Makanisa yavunje MoU na Serikali...

Makanisa yavunje MoU na Serikali...

Sideeq,

..YES, Muarabu aliwahi kuikalia Tanganyika kama koloni lake.

..kuna kipindi eneo la pwani ya Afrika Mashariki lilikuwa chini ya miliki ya Sultani wa Zanzibar/Oman.
Hakuja kama Mkoloni! aliitwa na WaKilwa kuja kusaidia kumng"oa Mreno ambaye aliivamia Islamic State ya Kilwa na kutaka kulifanya taifa la Kikristo.
Baada ya kumng`oa Mreno wakakubaliana na watu wa Zenj abakie katika hili eneo kwa ajili ya kuunusuru Uislamu dhidi ya Mreno ambaye aliingilia Kilwa mara mbili.
JokaKuu said:
..Pia baadhi ya Watawala wa kienyeji wa Tanganyika walikuwa wanashirikiana na Waarabu ktk ukamataji wa watumwa, pamoja na uwindaji wa ndovu na faru.

..Kwasababu mhimili wa uchumi na biashara ktk Tanganyika ya zama za Mwarabu ilikuwa ni biashara ya UTUMWA kwa kweli hapo tunazungumzia DAMU na siyo jasho tu.
Unazungumzia kipindi kabla ya mapinduzi ya viwanda hivyo uuzaji na ununuaji wa binadamu kwa ajili ya kazi ambazo nyingi sasa hivi zinafanywa na mashine ilikuwa na maridhiano ya pande zote kama ulivyoonyesha mwenyewe kuwa hata Waafrika pia waliuza na kumiliki watumwa/wafanyakazi.
Hili la uwindaji wa ndovu na faru inabidi ulithibitshe JokaKuu.
 
Sideeq,

..YES, Muarabu aliwahi kuikalia Tanganyika kama koloni lake.

..kuna kipindi eneo la pwani ya Afrika Mashariki lilikuwa chini ya miliki ya Sultani wa Zanzibar/Oman.

..Pia baadhi ya Watawala wa kienyeji wa Tanganyika walikuwa wanashirikiana na Waarabu ktk ukamataji wa watumwa, pamoja na uwindaji wa ndovu na faru.

..Kwasababu mhimili wa uchumi na biashara ktk Tanganyika ya zama za Mwarabu ilikuwa ni biashara ya UTUMWA kwa kweli hapo tunazungumzia DAMU na siyo jasho tu.

..Mimi nadhani tukiamua kuchunguza dini za Ukristo na Uislamu ziliingia vipi hapa Tanganyika/Afrika, na kwa malengo gani, basi tunaweza kukuta mambo ya kutia aibu na kusikitisha. Kwa mfano: maeneo kama Angola, Mreno alikuwa akikamata watumwa na kabla hajawapakiza kwenye meli watumwa wote walikuwa wakibatizwa!!

..naunga mkono hoja yako kwamba uchunguzi ufanyike kuhusu suala zima la MOU. Zaidi ijulikane kwanini MOU ililetwa wakati wa utawala wa Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Vilevile uchunguzi ufanyike ili kubaini kama kulikuwepo na ubadhirifu wa aina yoyote kwa pesa za walipa kodi kutumika kwa malengo tofauti na yale ya kutoa huduma za afya kwa jamii nzima bila ubaguzi wa kiimani, kikabila,na kijinsia.

NB:

..kuhusu NYERERE naomba nikufahamishe kwamba serikali yake ndiyo ilitaifisha shule za madhehebu ya kidini. Tena ukichunguza utakuta kwamba Wakatoliki ndiyo waliopoteza shule na hospitali nyingi kulinganisha na madhehebu mengine. Sasa hebu nieleze leo hii kama yupo kiongozi mwenye uwezo wa kufanya kama alivyofanya Mwalimu Nyerere.

jokaKuu,
Naomba umuelimishe Sideeq kuwa hakuna kanisa hata moja lililojengwa na serikali ya mkoloni. Makanisa yote Tanzania yamejengwa na fedha za mission societies katika nchi walikotoka, iwe Moravian, CMS, SDA, Lutheran, Catholic, hakuna hata senti moja iliyotolewa na serikali ya mkoloni kujenga makanisa hayo na hospitali. Walichofanya wakoloni ni kuwagawia maeneo na viwanja tu basi. Hawakutoa hata senti tano.
 
