yake aweze kupata elimu. Nice.
Watu wengine jamani hata hiyo shule walimu walipata taabu sana kuelezea.. yaani hadi sasa hvi hujanielewa tu.. Unaposikia ya waislaam unashangilia na kuweka wekundu lakini ya wakriustu ni meusi mazuri sana kichwnai mwako hata kama mali ile ilikuwa ya mkoloni..
 
Mkandara, Lukolo,

..unajua hii hoja yako inaweza kututoa nje ya mjadala.

..tukiendeleza hizi hoja zako tunaweza kuita shule nyingi sana, karibu zote, zilizojengwa tangu enzi za Waarabu, Wajerumani, na Waingereza, kuwa ni shule za wakoloni.

..halafu tukidai kwamba shule ni za wakoloni, what about Makanisa na Misikiti?? Je, tutakuwa tumekosea kusema kwamba kuna Misikiti na Makanisa ya wakoloni??

..for the sake of this discussion, tukubaliane tu kwamba shule za serikali ni zile zilizokuwa zikiendeshwa na serikali na kuitwa "goverment schools. Mfano wa shule hizo ni shule ya Tabora. Halafu kulikuwepo na shule za makanisa, pamoja na madhehebu mengine ya dini.

..Mwisho, kuna shule zilijengwa na madhehebu ya dini baada ya UHURU ambazo zilikuja kutaifishwa. Ndiyo maana nikaeleza kwamba utakuwa huutendei mjadala huu haki ukidai kwamba shule zilizotaifishwa zilikuwa shule za "mkoloni."

NB:

..kuna shule za madhehebu ya dini zilijengwa kwa njia ya kujitolea na waumini wa eneo husika.
 
Thanks mkuu kwa elaboration hii! Mimi nilishaamua kugive up, labda wewe atakuelewa.
 
Wewe sema unachojua. Hizo shule zilikuwa za kina nani..Walizijenga wazazi wetu?
Ninachojua ni hicho alichokieleza Joka kuu kwenye thread namba 297. Kwahiyo ukubali tu kwamba Nyerere aliwafanyia favor kwa kuwapora mashule wengine ili na wale wasio na shule zao kama waislamu wapate access kwenye shule ambazo kimsingi zilikuwa ni kwa ajili ya watu wa dini fulani tu. Huo ndo ukweli, ukubali ukatae, Nyerere aliwabeba waislam katika suala la elimu, full stop.
 
Mkandara, Lukolo,

..unajua hii hoja yako inaweza kututoa nje ya mjadala.

..tukiendeleza hizi hoja zako tunaweza kuita shule nyingi sana, karibu zote, zilizojengwa tangu enzi za Waarabu, Wajerumani, na Waingereza, kuwa ni shule za wakoloni.

..halafu tukidai kwamba shule ni za wakoloni, what about Makanisa na Misikiti?? Je, tutakuwa tumekosea kusema kwamba kuna Misikiti na Makanisa ya wakoloni??

..for the sake of this discussion, tukubaliane tu kwamba shule za serikali ni zile zilizokuwa zikiendeshwa na serikali na kuitwa "goverment schools. Mfano wa shule hizo ni shule ya Tabora. Halafu kulikuwepo na shule za makanisa, pamoja na madhehebu mengine ya dini.

..Mwisho, kuna shule zilijengwa na madhehebu ya dini baada ya UHURU ambazo zilikuja kutaifishwa. Ndiyo maana nikaeleza kwamba utakuwa huutendei mjadala huu haki ukidai kwamba shule zilizotaifishwa zilikuwa shule za "mkoloni."

NB:

..kuna shule za madhehebu ya dini zilijengwa kwa njia ya kujitolea na waumini wa eneo husika.
Mkuu wangu nadhani umeshindwa kuchanganya mchuzi huu.. Misikiti na Makanisa yalikuwa ya Mkoloni tukayachukua na hadi leo yanamilikiwa na sisi wenyewe. Iwe Msikiti wa Kitumbini japokuwa sijui ya kanisa St. Peter lakini kwa upande huu ipo misikti ilokuwa ya Mkoloni (mwarabu). Hivyo mali ilokwisha chukuliwa na Watanzania iwe kwa kutaifisha ama kuwafukuza wakoloni nchini ni mali yetu sasa hivi, hata Hiyo IKULU ni ya Mkoloni tumeichukua baada ya Uhuru na leo hii ni mali yetu.

Nachopinga mimi ni kuona leo tunamrudishia Mkoloni IKULU halafu tunashirikiana naye kuiendesha nchi kisha tunadai hatutawaliwi.. Hizi fikra ndizo zinapelekea mimi kupingana na Ubia wa aina hii baina ya serikali na Kanisa. Waislaam wana kila haki ya kulalamika kuwa wanatawaliwa ktk jambo muhimu sana kufikia maendeleo ya mtu maskini. Hata Mkoloni alitumia ELIMU na AFYA kuwa control wananchi, huu ni mfumo ulokuwepo kutokana na mahitaji ya umaskini wetu. Ukiweza kum control Maskini ktk Elimu na Afya basi umemtawala, maana atakuja tu kuomba huduma yako ili atoke, inamfanya yeye kuwa ndiye Mhitaji.
 
Back
Top Bottom