jamani tupeleke watoto wetu shule kwa manufaa yao ya baadaye. Ujinga ni bidhaa aghali mno jamani. ni heri ufe lofa kabisa lakini ufe ukiwa umeelimika....by the way wakati tunawakumbusha wale walio nyuma kielimu kugutuka na kukaza buti, tuwakumbushe pia ku-review mifumo yao ya maisha na kuangalia ni kwa jinsi gani wata-adjust mahusiano ya dini zao na ilmu dunia.
Kusoma ni aghali sana siku hizi. ili uweze kumudu lazima ufanye plans ikiwa ni pamoja na kuwa na idadi ndogo ya watoto ili uweze kumudu gharama. sasa kama wewe unajikusanyia ving'asti hadi dala na kuendelea, assuming kuwa kila king'ast akikutotolea dabo, ina maana una kumi halafu wamefuatana, ajira yako unayofanya ni jembe la mkono..haya utamudu?!! nyerere alisema ili tuendelee tunahitaji mambo manne: watu, ardhi siasa safi na uongozi bora. shule za kanisa zinafundisha kuwa ili wanafunzi wafanikiwe wanahitaji mambo mawili......KAZI na SALA.
Waislmu ndugu zanguni ili kufanikiwa sala peke yake hazitoshi japo ni muhimu pia (kutegemeana na imani yako). Salini sana jamani lakini msishau na KAZI. Na ninaposema KAZI ni pamoja na kazi ya kutafuta ILMU DUNIA. acheni perepende mingi, chacharkeni aisee, mbbllahh!! la sivyo hawa wakirisito mtawaskia kwenye bomba tena la maji machafu. wakti nyie mnapiga perepende ya mtoto aliyekojolea kitabu wakti akicheza na mwenzake, wenzenu wameshatua huko mars aisee, kweli papaangu nawaambia!!!!!........haya, mi ndo hifoo nimeshasema, mwenye maskio na askiiii.....askie kweliiii. mi ngoja nkatafute pesa aisee....