Ina maana unataka kuniambia kuwa pamoja na usomi wako huo umeshindwa kujua kuwa Wakoloni kila wanapokwenda wanakwenda na Wamisionari?! umeshindwa kujua kuwa Tanganyika pia walikuja pamoja na Wamisheni?
Umesema kuwa Wakatoliki walikuwa wakisoma shule za Kikatoliki, Waanglikana wanasoma Shule za Kianglikana hujasema pesa za ujenzi na uendeshaji zilitoka wapi, na ni katika mwaka gani Kanisa lilitenganishwa na Serikali!
Tunakwenda sehemu nzuri ambapo utakuja kujihakikishia kuwa MoU ni muendelezo wa ukoloni hasa ukizingatia kuwa aliyeshiriki kuuratibu ni former colonial Master (Mjerumani)
......kajipange!
Wewe ndiye unayehitaji kujipanga. Wakoloni hawakuambatana na wamishenari katika colonization yao. Ingekuwa ni hivyo, Tanzania nzima ingekuwa ni Anglican na Lutheran peke yake. Lakini kuna Moravian, nadhani hawa wametoka nchi za Scandinavia, kuna Wakatoliki, hawa wengi wao ni Wataliani, sasa iweje wamishenari wa Kimarekani nao waruhusiwe kuleta makanisa yao Tanganyika wakati ilikuwa ni koloni ya Uingereza? Kajipange wewe!
 
ebu sikilizeni niwaambie nyie WAKRISTO naomba mufaham kua waislamu wameamka na wanaelewa jinc gani mambo yanavoenda hakuna hasiefahamu dini ya kikristo inavobebwa na serikali katka nyanja mbalimbali za maisha nchini na kinachonickitisha ni kwamba hamjui kusoma alama za nyakati kwa kung"ang"ania kulazimisha watu wataje njano hali ya kua ni nyekundu na kusahau kua waislam cku moja moja watazinduka na kuhoji mambo yanvoenda.kwa nia njema naomba nawakumbushe kutumia plopaganda i.e waislam wanavunja amani ya nchi,waislam ni maghaid n.k c suluhisho la matatizo tuliyonayo kwani hata waandishi mbalimbali wa dini yenu kama DR. JOHN SIVALON wameelezea kwa kina suala hilo.PIA niwakumbushe kua hakuna mtu hasiye na uchungu na dini yake na acheni mchezo na imani za watu vile vile naomba mtambue kua hakuna mtu yeyote anayependa kuona nchi yetu inaingia kwenye machafuko na MOLA IBARIKI TANZANIA ila mi ninaamini kwa misingi hii ya makanisa kutaka kuiongoza nchi kwa manufaa yao itabadilisha HISTORIA ya nchi yetu mda c mrefu na mkitaka kulifahamu hilo tembeleeni kwenye mtandao na mcheki THE POLITICAL FUTURE OF TANZANIA.Haipingiki kusema kusema NYERERE kafanya jitihada kubwa kuliweka kanisa mahala hapo mlipo ktk nchi ila mi ninaamini WAKRISTO mda c mrefu mtakuja kulia kwa kusaga meno huku mkijuta kwa nini NYERERE alichukua uamuzi kama huu na hii ni kutokaka na expirience yangu ya kusoma alama za nyakati.Nawaomba ndugu zangu muamke na maunglie nini cha kufanya kwa usalama wa dini yenu na kwa usalama wa nchi yetu TANZANIA,Nawaomba msiwe kama NYERERE ambaye alitumia mda wake wa uongozi kuwapumbaza watu waamini njano ni nyekundu na nyekundu ndo njano kama alivofanya BI KILEMBWE ktka nchi ya GININGI kuwalazimisha watu waamini kitu kisicho sahihi ikibidi kwa kuwaua watu wenye mawazo tofauti na yeye na mwisho wake kujikuta anasalitiwa mpaka na viungo vyake vya mwili.
'MUNGU IBARIKI TANZZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA"

Unatutisha?
 
jokaKuu,
Naomba umuelimishe Sideeq kuwa hakuna kanisa hata moja lililojengwa na serikali ya mkoloni. Makanisa yote Tanzania yamejengwa na fedha za mission societies katika nchi walikotoka, iwe Moravian, CMS, SDA, Lutheran, Catholic, hakuna hata senti moja iliyotolewa na serikali ya mkoloni kujenga makanisa hayo na hospitali. Walichofanya wakoloni ni kuwagawia maeneo na viwanja tu basi. Hawakutoa hata senti tano.
Ni vizuri kuwa umekiri kiaina kuwa Wakoloni na Wamisionari walikuwa wakishirikiana! na ardhi ile ya Makanisa ilitolewa na Mkoloni kwa Wakristo bila ya idhini ya raia.

