Tatizo la waislamu lipo karibu kwa watu wote, WALIOSOMA NA WASIOSOMA. Wakati unategemea waliosoma wawasaidie ambao hawajasoma unakuta na wao wakiwa kwenye vikao vyao wote wanawaza vilevile. Mapendekezo ya mtoa mada siyo tu ni ya kitoto bali pia yanaonesha ni ya mtu aliye soma lakini ameamua kufikiri kama wasio soma.
NI KAMA ANAPENDEKEZA KUWAWALIO ENDELEA WAWASUBIRI WALIO NYUMA KIMAENDELEO.
Waislamu walio wengi elimu kwao ni kama anasa. Ukiangalia maeneo yaliyo na waislamu wengi mahudhurio ya watoto wao shuleni yako chini ya asilimia 50. Ukienda BAGAMOYO, CHALINZE, LINDI YOTE, MTWARA YOTE KASORO MASASI, siku mvua ikinyesha tu asubuhi mahudhurio yanashuka hadi asilimia 25!! Hali kama hiyo huwezi kuikuta Kilimanjaro, Mbeya, Shinyanga, Iringa, Ruvuma, na maeneo yote ya wakristo wengi.
Kama wakitambua kuwa elimu ni ufunguo wa maisha basi ungetegemea kuona wanajenga shule nyingi zenye ubora wa hali ya juu na kuimarisha uongozi wa shule zao sambamba na kutafuta walimu wenye sifa nzuri kitaaluma na siyo kiroho tu. Shule zao siyo tu zinatia huruma lakini pia nyingi zinaendeshwa kimagumashi. Karibu zote wastani wa kufaulisha watoto kwenda kidato cha tano ni asilimia kati ya 2 hadi 5 tu.
USHARI WANGU NI wajitathini wenyewe kwanza.