Mkuu
Sikonge,
Kwa labda nikusahihishe hizi MoU ni kwa taasisi zote ambazo si za kiserikali ziwe za kidini au kipagani inabidi zivunjwe kwa manufaa ya Taifa letu najua wadau wengi wamechangia labda nitakuwa narudia
1. MoU ni wizi tu rasiamali zetu kwa kutumia mgongo wa dini; taasisi husika zimekuwa zipokea free handout kutoka serikalini kwa kisingizio cha kupunguza gharama Za matibabu je ni kweli gharama zao ni nafuu? Si kweli hata kidogo hawana tofauti na hospitali za binafsi, ikiwa waislamu wanamudu kwenda hospitali za binafsi basi elewa fika hawatashindwa kulipia huduma za hospitali za taasisi husika.
2. Pesa wanazolipishwa wananchi zinakwenda wapi? Ni kweli pesa wanazolipa wananchi na pesa wanazopokea kutoka MoU zote zinakwenda kwenye kupunguza gharama za matibabu? Hayo si kweli taasisi husika zinatumia udhaifu wa serikali pesa hizo hizo ndizo zinazotumika kwenye miradi mengine ya elimu; ukichunguza kwa makini taasisi husika zimeweza kuongeza idadi ya mashule na vyuo baada ya mfumuko wa pesa MoU tusidanganyane eti ni pesa za sadaka za waumini.
3. Ikiwa hizi ni taasisi za kidini zinafanya kazi ya Mungu kuna ulazima gani wa wao kuchukua pesa kutoka serikalini? Hapo thawabu inapata serikali au taasisi husika? Yaani ni sawa kwa muumini aliyeshindwa kwenda kwenye sala na kumupa pesa jirani akamtolee sadaka.
3. Ukirudi kwenye hizi handout waathirika sio waislamu pekee wapo wakristo wengi tu waathirika wa wizi huu; inakuwaje taasisi husika zinachangia kujenga matabaka kwenye jamii? Ni kichekesho kwani hata hapa US upuuzi huu uliachwa siku nyingi zipo taasisi za kweli za kidini hatozi ada yoyote kwenye matibabu;inakuaje Tanzania tumeuzwa wajinga kiasi hiki kutetea upuuzi ambao athari zake ni kuja kuuana uvumilivu una kikomo; wana historia someni mapinduzi ya ulaya yalitokana na nini?
Niwahi kufanya kazi kwenye taasisi ya kidini hapa US kila mwisho mwaka kila mfanyakazi anapewa bonus kati dola 1000-700 baada yakutoa gharama zote kinachobaki kinagiwa wafanyakazi kwasababu zipo chini not for profit organization je hicho ndicho kinachoafanyika hapo Tanzania!Ningeomba nyie washabiki wakubwa mmoja wenu ende kwenye hospitali mnazozitetea aombe kutibiwa bila pesa halafu arudi hapa jamvini atueleze hatima yake.
Chama
Gongo lamboto DSM