Sasa tunataka ututhibitishie vipi Mkoloni Mjerumani kama ni Mlutheran asijenge Kanisa la Kilutheran kwa pesa ya nchi.
Halafu akaja Muingereza, vipi naye ajenge Kanisa la Kianglikana bila ya pesa za nchi? Mreno naye alikuwepo...
 
Nikuthibitishie vipi kuwa serikali ya Ujerumani haikutumia fedha za koloni lake kujenga makanisa? Soma historia ya makanisa Tanzania ujue yalijengwa kwa fedha za nani. Siyo kukurupuka tu na dhana kwamba wakoloni walijenga makanisa. Hawakujenga. Kulikuwa na Missionary societies ambazo zimejenga makanisa kwa hela za waumini wa nchi hizo.
 
Jasusi,

Moravian pia ni German. Ila asili hasa ni Czech, sehemu iitwayo Moravia.

Waczech walipoanza upagani, wakafukuza dini zote au kupiga marufuku.

Soma: Moravia - Wikipedia, the free encyclopedia
Wewe ndiye unayehitaji kujipanga. Wakoloni hawakuambatana na wamishenari katika colonization yao. Ingekuwa ni hivyo, Tanzania nzima ingekuwa ni Anglican na Lutheran peke yake. Lakini kuna Moravian, nadhani hawa wametoka nchi za Scandinavia, kuna Wakatoliki, hawa wengi wao ni Wataliani, sasa iweje wamishenari wa Kimarekani nao waruhusiwe kuleta makanisa yao Tanganyika wakati ilikuwa ni koloni ya Uingereza? Kajipange wewe!
 
Kwa nini Pro-Chadema wengi uwa wanakuwa upande wa CCM linapokuja suala la MoU... halafu hapo hapo eti wana mawazo ya kuing'oa CCM madarakani wanachekesha sana.
 
Nikuthibitishie vipi kuwa serikali ya Ujerumani haikutumia fedha za koloni lake kujenga makanisa? Soma historia ya makanisa Tanzania ujue yalijengwa kwa fedha za nani. Siyo kukurupuka tu na dhana kwamba wakoloni walijenga makanisa. Hawakujenga. Kulikuwa na Missionary societies ambazo zimejenga makanisa kwa hela za waumini wa nchi hizo.
Ungesoma kitabu cha P.Bergen anaposema kuwa kama si Serikali basi Makanisa yangekuwa hoi,hii ni baada ya Uhuru.
Kabla ya uhuru kanisa lilikuwa ndio serikali, wakati huo Kanisa lilikuwa halitenganishwi na Serikali.
Jasusi said:
Wewe ndiye unayehitaji kujipanga. Wakoloni hawakuambatana na wamishenari katika colonization yao. Ingekuwa ni hivyo, Tanzania nzima ingekuwa ni Anglican na Lutheran peke yake. Lakini kuna Moravian, nadhani hawa wametoka nchi za Scandinavia, kuna Wakatoliki, hawa wengi wao ni Wataliani, sasa iweje wamishenari wa Kimarekani nao waruhusiwe kuleta makanisa yao Tanganyika wakati ilikuwa ni koloni ya Uingereza? Kajipange wewe!
Je unajua kuwa wakati Mreno alipotia mguu wake ilikuwa tayari ameshatia saini ya makubaliano na Kanisa Katoliki kuueneza ukatoliki popote anapokwenda?
 
Hakuja kama Mkoloni! aliitwa na WaKilwa kuja kusaidia kumng"oa Mreno ambaye aliivamia Islamic State ya Kilwa na kutaka kulifanya taifa la Kikristo.
Baada ya kumng`oa Mreno wakakubaliana na watu wa Zenj abakie katika hili eneo kwa ajili ya kuunusuru Uislamu dhidi ya Mreno ambaye aliingilia Kilwa mara mbili.Unazungumzia kipindi kabla ya mapinduzi ya viwanda hivyo uuzaji na ununuaji wa binadamu kwa ajili ya kazi ambazo nyingi sasa hivi zinafanywa na mashine ilikuwa na maridhiano ya pande zote kama ulivyoonyesha mwenyewe kuwa hata Waafrika pia waliuza na kumiliki watumwa/wafanyakazi.
Hili la uwindaji wa ndovu na faru inabidi ulithibitshe JokaKuu.
Sideeq,

..ndugu yangu, hata Tanzania tuliitwa Ushelisheli kuwasaidia wakati makaburu walipojaribu kuwavamia. Lakini hukusikia Mwalimu Nyerere akihamisha makao makuu toka Dodoma kupeleka Port Victoria baada ya JWTZ kuwatimua makaburu.

