Makamu wa Rais anaeweza kukaa nje ya nchi kwa mwezi mmoja kwa shughuli maalamu?

Makamu wa Rais kazi yake ni kumsaidia Rais, nikijibu swali lako Makamu wa Rais anaweza kukaa nje ya nchi hata zaidi ya mwezi, kwa sababu yeye ni msaidizi tu, hasa Rais anapokuwa hayupo nchini au anadharula nyingine ya kikazi au kibinaadamu.

Utaona kazi zote ni za Rais, Makamu ni msaidizi hivyo umuhimu wake upo katika nafasi hiyo. Yeye sio muhimu kuwepo nchini muda wote, hasa pale Rais anapokuwa na uwezo wa kuyasimamia majukumu yote ndani ya nchi.

Hata hivyo Rais anawasaidizi wengi, yupo waziri mkuu, Makamu waziri mkuu na wengine wengi. Ukiangalia nafasi ya Makamu wa Rais ni kukidhi vigezo vya kikatiba zaidi, kwa kwa kuwa umoja ni nguvu.
 
Naomba kufahamishwa inawezekana vipi mtu mwenye wadhifa wa Umakamu wa Rais kukaa nje ya nchi kwa mwezi mmoja eti kwa shughuli maalumu.?

Hata Katibu Mkuu tu wa wizara ni nadra kuweza kukaa mwezi mzima, sasa iweje kwa Makamu wa Rais?

Ni kazi gani hiyo?

Makamu wa Rais anaweza kuwa mtendaji wa kuwa na kazi ya kumuweka nje ya nchi kwa mwezi mzima?

Kwa nafasi yake, ni msaidizi wa Rais, mtu wa kusimamia sera, sasa nini kinaweza kumuweka nje ya nchi kwa muda wote huo?

Maswali ni mengi kuliko majibu.
Utakuwa na umri mdogo, Kikwete na Mkapa wakiwa marais walikaa nje ya nchi kwa zaidi ya miezi miwili na waliporudi shughuli zikaendelea kama kawaida.
 
Makamu wa raisi ni mtu mkubwa sana. Taarifa kwamba yuko wapi ninafiiri ni muhimu kujua. Ninadhani there was something wrong somewhere that why Higher Authority didn't disclose his whereabouts. Hayo tuwaachie wakubwa.
 
Hapa kuna wanaotaka iwe makamu wa Rais alikuwa mgonjwa, na wengine wanasema hakuwa mgonjwa alikuwa nje kwa shughuli maalum.

Naamini hiyo yote inasababishwa na nafasi yake aliyonayo, watu wana haki ya kuhoji wapi alipo kiongozi wao, serikali inayosababisha ligi kwa kutuficha sababu ya kutoonekana kwake ndio inatukosea.

Makamu wa Rais ana bahati mbaya sijui kwanini haya makelele humkuta yeye, nakumbuka hata wakati ule wa Magufuli pia aliletwa kuongea na waandishi wa habari huku hali yake ikiwa haijakaa sawa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Sema anapenda kuficha ugonjwa wakati haiwezekani kwa nafasi aliyonayo.
 
VP siyo mali ya Umma.

Hakuna binadamu anamiliki binadamu.

Siyo kila kitu unaweza ukaambiwa kuhusu kiongozi wako; huna haki ya kujua hali na kila kitu cha kiongozi.

Kuhusu afya yake, hilo ni juu yake aidha akuambie ama asiseme au aseme kidogo.

Hata ukijua afya yake wewe inakusaidia nini? Unampa panado, au ni kutaka umbeya tu!
Hiyo panadol anayomeza nanunua mimi mlipa kodi, kwahiyo kuhoji ni halali ya kila raia wa nchi hii.
 
Hapa kuna wanaotaka iwe makamu wa Rais alikuwa mgonjwa, na wengine wanasema hakuwa mgonjwa alikuwa nje kwa shughuli maalum.

Naamini hiyo yote inasababishwa na nafasi yake aliyonayo, watu wana haki ya kuhoji wapi alipo kiongozi wao, serikali inayosababisha ligi kwa kutuficha sababu ya kutoonekana kwake ndio inatukosea.

Makamu wa Rais ana bahati mbaya sijui kwanini haya makelele humkuta yeye, nakumbuka hata wakati ule wa Magufuli pia aliletwa kuongea na waandishi wa habari huku hali yake ikiwa haijakaa sawa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Na bado hayuko sawa!!
 
Utajua mwenyewe kama kwenu unapoenda hospitali unaaga kwamba wenda kazini. Ua ukirudi toka hospitali ndugu hwakujulii hali bali salam yao ni pole kwa kazi maalum 🤣
hata wewe unaweza kua mgonjwa maalum na ukapatiwa matibabu maaluumu.
 
Back
Top Bottom