..zaidi, Muarabu alijimilikisha eneo zima la pwani ya Afrika Mashariki mpaka alipokuja kuporwa na wazungu. Vilevile Waarabu alikuwa wakifanya vurugu[terror] kubwa sana ktk interior of Tanganyika mpaka Congo ambapo walikuwa vinara/wamiliki wa njia za kusafirisha WATUMWA.

..NOW, tunaweza tusikubaliane ktk mambo mengi, lakini nadhani hakuna mashaka yoyote kwamba DINI hizi mbili zililetwa katika zama za UKATILI na UDHALILISHAJI mkubwa kwetu sisi WAAFRIKA. Wakati mwingine huwa nawaza kama kweli MUNGU alikua na nia Waafrika nao wawe waumini wa dini hizi.
 
Last edited by a moderator:
jokaKuu,
Naomba umuelimishe Sideeq kuwa hakuna kanisa hata moja lililojengwa na serikali ya mkoloni. Makanisa yote Tanzania yamejengwa na fedha za mission societies katika nchi walikotoka, iwe Moravian, CMS, SDA, Lutheran, Catholic, hakuna hata senti moja iliyotolewa na serikali ya mkoloni kujenga makanisa hayo na hospitali. Walichofanya wakoloni ni kuwagawia maeneo na viwanja tu basi. Hawakutoa hata senti tano.

Jasusi,

..I dont have enough materials on that.

..lakini kuna mahali nilisoma kwamba kazi za Wamisionari wa Kijerumani zilisitishwa hapa Tanganyika baada ya Muingereza kushika hatamu.

..pia ukisoma historia ya uhuru utaona kwamba wamisionari wa Mary Knoll wakimuunga mkono Nyerere ktk harakati za uhuru.

..zaidi, ni kwanini Waanglikani hawana nguvu hapa Tanganyika kulinganisha na Wakatoliki au Walutheri?? U would expect Waanglikani wawe wengi ukizingatia kwamba mtawala wa mwisho alikuwa Muingereza.

..Mwisho, nadhani turudi tu kwenye mada ambayo ni pendekezo la Sikonge kwamba MOU kati ya serikali na makanisa ifutwe. Mimi nadhani MOU inaleta uhasama na chuki zisizo na ulazima. Badala ya Waislamu kuiandama serikali iboreshe huduma za afya, wanayaandama makanisa na Wakristo.

..Sasa bora makanisa yajitoe ili tuweze kumjua mbaya wetu ni MOU au ni uzembe tu wa serikali na chama tawala.
 
..ndugu yangu, hata Tanzania tuliitwa Ushelisheli kuwasaidia wakati makaburu walipojaribu kuwavamia. Lakini hukusikia Mwalimu Nyerere akihamisha makao makuu toka Dodoma kupeleka Port Victoria baada ya JWTZ kuwatimua makaburu.
Wareno waliivamia Kilwa mara ya kwanza ambapo walitolewa kwa msaada wa Waturuki na kukimbilia Mombasa, mara baada ya waturuki kuondoka kurejea makwao Mreno alirejea tena hivyo safari hii akaitwa Sultan wa oman kuja kumng`oa na kubakia Zenj ili kuulinda Uislamu dhidi ya Wareno, tofauti na Shelisheli ambayo sikumbuki kuvamiwa mara mbili tofauti na makaburu.
JokaKuu said:
Vilevile Waarabu alikuwa wakifanya vurugu[terror] kubwa sana ktk interior of Tanganyika mpaka Congo ambapo walikuwa vinara/wamiliki wa njia za kusafirisha WATUMWA.
..NOW, tunaweza tusikubaliane ktk mambo mengi, lakini nadhani hakuna mashaka yoyote kwamba DINI hizi mbili zililetwa katika zama za UKATILI na UDHALILISHAJI mkubwa kwetu sisi WAAFRIKA. Wakati mwingine huwa nawaza kama kweli MUNGU alikua na nia Waafrika nao wawe waumini wa dini hizi
Sikutegemea kama mtu kama wewe angeandika hoja dhaifu, duni na isiyo na mshiko kama hii:
Umetaja Waarabu kufanya vurugu (acha tuseme walifanya) halafu unawanasibisha Waarabu hao na Uislamu kama vile ambae hujui kuwa katika Waarabu kuna Wakristo, Mayahudi, Wapagani n.k!!
 
Wareno waliivamia Kilwa mara ya kwanza ambapo walitolewa kwa msaada wa Waturuki na kukimbilia Mombasa, mara baada ya waturuki kuondoka kurejea makwao Mreno alirejea tena hivyo safari hii akaitwa Sultan wa oman kuja kumng`oa na kubakia Zenj ili kuulinda Uislamu dhidi ya Wareno, tofauti na Shelisheli ambayo sikumbuki kuvamiwa mara mbili tofauti na makaburu.Sikutegemea kama mtu kama wewe angeandika hoja dhaifu, duni na isiyo na mshiko kama hii:
Umetaja Waarabu kufanya vurugu (acha tuseme walifanya) halafu unawanasibisha Waarabu hao na Uislamu kama vile ambae hujui kuwa katika Waarabu kuna Wakristo, Mayahudi, Wapagani n.k!!

Waaraabu waliokuja Tanganyika walikuwa wote Waislamu. Hili halina ubishi.
 
Sideeq,

..hebu nieleze ni wapi hapa Tanganyika ambapo Waarabu walieneza Ukristo, Uyahudi, au Upagani, ili tuweze kuwanasibisha na imani hizo.

..kuhusu Sultani na kuhamia Zanzibar, bila shaka alifanya hivyo kutokana na kishawishi cha biashara ya WATUMWA pamoja na pembe za ndovu.
 
Last edited by a moderator:
Sikonge, kwa nini wavunje? Mimi naona kuwa hili ni Hannity zuri linalofaa kuigwa. Hivyo ushauri wangu ni Huu-nendeni shule mkapate elimu ya kuweza kuandika proposal kuomba makubaliano na serikali.
 
Last edited by a moderator:
Usichangie hoja hii kwa kuirukia, isome na uelewe context
kwa nini wavunje? Mimi naona kuwa hili ni Hannity zuri linalofaa kuigwa. Hivyo ushauri wangu ni Huu-nendeni shule mkapate elimu ya kuweza kuandika proposal kuomba makubaliano na serikali.
 
Mkuu Sikonge,

Kwa labda nikusahihishe hizi MoU ni kwa taasisi zote ambazo si za kiserikali ziwe za kidini au kipagani inabidi zivunjwe kwa manufaa ya Taifa letu najua wadau wengi wamechangia labda nitakuwa narudia

1. MoU ni wizi tu rasiamali zetu kwa kutumia mgongo wa dini; taasisi husika zimekuwa zipokea free handout kutoka serikalini kwa kisingizio cha kupunguza gharama Za matibabu je ni kweli gharama zao ni nafuu? Si kweli hata kidogo hawana tofauti na hospitali za binafsi, ikiwa waislamu wanamudu kwenda hospitali za binafsi basi elewa fika hawatashindwa kulipia huduma za hospitali za taasisi husika.

2. Pesa wanazolipishwa wananchi zinakwenda wapi? Ni kweli pesa wanazolipa wananchi na pesa wanazopokea kutoka MoU zote zinakwenda kwenye kupunguza gharama za matibabu? Hayo si kweli taasisi husika zinatumia udhaifu wa serikali pesa hizo hizo ndizo zinazotumika kwenye miradi mengine ya elimu; ukichunguza kwa makini taasisi husika zimeweza kuongeza idadi ya mashule na vyuo baada ya mfumuko wa pesa MoU tusidanganyane eti ni pesa za sadaka za waumini.

3. Ikiwa hizi ni taasisi za kidini zinafanya kazi ya Mungu kuna ulazima gani wa wao kuchukua pesa kutoka serikalini? Hapo thawabu inapata serikali au taasisi husika? Yaani ni sawa kwa muumini aliyeshindwa kwenda kwenye sala na kumupa pesa jirani akamtolee sadaka.

3. Ukirudi kwenye hizi handout waathirika sio waislamu pekee wapo wakristo wengi tu waathirika wa wizi huu; inakuwaje taasisi husika zinachangia kujenga matabaka kwenye jamii? Ni kichekesho kwani hata hapa US upuuzi huu uliachwa siku nyingi zipo taasisi za kweli za kidini hatozi ada yoyote kwenye matibabu;inakuaje Tanzania tumeuzwa wajinga kiasi hiki kutetea upuuzi ambao athari zake ni kuja kuuana uvumilivu una kikomo; wana historia someni mapinduzi ya ulaya yalitokana na nini?

Niwahi kufanya kazi kwenye taasisi ya kidini hapa US kila mwisho mwaka kila mfanyakazi anapewa bonus kati dola 1000-700 baada yakutoa gharama zote kinachobaki kinagiwa wafanyakazi kwasababu zipo chini not for profit organization je hicho ndicho kinachoafanyika hapo Tanzania!Ningeomba nyie washabiki wakubwa mmoja wenu ende kwenye hospitali mnazozitetea aombe kutibiwa bila pesa halafu arudi hapa jamvini atueleze hatima yake.

Chama
Gongo lamboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini Pro-Chadema wengi uwa wanakuwa upande wa CCM linapokuja suala la MoU... halafu hapo hapo eti wana mawazo ya kuing'oa CCM madarakani wanachekesha sana.

Kuna MOU pia katk ya mashirika ya Kikristu(makanisa) na misikiti katik maeneo ya HIV,education centres, and other medical services(world Vision,Compassion,CRS) wilaya ya pwani,zenj ,lindi na Tanga sehemu Wakristu hawana makanisa au wakristu. Nayo unasemaje?
 
A bunch of jib jabber!!! Tunalipa kodi ili serikali ifanye kazi gani? Nduguzetu wakristo hii Memorandum of Understanding ni wizi na ufisadi na hizo Trillioni za 3 mlizochukua kutoka katika kodi ya waislamu zitawatokea puani. Waislamu wanaanza kufahamu mchezo wa kuigiza unaondelea hamundanganyi mtu sasa hivi. Nimejadiliana na nyie katika thread iliyopita kule Jamii Intelligence nikitegemea kuna mtu atakuja na hoja ya msingi but sijaiona mpaka sasa.

Narudia tena MOU ni ufisadi kwasababu hela inayokwenda kule ni kama sadaka ya serikali kanisani period!!!! Sasa kodi yangu mie mwislamu inaenda kufanya nini kanisani?

unafahamu World Vision,CRS,compassion,red cross hela zao zinatoka nje mojakwa moja?Na miradi inayooombewa hela nje ya nchi ?Nilidhani unafahamu usemacho hapa kumbe unategemea tukwambie halafu ndipo u apply taarifa za ponda.Sasa msikiti utatokaje kwenya hivi vimikataba?
 
A bunch of jib jabber!!! Tunalipa kodi ili serikali ifanye kazi gani? Nduguzetu wakristo hii Memorandum of Understanding ni wizi na ufisadi na hizo Trillioni za 3 mlizochukua kutoka katika kodi ya waislamu zitawatokea puani. Waislamu wanaanza kufahamu mchezo wa kuigiza unaondelea hamundanganyi mtu sasa hivi. Nimejadiliana na nyie katika thread iliyopita kule Jamii Intelligence nikitegemea kuna mtu atakuja na hoja ya msingi but sijaiona mpaka sasa.

Narudia tena MOU ni ufisadi kwasababu hela inayokwenda kule ni kama sadaka ya serikali kanisani period!!!! Sasa kodi yangu mie mwislamu inaenda kufanya nini kanisani?

Mdondoaji ni CCM ndiyo imefanya haya yote; mwaka 2010 kundi la watu (wakiwemo Waislamu wengi tu) walitaka CCM irudi madarakani. Sasa hilo la MoU siyo la Wakristu ni la serikali ya CCM. Imeshaoneshwa huko nyuma ni Ally Hassan Mwinyi (Muislamu) ambaye aliingia mkataba huo na wakati wanaingia na kanisa walifanya pia na Imam Aga Khan (Muislamu). Hicho kilichoingiwa kwa Kanisa kiliingiwa na kwa Aga Khan na taasisi yake inafanya karibu mambo yale yale ambayo yanafanywa na makanisa (elimu, shule n.k).

Ni kweli wakiamua kuvunja hii MoU isiwe nusu nusu; ihusishe na hizi taasisi nyingine lakini kama watu kweli wanataka an absolute secularization ya serikali yetu wasiishie hapo waende mbele zaidi.
 
Back
Top Bottom